Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

kawambwa.jpg


MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa.

Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wanafunzi 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137,

  • wa shule wakiwa 397,136 huku
  • wa kujitegemea wakiwa 68,806.

“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla:

waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao


  • wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33

  • wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67
​lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.
Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo.

Ufaulu kwa madaraja
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata

Daraja la kwanza ni 1,641,


  • wavulana wakiwa 1,073 na
  • wasichana 568,

Daraja la pili ni 6,453,


  • wavulana wakiwa 4,456 na
  • wasichana 1,997.

Waliopata daraja la tatu ni 15,426,


  • wavulana 10,813 na
  • wasichana 4,613, waliopata wa

Daraja la nne 103,327,


  • wavulana 64,344 na
  • wasichana 38,983 huku

Daraja
sifuri wakiwa 240,903,


  • wavulana 120,664 na
  • wasichana 120,239.

Shule 20 bora
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wizara ilitaja shule 20 zilizofanya vizuri badala ya 10 kama ilivyozoeleka, kati yake 18 zilikuwa za watu binafsi na mashirika ya dini na mbili za Serikali. Shule hizo ni pamoja na


  1. St.Francis Girls ya Mbeya,
  2. Marian Boys ya Pwani,
  3. Feza Boys ya Dar es Salaam,
  4. Marian Girls ya Pwani,
  5. Rosmini ya Tanga,
  6. Canossa ya Dar es Salaam,
  7. Jude Moshono ya Arusha,
  8. St. Mar’s Mazinde Juu ya Tanga,
  9. Anwarite Girls ya Kilimanjaro na
  10. Kifungilo Girls ya Tanga. Nyingine ni
  11. Feza Girls ya Dar es Salaam,
  12. Kandoro Sayansi Girls ya Kilimanjaro,
  13. Don Bosco Seminary ya Iringa,
  14. St. Joseph Millenium ya Dar es Salaam,
  15. St. Iterambogo ya Kigoma,
  16. St. James Seminary ya Kilimanjaro,
  17. Mzumbe ya Morogoro,
  18. Kibaha ya Pwani,
  19. Nyegezi Seminary ya Mwanza na
  20. Tengeru Boys ya Arusha.

Shule 10 za Mwisho
Kwa upande wa shule 10 za mwisho, iliyofanya vibaya zaidi ni


  1. Mibuyuni ya Lindi,
  2. Ndame ya Unguja,
  3. Namndimkongo ya Pwani,
  4. Chitekete ya Mtwara,
  5. Maendeleo ya Dar es Salaam,
  6. Kwamndolwa Tanga,
  7. Ungulu Morogoro,
  8. Kikale ya Pwani,
  9. Mkumba na
  10. Tongoni za Tanga.

Matokeo yaliyofutwa
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu na kuandika matusi. Baadhi ya udanganyifu huo ni karatasi za majibu kuwa na mfanano usio wa kawaida, kukamatwa na simu za mkononi kwenye chumba cha mtihani, kukutwa na karatasi au madaftari pamoja na kubadilishana karatasi za majibu.


Waziri akwepa
Kabla ya kutangaza matokeo hayo, Waziri Kawambwa alitumia muda mwingi kuzungumza sababu za yeye mwenyewe kuamua kutangaza matokeo hayo badala ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mirihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako kama ilivyozoeleka. “Najua kila mtu ana shauku ya kusikia matokeo leo, naona mkimwangalia Katibu (Dk Ndalichako) hapa, lakini mimi kwa kujua jambo hili, nimeona kwa nini nimbebeshe jukumu hilo zito wakati waziri mwenyewe mwenye dhamana hiyo nipo! Ndiyo nimekuja niwape matokeo haya,” alisema Dk Kawambwa.


Baadaye Dk Kawambwa aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikuwa na haraka hivyo asingekuwa na muda wa kujibu maswali, huku akitumia muda mwingi kuzungumza mambo yaliyokuwa nje ya matokeo aliyotarajiwa kuyasoma. Pia alikwepa kujibu maswali ya msingi likiwamo kutaja majina ya wanafunzi bora pamoja na majina ya shule 10 bora zenye wanafunzi chini ya 40 akisema anajua umuhimu wa kueleza mambo hayo, lakini wataalamu wake wamekwepa kuandika kila kitu katika taarifa hiyo kwa kile alichoeleza kukwepa kuwa na taarifa ndefu. Taarifa iliyosomwa na waziri kwa waandishi ilikuwa na karatasi nne.

Ufaulu mwaka 2011
Kwa mujibu wa matokeo ya mwaka 2011, ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule ulionyesha kuwa
watahiniwa 33,577 sawa na asilimia 9.98 walifaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu.



  • [*=1]Wasichana waliofaulu katika daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 10,313 sawa na asilimia 7.13 na

    [*=1]wavulana 23,267, sawa na asilimia 12.13.
Waliopata daraja la nne mwaka huo walikuwa 146,639 sawa na asilimia 43.60.


  • [*=1]Wavulana 87,039 sawa na asilimia 45.40 na

    [*=1]wasichana 59,600, sawa na asilimia 41.22 huku
Waliofeli wakiwa 156,089 sawa na asilimia 46.41, kati yao


  • [*=1]wavulana wakiwa 81,418 sawa na asilimia 42.47 na

    [*=1]wasichana 74,667, sawa na asilimia 51.64.

Dk Kawambwa alisema matokeo ya watahiniwa 28,582 yamezuiwa kwa sababu ya kutolipa ada ya mtihani na wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja.


Matokeo ya QT
Dk Kawambwa alisema waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) walikuwa 21,310,
wasichana 13,134 na
wavulana 8,176
Waliofanya ni 17,137 sawa na asilimia 80.42... “Watahiniwa 5,984 kati ya 17,132 waliofanya mtihani huo wamefaulu.”

 
Nawasalim kwa heshima na taadhima! Nimekuwa nikitafakari juu ya matokeo ya kidato cha nne 2012 kwa usiku mzima pasipo majibu,nilikuwa nasikiliza redio one asubuhi, nimesikia wakisema sababu ya kufeli nusu ya watahiniwa wote imetokana na ukosefu wa maabara na walimu! Hanitii akilini kwani tuna mifano dhahiri ya shule zenye walimu wa kutosha na maabara lakini mtoke dvs0 niwengi kuliko 1,2,3,na4. Nakumbuka hotuba ya Rais wakati wa mgomo wa waalimu dhihaka na dharau alizo zisema na kuwaita waalimu mbayuwayu, anayeona mshahara hautoshi aache kazi, athari za mgomo wa madaktari ni kubwa kuliko za mgomo wa waalimu kwani waalimu hata mkigoma mtarudi namtafundisha, madhara amboyo pia aliyaona kwa mwanae mwenyewa wa kumzaa.UKWELI SERIKALI WEKENI PAMBA MASIKIONI ILA UKWELI UTABAKI PALEPALE, WAALIMU BADO WAPO KWENYE MGOMO AMBAO MGOMO HUU, NI HATARI HATA KULIKO WA MADAKTARI.NAOMBA SIASA NA ELIMU VISICHANGAMANE.
 
Na tabasamu analipataje?
Kuna watu nawatamani sana jinsi wanavyochukulia mambo.
 
Tunashukuru ndugu kwa taarifa nzuri ya kiuchambuzi. Kiukweli kama kweli Waziri Kawambwa ameguswa na Matokeo hayo basi hana budi kujiuzuru.
 
Kwa hali ilivyo..ts better hata kawambwa ajiuzulu, atawafuta wengi machozi..
 
kazi ipo! hawapeleki watoto mwao shule za kata! ila watoto wa wenzao ndio wamewajaza huko, rubbish!
 
Technically, Division IV wanaangukia kwenye kundi la walio feli. Na ukijumlisha Division IV na wale wa Zero, unapata 93% ya wanafunzi waliofanya mtihani wamefeli. 93% failure! Heads must roll!
 
Tusubilie maandamano tena ya waslimu kwa ndalichako, kwani 20 bora hakuna shule yao kabisa..... lakin sijui kwani wanaandamana wakat shule zao wanafundishwa sana elimu ya dini kuliko masomo mengne wanategemea waongoze yani waganafurahisha sanaaaaaaaaaaaaaa....

~ Utawasikia mfumo kirstu
~ Wamefaulu wakirstu na shule zao wakati hamis na asha usoma hapo
~ Anaeongoza baraza ni mkirstu wakat watendaj weng ni wasilamu
~ Wamesaisha vibaya somo la uisilmu wakati wataalum hawana plus mitaala wakulifundisha somo hili lakin wataalamu wanojua uislam wapo weng na ndio ufundisha

Yani nchi yangu tamu sana, hongelen shule 20 bora endele kuweka misingi bora ya elimu musijibizane nao.....
 
Dharau zenu kwa walimu ndo zinawapa matokeo hayo. Haya nani mjanja hapo?
 
ndugu zangu, maisha tulionayo ni magumu, kwani nguvu kazi ya taifa inategemea wasomi sasa tutapata wataalam kutoka wapi wakati taifa letu linazalisha daraja la 4 na 0? mimi nadhani wizara ya elimu ni kivuli, waziri ni shadow!!!! hivyo yapaswa tufanye mageuzi ya kweli ktk nyanja zote za maisha ya binadamu na tuwekeze katika elimu, tutafakari kwa umakini, na tutoe muongozo yakinifu wa tanzania ijayo..
 
