DOKEZO Uhalifu umezidi sana mji wa Tunduma, Serikali iingilie kati

DOKEZO Uhalifu umezidi sana mji wa Tunduma, Serikali iingilie kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yaani iwekwe kambi ya jeshi kwa sababu ya vibaka? Jeshi unalichukulia poa sana inaonekana.

Sema iundwe kanda maalum ya kipolisi. Hiyo ni kazi ndogo sana.

Hao vibaka ni mnaoshinda nao na labda hata kununuliana msosi.

Asilimia kubwa ya uhalifu wa hivyo hutekelezwa na wazawa wachache wa eneo husika.
Haya yote ni majeshi yetu ya ulinzi. Sioni tatizo wakutumika hasa kipindi hiki ambacho tuna amani ya kutosha na nchi majirani zetu. Nawasifu sana mikoa ya Katavi na Kigoma kwa sababu wao huwatumia sana JW kwenye operesheni/doria za kukabiliana na wavamizi na waharibifu wa misitu ya hifadhi na wanyama pori. Imesaidia sana kuwadhibiti hawa majangili na wavamizi wa maliasili zetu, ambao wengine ni jeuri, majatili na wana mpaka silaha za moto.
 
Sasa km jeshi la Polisi limezidiwa, kuna ubaya gani wa kuomba jeshi litusaidie?
Jeshi la Wananchi sio kazi yake kuzuia vibaka acha kujitoa ufahamu. Kazi za migambo inayoshika rungu na kuvaa tisheti ndio unataka ijengwe kambi ya jeshi. Yani tujenge kambi kisa vibaka wanaopiga roba? Kuwa serious na vipaumbele vya nchi.
 
Kutokuwa na kazi maalum siyo kigezo Cha kuwa mhalifu. Wapo wenye mahela Yao lakini ni wahalifu wakuu, ndiyo wenye makundi hayo.

Kwa hiyo tutumie vigezo vya kuwabaini wahalifu wenyewe. Tusikate vidole kwasababu ya Funza Mkuu.
 
Back
Top Bottom