Uhamiaji naomba muwamulike Wanaijeria walio Tanzania

Uhamiaji naomba muwamulike Wanaijeria walio Tanzania

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2019
Posts
1,952
Reaction score
4,416
Niwape pongezi Idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kazi nzuri mnayozidi kuifanya.

Ila kuna vitu vidogo mnahitaji kuvifanyia kazi. Kuna wimbi kubwa la vijana wa Nigeria wapo humu nchini wanafanya biashara ambazo hazieleweki.

Unakuta mNigeria eti anashona nguo. Kuna tukio moja limetokea Kidimbwi mwezi mmoja nyuma ambako waNigeria walinunua chupa 100 za champagne aina ya Moet na kugawia watu hovyo.

Bei ya Moet ni 250,000/= Hawa vijana wa Nigeria inabidi wachunguzwe maana sasa hivi wanaenda mbali na kujificha kwenye kujifanya wameoa dada zetu wa kiTanzania.

Lingine ni kuhusu hawa raia wa kigeni wanaopewa Business visa wakati wanafanya kazi ambazo wazawa pia wanaweza kufanya. Hili pia kwakweli tunawaomba muliangalie kwa umakini sana.
 
Mikoa ya Pembezoni haswa Kigoma wamejazana Raia wa kigeni amabo hawana vibali vya kufanya kazi,
Kuna wimbi la raia wa Burundi na DRC.
ni vyema mikoa ya mipakani ikapewa uangalizi wa hali ya Juuuuu maana wahalifu hugeuza mikoa hiyo kuwa chimbo.
 
Utaratibu ni ule ule, ukitaka kukaa nchi ya ugeni ili kupata urahisi fulani fulani OA dada zao. Hii formula imesaidia sana.

Kuhusu scamming, kweli serikali iwe macho ila kumbuka unapokua nchi ya ugeni akili inachangamka kwa sababu only way to survive ni kuhakikisha akili iko active muda wote😃😃.

Kuna “pahala” Nigerians wameni-inspire sana
 
Kuna mmoja yuko mwanza anauza spea used za magari, nadhani sheria za JF hazikubali kutaja majina. Aisee huyu tunaita wa mwisho, spea ya 40000 ukienda kwake anakutajia laki moja kama hutaki sepa. Yaani ukienda kwake, unaeza amua kupaki gari tu
 
Niwape pongezi Idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kazi nzuri mnayozidi kuifanya.

Ila kuna vitu vidogo mnahitaji kuvifanyia kazi. Kuna wimbi kubwa la vijana wa Nigeria wapo humu nchini wanafanya biashara ambazo hazieleweki. Unakuta mNigeria eti anashona nguo. Kuna tukio moja limetokea Kidimbwi mwezi mmoja nyuma ambako waNigeria walinunua chupa 100 za champagne aina ya Moet na kugawia watu hovyo. Bei ya Moet ni 250,000/= Hawa vijana wa Nigeria inabidi wachunguzwe maana sasa hivi wanaenda mbali na kujificha kwenye kujifanya wameoa dada zetu wa kiTanzania.

Lingine ni kuhusu hawa raia wa kigeni wanaopewa Business visa wakati wanafanya kazi ambazo wazawa pia wanaweza kufanya. Hili pia kwakweli tunawaomba muliangalie kwa umakini sana.
Unateseka ukiwa wapi?
Tafuta hela....na ukizipata, hutaona kuna wanaijeria wanagawa moet......
 
WanaJeria wanaiba kwa njia ya Mtandao, wanaweza kuwa Tanzania lakini Mpunga unapigwa Dubai, Taiwan nk lkn ukiwaona wamejazana mahala tambua kuna mifumo dhaifu ya Kimtandao na Ulinzi kwa Ujumla.
All in all hao jamaa siyo wa kukaribishwa
 
Back
Top Bottom