Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

ukichanganya Azania, jangwani, zanaki na makongo div 1 hazifiki 50.
 
Lakini wapiga kura wengi watakua ni wale walio baki mitaaani na waliopata division zero.....

Sidhani kama target yao ndio hiyo walifikiri vema katika hili....
 
Pamoja na mambo mengine kinachowafelisha watoto wetu ni utandawazi usiokuwa na nidhamu. Mwalimu anatakiwa achangie 25% tu. Kama mtoto akiwa anaenda shule yuko busy na simu (facebook, na muziki kwa earphones), akiwa shuleni vivyo hivyo na kuota jua, akiwa anarudi home hivyo hivyo na akiwa nyumbani tamthilia tunategemea nini. Ni hatari kudhani kuwa walimu pekee wanafaulisha. Kwa tabia tegemezi na "starehe wanazopenda" hawa vijana wakifaulu hata Mungu "ATASHANGAA". Hakuna elimu bila nidhamu
 
Hizi ndo impacts za kuwadharau waalimu.. Matokeo ya mgomo wa waalimu ndo haya..
Yes 12+12=1212 halafu mwalimu huyohuyo ndo unamchukua kwenda kumark mitihan

Kila sector ina uwalakini! ukianza na NECTA mpaka MOEVT
 
Wazazi wawajibike kwanza ndio suluhisho. Wewe mzazi halafu hujali mwenendo wa mwanao, unataka uje umlaumu nani?
 
Samahan wakuu hv kwenye haya matokeo mtu akiwekewa
E ina maana gan? Naomba kufahamishwa wakuu.
 
Walimu waliofeli kidato cha nne na sita hawawezi kufaulisha juu ya kiwango walichofaulu wao.
 
Lakini wapiga kura wengi watakua ni wale walio baki mitaaani na waliopata division zero.....

Sidhani kama target yao ndio hiyo walifikiri vema katika hili....
ni kweli unalosema ila kwakuuwa tumezoea kujisifia kwa namba hiyo wanaweza kuitumia kama kigezo kwamba watoto wote wa masikini wamepata mkopo 100 percnt.
 
necta wametangaza matokeo..jamani watu wamefeli sana, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi..hali ni tete!

Hongera kwa waliofaulu, waliofeli ni wao kujipanga sana.

Kwa mujibu wa habari hii chini, tunaweza kusema:

kati ya wanafunzi 397,136 waliofanya mtihani; 240,750 walipata sifuri!
- division i - 1,641 => 0.41%
- division ii - 6,453 => 1.62%
- division iii - 15,426 => 3.88%
- division iv - 103,327 => 26.02%
- division 0 = [397,136 - (1,641+6,453+15,426+103,327)] -> 270,289 => 68.06%

tuache kuwawowa hawa wanetu wa kike kwa kuwadobo;lesha na ipad na bbery
 
Swala si matokeo, mwenendo mzima wa elimu yetu kwa sasa asiyeuona kama unakasoro huyo ni kipofu.

utambulisho wako wa jina humu JF na unachochangia havina mahusiano kabisa, swala la mtu kufikia hitimisho kabla hata ya kujua kinachoendelea ndio tamaduni na desturi ya watanzania.

tiririsha hoja za msingi ndio ulete hitimisho, sio kukaa kulalamikia serikali kila siku kupitia chama tawala, wakati mitoto yenu haipendi kusoma na wala wazazi hamtoi msukumo kwa watoto kusoma. Unadhani serikali itakugongea hodi kuja kumuhamasisha mwanao apende kusoma? wote tumepitia mazingira hayo hayo maguju, lakini tumetimiza malengo yetu.
 
Haya sasa kuanzia matokeo ya darasa la saba,kidato cha pili na sasa kidato cha nne nani zaidi kati ya Serikali na Walimu?

Naomba kuwasilisha!
 
necta wametangaza matokeo..jamani watu wamefeli sana, hiki kizazi sijui kinaelekea wapi..hali ni tete!

Hongera kwa waliofaulu, waliofeli ni wao kujipanga sana.

Kwa mujibu wa habari hii chini, tunaweza kusema:

kati ya wanafunzi 397,136 waliofanya mtihani; 240,750 walipata sifuri!
- division i - 1,641 => 0.41%
- division ii - 6,453 => 1.62%
- division iii - 15,426 => 3.88%
- division iv - 103,327 => 26.02%
- division 0 = [397,136 - (1,641+6,453+15,426+103,327)] -> 270,289 => 68.06%
kama taifa halina mtaala waelimu unategemea nini? Hakuna waalimu ,vitabu wala maabara mnategemea wafaulu kwa nguvu za kiza? Kwanza nawapongeza sana waliofeli na waliofaulu. Bungeni tukisema sana tunaambiwa wakorofi wadogo zetu wakifeli hawasoni kipindi cha kampeni
tutatatua matatizo ya wananchi.
 
yaani naona mwelekeo wa elimu hapa nchini inasuasua sana kwasababu serikali aina sera ambayo ni endelevu .they are not concreate at all in their education system,they keep on changing every now and then.
 
vipi ile somo ya dini imewekewa alama, isije zua mzozo baadae
 
Walimu zaidi, Serikali kuweni wapole kwa walimu jamani hali ni mbaya!
 
Mi nazani walimu kwa shule za msingi na sekondari waangaliwe madai yao ili kupunguza aibu kwa taifa ambalo tunaenda kupata wasomi wasiokuwa na vigezo.
 
utambulisho wako wa jina humu JF na unachochangia havina mahusiano kabisa, swala la mtu kufikia hitimisho kabla hata ya kujua kinachoendelea ndio tamaduni na desturi ya watanzania.

tiririsha hoja za msingi ndio ulete hitimisho, sio kukaa kulalamikia serikali kila siku kupitia chama tawala, wakati mitoto yenu haipendi kusoma na wala wazazi hamtoi msukumo kwa watoto kusoma. Unadhani serikali itakugongea hodi kuja kumuhamasisha mwanao apende kusoma? wote tumepitia mazingira hayo hayo maguju, lakini tumetimiza malengo yetu.
Naomba nikuwekee ujumbe wangu niliouweka face book jana kukuthibitishia kwamba ninatambua kuwa shule inahitaji washikadau wanne muhimu, serikali, wanafunzi, walimu na wazazi, lakini kiliochangu ni kwamba serikali haijatekeleza wajibu wake ipasavyo, kwanza rejea maelezo ya Kawambwa jana, nafahamu kabisa kuwa uzaifu wa elimu nchini hauwezi kuongelewa kwa kigezo kimoja tu, lakini kwa nini serikali ya ccm juzi ilitupilia mbali hoja binafsi ya Mbatia?

[h=5]From facebook page,
Matokeo ya kidato cha nne 2012 ni ujumbe tosha kwa serikali na jamii kwa ujumla.

Hatimaye leo Baraza la Taifa la Mitahini Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanywa mwaka jana.

Haisaidii sana kukueleza idada ya watahiniwa, shule zilizoongoza na majina yao, kikubwa nilichokiona mimi MATOKEO HAYO NI MABAYA wala hakuna haja ya mtu atuambie njano ni nyekundu na nyekundu ni njano, kwa mfano inasikitisha sana pale unapopitia shule unakuta ukijumlisha DIV I hadi IV idadi yake haifikii hata nusu ya wale waliopata DIV 0, na kwa haraka unaweza kukuta shule tano ukijumlisha idadi ya DIV I hazifiki hata kumi.

Hii ni aibu kwa serikali na nchi yetu kwa ujumla, serikali yapasa iangalie sekta hii kwa jicho la pekee hasa maslahi na mazingira ya walimu, pili wazazi washirikiane na walimu kuhakikisha wanasimamia vyema myenendo ya watoto wao badala ya kuachia jukumu lote kwa walimu, vilevile inapasa tujiuluze je idadi kubwa ya vijana hawa wanakwenda wapi baada ya hapa?[/h]
 
Back
Top Bottom