Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo Hotel wateja wake walikua wanasomewa ramani karibu siku nzima hasa wale wanaowahi bus za daslm au kachelewa kufika maana hotel zinazoizunguka hiyo Silver Hotel ni zile za bei ndogo humo ndio walikua wanalala hao wezi...mimi nilikua nalala Upande wa Nakonde Hotel za Watanzania huku Tunduma labda uwe dereva wa truck wanajua huyu hata posh hana...Kuna wakati tulikuwa hapo silver stone Hotel, kuna jamaa alikuja alidai aliibiwa hela,sim na kipondo juu
Kwenye kuwafatilia jamaa walikuwa washavuka upande wa nakonde wenyewe chocho wanazijua
Ova
Kweli kabisa mkuu,wapo bize kutafuta pesa.Tunduma ni hatari sana usiku hapo...Manjagu usiku wanakua kwenye dili za kukamata magendo kwa hiyo kuona wakizunguka usiku mitaa ya makazi labda waanze kipindi hiki gari zao huwa zinategwa chini pale kuelekea bara bara ya Mpemba ili wapate ridhiki yao ya usiku...
Hapana sio mkinga.We sio mkinga?
Yaani ni hatari mno.Nimesikia hata Sogea maeneo ya makambini napo hali si shwari nyakati za usiku.
Aisee mkuu umenena.Ukitaka kuona kuwa askari wako kazini beba magendo yako Tunduma alafu tembea usiku utacheka sana .
Ukiwakosa mpemba , basi wapo mayenje kote uko wapo kama mia wanataka chochote kitu
Ila usipobeba chochote basi unaweza kuwalipua na wao maana hawana muda na wewe wanahisi wewe ni mfu tu.
Sasa huo ndiyo mwanya wa wahuni kuwafunza adabu watu wema.
Ila yote kwa yote wana usalama wa Tunduma wana njaa sana
Makambi ya nn hayoNimesikia hata Sogea maeneo ya makambini napo hali si shwari nyakati za usiku.
Pole sana kamanda naelewa unachosema hali ya Tunduma haifai kabisaWapendwa habari za Jioni? Bila kupoteza muda, Mji huu wa Tunduma ni mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Sasa lengo la Uzi huu ni kuiomba Serikali yetu pendwa ya Mama Dkt.Samia Suluhu Hassani, kuwa kupitia vyombo vya Ulinzi na Usalama watusaidie, Mambo yenyewe yako hivi.
Watu wanatekwa na kupigwa vibaya na kisha kuporwa kila kitu, Wakati Mwingine Muhanga huachiwa majeraha mazito au kuaga Dunia Kabisa.
Kuna visa kadhaa, Mojawapo ilihusu mimi mwenyewe siku ya Jumapili ya tarehe 15/01/2023, mida ya saa tano usiku hivi nilivamiwa kukiwa kumebaki hatua chache kufika nyumbani na watu wawili, ambao walikuwa wamevalia Mask wakanipiga sana nikapiga kelele lkn wapi, Mungu ni mwema nikawaponyoka Baada ya purukushani kali.
Kuna Jamaa yangu alivamiwa hivyo hivyo na kundi kubwa la Vijana wakamdhuru na kumnyang'anya vitu vyake.Matukio ni mengi sana.
USHAURI WANGU KWA SERIKALI.
1.Tunduma ingepewa uangalizi maalumu kiusalama km ambavyo imefanyika huko Tarime, kwa kuundiwa Kanda maalumu. Hii itasaidia sana kuweka hali ya usalama kwani ni mji wa Kibiashara hivyo usalama mkubwa ni suala nyeti ili kuwaondole hofu Wafanyabiashara na hivyo kukuza biashara na Serikali kujikusanyia mapato mengi.
2. Iwekwe kambi ya jeshi km ilivyo kwenye mipaka mingi ya Kagera na Kigoma.
3. Ifanyike operasheni kabambe ya kuteketeza wahalifu km zilivyowahi kufanyika baadhi ya Operasheni siku za nyuma,Mfano mzuri ni ile Operesheni iliyoongozwa na Kamanda Saimoni Siro kule Kagera na Kibiti,Ambao wahalifu wengi walipata cha mtemakuni.
4. Wananchi wahamasishwe kutoa taarifa za Siri kwa jeshi la Polisi na kuwe na utaratibu kutunza taarifa hizo za Siri,na Kuwe na posho hata Kidogo kwa Wananchi wazalendo.
5. Serikali za mitaa ziwabaini vijana wanaoshinda bila kazi maalumu na kisha ziwabane ili kujua wanawezaje kumudu maisha ili hali hawana shughuli maalumu.
Mwisho tuzidi kuomba Mungu, atunusuru na hali hii maana hali si shwari kabisa.
Ni sisi Wananchi wanyonge wa Tunduma.
Panaitwa makambini ila sijui ni makambi ya nini. Wenyeji wa Sogea Tunduma wanaelewa.Makambi ya nn hayo
Sogea na mpakani kuanzuia saa 2 Ni hatari tupuNimesikia hata Sogea maeneo ya makambini napo hali si shwari nyakati za usiku.
Tunduma kuuwa wanaita ku kasheleeYaani iwekwe kambi ya jeshi kwa sababu ya vibaka? Jeshi unalichukulia poa sana inaonekana.
Sema iundwe kanda maalum ya kipolisi. Hiyo ni kazi ndogo sana.
Hao vibaka ni mnaoshinda nao na labda hata kununuliana msosi.
Asilimia kubwa ya uhalifu wa hivyo hutekelezwa na wazawa wachache wa eneo husi
Sawa mkuu,lkn pole pia kwa yaliyokusibu.Pole Sana Kuna kitu kinatakiwa kieleweke vema KAZI ya Jeshi la Wananchi siyo kupambana na uhalifu ni Sawa na kubadili Rubani Kuwa dereva wa Magari makubwa.
Kupambana na wahalifu kunahitaji kuzingatia na kuifuata sheria ya mwendo wa Makosa ya jinai lakini kupambana na adui wa kivita ni tofauti kabisa na mkikosea wanajeshi wa Jwtz wakaingia kukamata vibaka mtazalisha kitu kipya cha ukiukwaji wa haki za Binadamu.
Pamoja na mmomonyoko wa maadili Kwa Jamii lakini vyombo vyetu vya Dola vipo duni Sana sina hakika kama wanatosha.
Vyombo vya kutoa haki vimejaza watu wasiomuogopa Mungu wanashirikiana na wahalifu kunyang'anya haki za Raia mfano Mimi nimepata dhuruma moja mpaka nawaza kujitoa muanga mbele ya Hakimu mmoja hapo Tunduma.
Kipindi hiki ambacho majukwaa ya kutoa kero zetu yameanza ni nafasi yetu kutoa ya Moyoni ili viongozi waweze kutusaidia.
Uko sahihi,huo mchezo mchafu upo sana.Tunduma kuuwa wanaita ku kashelee
mpango wanaita kipengele
pale ukiokota Hera mtu akija akisema nimekuona umeokota Hera twende sehem tukagawane
mwambie staki mgao nakupa zote
Ukithubutu kuwaskiliza walicho kushauri tuta wapa pole nduguzako kwa msiba
kiukweli ni mji uliontawaliwa ma mama mafia na umafia mwingi
Sema usiwe mtu wa kufuatitilia Mambo ya watu
Kweli unaweza kuwa mbali na yote uliyoweka hapo,lkn bado watu wakawa wanakufuatilia kutaka kujua mishe zako na wakishajua tu,ndio wanakutengenezea kipindi sasa.Tunduma ukitaka kuishi maisha malefu kaa mbali na wake za watu, siasa, na kuingilia Mishe za watu ,utaniambia brother
Utaishi kwa amani lakini uliyo yaongea hapo yote nikweli
Na Yana tendeka
pale nihatari nashauri ulicho shauri pia
tatizo pale pesa mingi Mishe mingi jpm alijaribu lakini ndiyo hivyo aka pewa R.i.p
Asante mkuuPole sana mkuu