Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Idara ya Uhamiaji nchini imefafanua kuwa huduma zake za kimfumo zimerudi katika hali ya kawaida baada ya changamoto iliyosababisha ucheleweshaji wa baadhi ya maombi ya wananchi, na kueleza kuwa mbombaji hatakiwi kulipia huduma mara mbili.
Akizungumza kuhusu suala hilo, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Paul John Mselle, amesema kuwa ni kweli mfumo ulipata changamoto iliyosababisha baadhi ya maombi kuchelewa, lakini kwa sasa hitilafu hiyo imetatuliwa na huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida.
Kuhusu hoja iliyotolewa na Mdau wa JamiiForums.com kuwa aliniandikisha tangu Februari 2026 kwa ajili ya kupata Passport katika Kituo cha Uhamiaji Arusha, lakini aliporejea hapo ameambiwa taarifa zake zimefutika na anatakiwa kulipia tena ili kupata huduma ya Pasi ya kusafiria.
Hoja ya awali ~ Uhamiaji Arusha wanasema maombi yetu ya Passport hayaonekani kwenye mfumo, wanasema tulipie tena
Mselle amesema licha ya mfumo kusumbua hapo awali lakini hakuna taarifa zilizofutika za Mwananchi yeyote, zote zipo, pia Uhamiaji haijatoa agizo lolote la jumla linalomtaka mwananchi aliyeishalipia huduma kuanza mchakato upya na kulipia tena.
Amesema "Taarifa za watu zipo na wanaendelea kuhudumiwa. Kama kuna mtu ana changamoto ya namna hiyo, hiyo itakuwa ni changamoto yake binafsi (case ya mtu mmoja mmoja) na sio suala la jumla.
“Inapotokea hali hiyo Mwananchi akatakiwa kulipia mara ya pili anatakiwa kuwasilisha maombi ya kurejeshewa malipo yake ya awali kwa njia halali za Kiserikali, akifika kwenye kituo chetu chochote atapewa maelekezo," amesema.
Aidha, ametoa wito kwa Wananchi kuwa muombaji yeyote anayekutana na changamoto kama hiyo, ikiwemo kuambiwa alipie upya au kwamba taarifa zake hazionekani, kutochukua hatua hiyo badala yake afike haraka kwenye Ofisi ya Afisa Uhamiaji wa Mkoa husika ili changamoto yake binafsi iweze kushughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi.