Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Mimi naona uhamiaji inalaumiwa bure. Je, huyo mama alikuwa na na passport ya Africa Mashariki akakataliwa kuendelea na safari? Tukitunga sheria lazima tuzifuate. Hatuwezi kuchagua sheria ipi ifuatwe na ipi isifuatwe. Huyu mama angekuwa na makaratasi yanayotakiwa angeendelea na safari. Kwanza unajuaje ni kweli anaenda Kenya. Unajuaje ni Mrundi. Kwa nini hakuwa na passport? Je huko Kenya angeingiaje bila passport? Si angeisha kurudishwa mpakani. Kama alipata uchungu na kwenda Nyasho Clinic, si ni afadhali kuliko kupatia uchingu ndani ya gari ambapo huduma ya ukunga hakuna?
Huelewi kitu ,Tuliza kichwa Kwanza.

Uhamiaji wa Kwanza ilikuaje wakamuruhusu kuvuka mpaka?(Burundi -Ngara)

2. Umejua chanzo cha uchungu huo?

3. Uhamiaji hawezi kuwa na Sheria zinaweza kusaidia kwa watu kama hao?

4. Passport atatoa wapi hata hela ya chakula nyumbani imeshindikana.
 
Mama mjamzito ametoka Burundi kwenda Kwa mume wake Kenya Juzi tarehe 25/02/2022.Alivyofika Musoma alikamatwa na uhamiaji sehemu ainayoutwa Kurumuli(Barrier) .Alijitetea kwa uchungu Sana mpaka tulio kuwa kwenye gari lile tulipata huruma.

Mama alijitetea kuwa anaenda Kenya kujifungulia huko kwa mchumba aliyempa ujauzito ,asingeweza kujifungulia kwao maana hana msaada na hata hivyo hajapata chakula tangu aanze Safari akitokea Burundi Kupita mpaka wa BURUNDI na NGARA na hata hivyo alijitetea kwenye mpaka huo na akasikilizwa.

Afisa wa uhamiaji Musoma hakutaka kabisa kusikiliza na hakujali hali ya mama yule.Alishikiliwa mpaka akapata labour pain(Uchungu) akakimbizwa Kituo cha AFYA NYASHO .

Mama hakuwa na chochote hata nguo hana ,kibaya zaidi alipaswa kufanyiwa upasuaji kwa sababu alipata uchungu pingamizi.

Maafisa uhamiaji waliomleta wakatokomea na hata walipotafutwa hawakuwa na msaada ,maana kituo hawakuwa na vifaa vya kama surgical gloves,Dawa za baada na kabla ya upasuaji,drip n.k

Watumishi wa kituo hiki walichanga pesa wakamsaidia.Leo yuko wodini hata chakula anapewa na wagonjwa wenzie.Hana nguo anatumia mashuka ya Kituo.

"Hivi uhamiaji pamoja na Sheria za nchi kwa Hali kama hiyo hawakuwa na chakufanya kuanzia kwenye ukamataji"???
Sas mtu Kama kweli huna nyaraka unavukaje vukaje kwenda point a na b kienyeji HV mbna wazungu hawana mzaah wa namna hi yetu ya kiafrica.

Unajuwa kbsa kuwa huna nyaraka unaamaama kienyeji Kama kuku mtu akibanwa mnakuja huku kutafuta huruma kwetu sijaona kosa la afsa uamiaji mm Yuko sahih as long amefata Sheria iliyopo

Mam yule angerudishwa tu ndio chanzo viongoz wanakuja kuzaliwa kina jiwe Kam inavyodaiwa kuwa Ni mmburundi jiwe
 
Mipaka ya wakoloni imetufanya waafrika tuishi kwa ubaguzi mkubwa sana sio sawa basi tu
 
clinician Mimi nilikuwa nasafiri nikitokea Mwanza kwenda TARIME alivyosushwa kwenye gari abilia tulipatwa hasira zilizo changanyika na huruma .Kesho yake nilikuwa naenda MUSOMA MJINI huko nilipata full story ya mama huyo.Nilifika mpaka kituo cha Afya Nyasho kumuona anatia huruma sana hata Kiswahili hajui vizuri
Sas wee unaona kbsa yule mam Yuko sahih kuvuka boda Bila nyaraka muhimu hpn angetulia kwao tu jama ake amfate siyo kuwateza viumbe
 
clinician Mimi nilikuwa nasafiri nikitokea Mwanza kwenda TARIME alivyosushwa kwenye gari abilia tulipatwa hasira zilizo changanyika na huruma .Kesho yake nilikuwa naenda MUSOMA MJINI huko nilipata full story ya mama huyo.Nilifika mpaka kituo cha Afya Nyasho kumuona anatia huruma sana hata Kiswahili hajui vizuri
Yaani ulienda Tarime, ukarudi Musoma na kwenda Nyasho kuona tu? Wewe huruma yako iko wapi? Ulimsaidiaje huyo mama.

Yote hii ni umbea usiyo msingi. Wala hukushuhudia hili. Umetunga stori ya kukamatwa.

Hujui kuwa raia pia tuna nafasi ya kujitolea kusaidia, sio kwenda kuangalia unafikiri unatalii na kisha kueneza uzandiki.
 
Mimi naona uhamiaji inalaumiwa bure. Je, huyo mama alikuwa na na passport ya Africa Mashariki akakataliwa kuendelea na safari? Tukitunga sheria lazima tuzifuate. Hatuwezi kuchagua sheria ipi ifuatwe na ipi isifuatwe. Huyu mama angekuwa na makaratasi yanayotakiwa angeendelea na safari. Kwanza unajuaje ni kweli anaenda Kenya. Unajuaje ni Mrundi. Kwa nini hakuwa na passport? Je huko Kenya angeingiaje bila passport? Si angeisha kurudishwa mpakani. Kama alipata uchungu na kwenda Nyasho Clinic, si ni afadhali kuliko kupatia uchingu ndani ya gari ambapo huduma ya ukunga hakuna?
Jama. Uko sahih Sana watanzania wnajifanyaka wako na huruma kumbe Ni wanafiki eti achiwe apite vipi sasa huku huna nyaraka huyu uhamiaji wako sahihi Bila kujali unaujauzito au laah" nchii hii inachezewa Sana in jiwe voice"
 
Acha wehu wewe Inanisaidia nini mi kuwa chadema au ccm kama wewe uko ofisi hiyo Acha kupora watu taratibu si zipo kwa watu wa namna hiyo
Ukisika uongo ndiyo huu. Nafikiri wewe ni CHADEMA.
 
Yaani ulienda Tarime, ukarudi Musoma na kwenda Nyasho kuona tu? Wewe huruma yako iko wapi? Ulimsaidiaje huyo mama. Yote hii ni umbea usiyo msingi. Wala hukushuhudia hili. Umetunga stori na kukamatwa. Hujui kuwa raia pioa tuna nafasi ya kujitolea kusaidia, sio kwenda kuangalia unafikiri unatalii na kisha kueneza uzandiki.
Chief, acha kukurupuka soma vizuri sikuenda MUSOMA Kwa ajili ya mama huyo. Nilienda Musoma Kwa Issue zangu mwenyewe nilivyofika MUSOMA nikakuta story hiyo mtaani.

Bahati nzuri nilikuwa naye nikakumbuka ilivyokuwa. Nilifika NYASHO baada ya kusikia, Chief nimetoa msaada kwa mama huyo Kadiri ya uwezo wangu siyo lazima niandike msaada niliyoutoa .

Unaweza kuwasiliana na Mganga mfawidhi wa kituo hicho utapata full story
 
Kila tukio lina makusudi yake.naamini asingezuiliwa hapo angekutwa na hali hiyo akiwa polini sijui.angekuwaje.

Waliomzuia walikua na baya labda lakini kumbe ndio msaada kwake.

Uhamiaji walimsaidia bila ya kujua wanamsaidia.

Huyo mtoto atakua ni mwenye bahati sana katika maisha yake.
 
Huyo muongo tu. CHADEMA huyo
Kiongozi kwasasa dunia ni kama Kijiji na wewe CCM, hushindwi kupata ukweli kutoka MUSOMA .

Mganga mkuu yupo, Mganga mfawidhi yupo. Unaweza kupata maelezo kutkea huko. Kwanini uniite muongo bila kupata ukweli U au uongo upande wa pili?
 
Kila tukio lina makusudi yake.naamini asingezuiliwa hapo angekutwa na hali hiyo akiwa polini sijui.angekuwaje.

Waliomzuia walikua na baya labda lakini kumbe ndio msaada kwake.
Uhamiaji walimsaidia bila ya kujua wanamsaidia.
Huyo mtoto atakua ni mwenye bahati sana katika maisha yake.
Umeelewa chanzo cha uchungu kwa huyo mama?
 
Kuna ofisi moja ya uhamiaji wakiwakamata watu wa namna hiyo (wasio raia) huwapiga sana na kuwanyang'anya fedha zao wanazokuwa wamezipata katika kufanya kazi aidha wakiwa wanarudi nchini kwao au wakiwa wameingia nchini kwetu katika utafutaji.
Sasa ninapofanyia kazi ni karibu na ofisi hiyo Sasa wakiwa wanawapiga wanatoa kilio cha uchungu sana utakuta mtu anapigwa zaidi ya masaa matatu roho yangu huwa inaugua sana kwa kusikia vilio vile.
Baada ya kuwapiga huwapora fedha zao na kuwaachia warudi nchini kwao huku hawana nauli wala hela ya chakula, uhamiaji fuateni taratibu zenu za kazi tafadhari

Taja ni wapi ili usaidie.
 
Kila tukio lina makusudi yake.naamini asingezuiliwa hapo angekutwa na hali hiyo akiwa polini sijui.angekuwaje.

Waliomzuia walikua na baya labda lakini kumbe ndio msaada kwake.
Uhamiaji walimsaidia bila ya kujua wanamsaidia.
Huyo mtoto atakua ni mwenye bahati sana katika maisha yake.
Uko sahih lkn Sheria zizifunjwa ili watu wajiondokee kienyejienyeji
 
Chief taratibu achana uvyama ,tujikite kwenye hoja .

Pointi yangu ni ,

1.Kwanini Uhamiaji hawakuhusika na kusaidia matibabu ya mama huyu hata kama ni mhamiaji haramu ?Je,Kuna ubinadamu ulipaswa kufika katika hili?
Hakuna muhamiaji haramu ndani ya Africa kumbuka mipaka imewekwa na wakoloni
 
Back
Top Bottom