Uhamiaji ianze uchunguzi jinsi watoto wa Lissu, ambao ni raia wa Marekani walipata passport za Tanzania, kama Lissu alidanganya, ashughulikiwe

Siasa zimeharibu sana akili za watanganyika......siasa imefubaza akili za watanganyika.......siasa zimewafanya watu kuwa mazezeta.....

Yaani kwa sababu za kisiasa kila mtu anauona ubaya kulingana na aliyetenda ubaya na sio kwa uhalisia wa ubaya wenyewe......

Yaani mtu uzuri au ubaya wa jambo au kitu unategemea umetendwa na nani na sio ubaya wenyewe......na wanasiasa wetu wanatuona kama makatuni.....

Wafuasi wa vyama wanashindana mabaya baada ya kuyakemea mabaya.......utamsikia mbona wale hamuwakamati........

Siasa zetu zimeegemea kwenye ushabiki zaidi na sio weledi ndio maana tunawaona wanasiasa wetu kama miungu watu........

Wafuasi wamekabidhi akili zao Kwa viongozi wao...wao vichwa vyao vimegeuka mabox ya kuhifadhia maoni na utashi wa viongozi wao......ndio maana wanaweza kuambiwa kuwa kiongozi fulani hafai na wakamtukana lakini wafuasi hao hao wanaambiwa anafaa na wanamsifia.......


Ni rahisi sana kuzimudu siasa za TANZANIA wewe tengeneza tu mazezeta yako tu yanayokuabudu na kukutetea na uweze kucheza na matukio basi umemaliza...........

Wakati mwingine unawatazama wafuasi wa wanasiasa na unawatazama wanasiasa wenyewe unabakia tu kucheka.......
 
Hao watoto wana umri gani??
 
Wengi tumewaona na tunawaona wakipaa uraia mwingine wakifika 18 years old. Hasa watoto wa wakubwa.

Uraia Pacha sio issue kubwa kivile kwenye dunia ya sasa.
 
Ukizaliwa Marekani wewe ni raia wa Marekani upende usipende kwa hiyo ni muhimu kutumia akili kidogo unapozungumzia urai pacha
 
Msameheni jamani,, sawa najua nchi yetu hairusu uraia pacha labda alidaganya kwa kutojua tu sheria, asamehewe tu, kisha achague anataka awe mmarekani au mtanzania🤷🏾‍♂️
Angalia katiba ya Tanganyika kabla ya CCM ndio inakupa haki hayo mengine ni porojo
 
Nia ya haya maandiko ni nini kumkomoa Lisu au kuelimisha Watanzania?? Kama ni kuelimisha naomba nikusaidie mtoto akizaliwa Marekani ni mmarekani awe na passport au hana ni Marekani.

Mwanamke yeyote akiolewa na mwanaume ambae nchi yake ina mfumo dume yule mwanamke na watoto wake ni raia wa nchi ya mumewe kwa hiyo hata kama ana passport ya Tanzania haimzuii kuwa raia nchi ya mumewe
 
humohumo uhamiaji kuna wanyarwanda kibao nani atawachunguza?
 
Mkuu, hiyo pressure itafupisha maisha yako.
 
Ile roho ya mauaji bado mnayo tu? Huyu mtu kawakosea nini? Mwanzo mlitaka kutoa roho yake Mungu kamlinda, kaibuka ibilisi mwingine anataka roho za watoto wake, hebu mwacheni huyu mtu, mateso aliyopitia yanatosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…