Sio mgomo wa walimu ni matoto yetu yamezidi umcharuko eti toto la form one lina bwana ujue ni vichekesho. La saba limeshatolewa bikra,mara maviduku,mara watsapp,fb na n.k.
 
Ngoja kesho kuyasikia ni kazi ya Ndalichako.

Ifikie hatua..kama inawezekana, hizo paper baada ya kusahishwa ziwe zinarudishwa kwa wanafunzi au hata kwenye vituo vya mitihani! ndiyo tuwaamini NECTA.
 
Jumla

[TD="class: xl67, width: 90"]Division[/TD]
[TD="class: xl67, width: 65"]F[/TD]
[TD="class: xl67, width: 70"]M[/TD]
[TD="class: xl67, width: 67"]Totals[/TD]
[TD="class: xl68, width: 6"][/TD]
[TD="class: xl67, width: 64"]F[/TD]
[TD="class: xl67, width: 64"]M[/TD]
[TD="class: xl67, width: 64"]Totals[/TD]

[TD="class: xl64"]Div I[/TD]
[TD="class: xl65"] 568 [/TD]
[TD="class: xl65"] 1,073 [/TD]
[TD="class: xl65"] 1,641 [/TD]

[TD="class: xl66, align: right"]0.2%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]0.3%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]0.4%[/TD]

[TD="class: xl64"]Div II[/TD]
[TD="class: xl65"] 1,997 [/TD]
[TD="class: xl65"] 4,456 [/TD]
[TD="class: xl65"] 6,453 [/TD]

[TD="class: xl66, align: right"]0.5%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]1.2%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]1.8%[/TD]

[TD="class: xl64"]Div III[/TD]
[TD="class: xl65"] 4,613 [/TD]
[TD="class: xl65"] 10,813 [/TD]
[TD="class: xl65"] 15,426 [/TD]

[TD="class: xl66, align: right"]1.3%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]2.9%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]4.2%[/TD]

[TD="class: xl64"]Div IV[/TD]
[TD="class: xl65"] 38,983 [/TD]
[TD="class: xl65"] 64,344 [/TD]
[TD="class: xl65"] 103,327 [/TD]

[TD="class: xl66, align: right"]10.6%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]17.5%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]28.1%[/TD]

[TD="class: xl64"]Div Zero[/TD]
[TD="class: xl65"] 120,239 [/TD]
[TD="class: xl65"] 120,664 [/TD]
[TD="class: xl65"] 240,903 [/TD]

[TD="class: xl66, align: right"]32.7%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]32.8%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]65.5%[/TD]

[TD="class: xl70"] 166,400 [/TD]
[TD="class: xl70"] 201,350 [/TD]
[TD="class: xl70"] 367,750 [/TD]

[TD="class: xl69, align: right"]45%[/TD]
[TD="class: xl69, align: right"]55%[/TD]
[TD="class: xl69, align: right"]100%[/TD]

[TD="class: xl63"][/TD]
[TD="class: xl63"][/TD]
[TD="class: xl63"][/TD]

[TD="class: xl64"]Waliofanya[/TD]
[TD="class: xl65"] 166,400 [/TD]
[TD="class: xl65"] 201,350 [/TD]
[TD="class: xl65"] 367,750 [/TD]

[TD="class: xl66, align: right"]42.7%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]51.7%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]94.4%[/TD]

[TD="class: xl64"]Hawakufanya[/TD]
[TD="class: xl65"] 14,090 [/TD]
[TD="class: xl65"] 7,730 [/TD]
[TD="class: xl65"] 21,820 [/TD]

[TD="class: xl66, align: right"]3.6%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]2.0%[/TD]
[TD="class: xl66, align: right"]5.6%[/TD]

[TD="class: xl70"] 180,490 [/TD]
[TD="class: xl70"] 209,080 [/TD]
[TD="class: xl70"] 389,570 [/TD]

[TD="class: xl71, align: right"]46.3%[/TD]
[TD="class: xl71, align: right"]53.7%[/TD]
[TD="class: xl71, align: right"]100.0%[/TD]
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wallah kazi ipo! Mimi hata sijui hii elimu ya TZ inaelekea wapi kwa sababu graph ya ufaulu wa wanafunzi inashuka kila miaka ikienda mbele mwisho wa siku watakao faulu div I-III watakua 20 tena sio elfu 23


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom