DOKEZO Uhalifu umezidi sana mji wa Tunduma, Serikali iingilie kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nahisi madini yanafanya mji uchangamke kwa haraka.

Maendeleo yanakuja na wivu mwisho kuzaa uhalifu.

Serikali inafuatilia hili.
 
Kuna wakati tulikuwa hapo silver stone Hotel, kuna jamaa alikuja alidai aliibiwa hela,sim na kipondo juu
Kwenye kuwafatilia jamaa walikuwa washavuka upande wa nakonde wenyewe chocho wanazijua

Ova
Hiyo Hotel wateja wake walikua wanasomewa ramani karibu siku nzima hasa wale wanaowahi bus za daslm au kachelewa kufika maana hotel zinazoizunguka hiyo Silver Hotel ni zile za bei ndogo humo ndio walikua wanalala hao wezi...mimi nilikua nalala Upande wa Nakonde Hotel za Watanzania huku Tunduma labda uwe dereva wa truck wanajua huyu hata posh hana...
 
Kweli kabisa mkuu,wapo bize kutafuta pesa.
 
Ukitaka kuona kuwa askari wako kazini beba magendo yako Tunduma alafu tembea usiku utacheka sana .

Ukiwakosa mpemba , basi wapo mayenje kote uko wapo kama mia wanataka chochote kitu

Ila usipobeba chochote basi unaweza kuwalipua na wao maana hawana muda na wewe wanahisi wewe ni mfu tu.

Sasa huo ndiyo mwanya wa wahuni kuwafunza adabu watu wema.

Ila yote kwa yote wana usalama wa Tunduma wana njaa sana
 
Aisee mkuu umenena.
 
Pole sana kamanda naelewa unachosema hali ya Tunduma haifai kabisa
 
Pole Sana Kuna kitu kinatakiwa kieleweke vema KAZI ya Jeshi la Wananchi siyo kupambana na uhalifu ni Sawa na kubadili Rubani Kuwa dereva wa Magari makubwa.
Kupambana na wahalifu kunahitaji kuzingatia na kuifuata sheria ya mwendo wa Makosa ya jinai lakini kupambana na adui wa kivita ni tofauti kabisa na mkikosea wanajeshi wa Jwtz wakaingia kukamata vibaka mtazalisha kitu kipya cha ukiukwaji wa haki za Binadamu.

Pamoja na mmomonyoko wa maadili Kwa Jamii lakini vyombo vyetu vya Dola vipo duni Sana sina hakika kama wanatosha.

Vyombo vya kutoa haki vimejaza watu wasiomuogopa Mungu wanashirikiana na wahalifu kunyang'anya haki za Raia mfano Mimi nimepata dhuruma moja mpaka nawaza kujitoa muanga mbele ya Hakimu mmoja hapo Tunduma.

Kipindi hiki ambacho majukwaa ya kutoa kero zetu yameanza ni nafasi yetu kutoa ya Moyoni ili viongozi waweze kutusaidia.
 
Tunduma ukitaka kuishi maisha malefu kaa mbali na wake za watu, siasa, na kuingilia Mishe za watu ,utaniambia brother

Utaishi kwa amani lakini uliyo yaongea hapo yote nikweli
Na Yana tendeka

pale nihatari nashauri ulicho shauri pia

tatizo pale pesa mingi Mishe mingi jpm alijaribu lakini ndiyo hivyo aka pewa R.i.p
 
Tunduma kuuwa wanaita ku kashelee
mpango wanaita kipengele

pale ukiokota Hera mtu akija akisema nimekuona umeokota Hera twende sehem tukagawane
mwambie staki mgao nakupa zote
Ukithubutu kuwaskiliza walicho kushauri tuta wapa pole nduguzako kwa msiba

kiukweli ni mji uliontawaliwa ma mama mafia na umafia mwingi

Sema usiwe mtu wa kufuatitilia Mambo ya watu
 
Sawa mkuu,lkn pole pia kwa yaliyokusibu.
 
Uko sahihi,huo mchezo mchafu upo sana.
 
Kweli unaweza kuwa mbali na yote uliyoweka hapo,lkn bado watu wakawa wanakufuatilia kutaka kujua mishe zako na wakishajua tu,ndio wanakutengenezea kipindi sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…