Uhamiaji ianze uchunguzi jinsi watoto wa Lissu, ambao ni raia wa Marekani walipata passport za Tanzania, kama Lissu alidanganya, ashughulikiwe

Mleta mada labda ungetuambia kwanza hao watoto wa Lisu walikua na uraia wa USA kabla ya kua na uraia wa Tanzania? Na je kwa hivi sasa wana uraia wa nchi mbili kwa pamoja?
 
Akili mgando hizi.
 
Uraia pacha uruhusiwe tu Ili tukuze uchumi, wabongo kibao wanataka kuwekeza home nje ni pa kutafuta walichukua pasipoti za nje Ili iwe rahisi kupata kingi.
Wanaweza kuwekeza kama wawekezaji
Kipi kinachowashinda?
Ndio ujue waliopo nje wengi shughuli zao ni za kijungu jiko[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Wanaweza kuwekeza kama wawekezaji
Kipi kinachowashinda?
Ndio ujue waliopo nje wengi shughuli zao ni za kijungu jiko[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Kibali na gharama za uwekazaji sio pesa kidogo,pili unaishi kwa kibali KILA baada ya miaka 2 unaomba tena.
 
Kijana Fanya kazi umiliki vyakoo atakama wanae watakuwa wana uraia wa nje ila haiondoi haki za lisu kumuliki ardhi, kumiliki kitu chochote kisheria maana yeye si RAIA wa marekani bali wanae na haki zote alizostaili kuzipata ni zake kwaiyo Fanya kazi upate pesa uachane na roho mbaya inayokuandama

Sent from my Infinix X571 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza hao watoto waweza kuwa raia wa Matekani kwa kuzaliwa.
Nijuavyo mke wa Lissu aliwahi kuishi na kusoma Us
Marekani wanatumia Juis soil
Bongo tunatumia juis sanguine

Hapa hatuwezi kufanana
 
Umeme unakatika hovyo unakuja na hoja za passport za Watanzania wenzio kisa unawajua wakati hizi Nchi za Afrika karibu nyingi Wahindi na watu wa Bara la Asia wanazitumia vizuri wakimaliza mambo yao wanaendelea na mishe zingine...
 
Tanzania inavitu vingi vya kushughulikia, imagine wewe ni Lissu na umepigwa risasi USALAMA wake na WA familia yake ni WA muhimu kuliko chochote let them be where they Wana be, it's their freedom and right to chose what they chose
 
Umeme unakatika hovyo unakuja na hoja za passport za Watanzania wenzio kisa unawajua wakati hizi Nchi za Afrika karibu nyingi Wahindi na watu wa Bara la Asia wanazitumia vizuri wakimaliza mambo yao wanaendelea na mishe zingine...

Mkuu ninasikitika sana sasa tumezoea shida na hatuoni ni tatizo ndio maana tunaongelea vitu visivyo na faida
 
Kibali na gharama za uwekazaji sio pesa kidogo,pili unaishi kwa kibali KILA baada ya miaka 2 unaomba tena.
Ndio gharama ya kukana uraia wako wa nchi ya asili kwa faida binafsi za kiuchumi.

Mtu kama huyu hawezi kuwa na uchungu na bongo ila anaweza kutumika vibaya au kutumiwa vibaya kama wakala kwa sababu siku zote yeye ana option ya second home.

Gharama sio kubwa kwa raia wa kigeni tusidanganyane ila wengi shughuli zao ni kijungu jiko
 
Hao watoto wanaumri chini ya miaka 22! Bado wanasoma wameweza vipi kumiriki ardhi?

Unasema wamekuwa wakifaidi pesa ya nchi, bongo, pesa ipi? Kama walikuwa wakifaidi wakati Bado ni wabongo, ni haki yao?

Yaani mtu kutafuta uraia wa nchi nyingine, na kuukana uraia wake wa awali, we unaona ni ufisadi? akili huna kabisa, kila mtu duniani ana haki ya kubadilisha uraia, passport zao za bongo, zipo USA, zifste pale ubalozini.

Kuna ufisadi unapigwa kwenye SGR, umeme, mafuta, na gesi, mbuga zetu,
Ila wewe kwa kuwashwa unamuona lisu tu!!
 
Lissu aliwakosea nini jamii hii?
Ukifuatilia wote wanaomshambulia ni jamii moja tu
 
Wewe unamsemea huyo ambae sio kiongozi hata wa nyumba 10 na wakati kuna wageni wengi kwenye safu za uongozi wa serikali ya mboga mboga kuanzia chini kabisa ambao ni wageni na wanasumbua watanzania kwa raha zao
 
Wewe utafaidika nini katika hili?

Watoto waliozaliwa nje ya nchi na wazazi watanzania wanakuwa na uraia wa nchi hii mpaka pale watakapofikia miaka 18 ndiyo wanaamua wenyewe kuwa waendelee na uraia wa nchi hii au wawe raia wa nchi ile waliyozaliwa.

Sasa hao watoto waliokula bajeti yako ya elimu na afya ni haki yao kwani wazazi wao nao wanalipa kodi.
 
Wako under 18 ya konyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…