Uhamiaji naomba muwamulike Wanaijeria walio Tanzania

Uhamiaji naomba muwamulike Wanaijeria walio Tanzania

Ni wivu, gubu na akili ya kimasikini a.k.a wanyonge ndio mnawaona wanaigeria, sababu mpo mpo tu vijiweni na kuzurura mjini bila shughuli badala kujishughulisha..... muuza duka Mangi hawaoni, muuza mazao kutoka mikoani hawaoni na sisi mbona hata hatuwaoni......
 
Kwani kuna kipengele kinasema business visa ni kwaajili ya kazi ambazo wazawa hawawezi kufanya??

Hakuna hilo business visa ina kanuni zake na sio eti hiyo biashara iwe wazawa hawawezi maana hadi sasa watz tunaweza kila kitu

Point yangu ni kwamba “work permit” wanaogopa kuziomba kwa sababu unakuta hiyo kazi na mzawa anaweza kufanya. Kwahiyo wanaomba business visa ambazo zipo renewable kila miezi 3.
 
ENDAPO WAPO KIHALALI NA WANAFANYA SHUGHULI KIHALALI HAKUNA TATIZO LOLOTE,TUACHE CHUKI NA WIVU TUJIFUNZE KUTOKA KWA ON HOW THEY DO?, TO GET A LOTS OF MONEY HALAL.
 
Niwape pongezi Idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kazi nzuri mnayozidi kuifanya.

Ila kuna vitu vidogo mnahitaji kuvifanyia kazi. Kuna wimbi kubwa la vijana wa Nigeria wapo humu nchini wanafanya biashara ambazo hazieleweki.

Unakuta mNigeria eti anashona nguo. Kuna tukio moja limetokea Kidimbwi mwezi mmoja nyuma ambako waNigeria walinunua chupa 100 za champagne aina ya Moet na kugawia watu hovyo.

Bei ya Moet ni 250,000/= Hawa vijana wa Nigeria inabidi wachunguzwe maana sasa hivi wanaenda mbali na kujificha kwenye kujifanya wameoa dada zetu wa kiTanzania.

Lingine ni kuhusu hawa raia wa kigeni wanaopewa Business visa wakati wanafanya kazi ambazo wazawa pia wanaweza kufanya. Hili pia kwakweli tunawaomba muliangalie kwa umakini sana.
Kwa Sasa nchi inamatundu kila kona. Wengi wanaingia na kutoka wapendavyo. Uhamiaji ya Leo sio ya mwaka mmoja uliopita.
 
WanaJeria wanaiba kwa njia ya Mtandao, wanaweza kuwa Tanzania lakini Mpunga unapigwa Dubai, Taiwan nk lkn ukiwaona wamejazana mahala tambua kuna mifumo dhaifu ya Kimtandao na Ulinzi kwa Ujumla.
All in all hao jamaa siyo wa kukaribishwa
Uhamiaji wapo wapo tu! Ila waambie Kuna kiongozi fulani wa CHADEMA sio raia, fasta!!!
 
Niwape pongezi Idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kazi nzuri mnayozidi kuifanya.

Ila kuna vitu vidogo mnahitaji kuvifanyia kazi. Kuna wimbi kubwa la vijana wa Nigeria wapo humu nchini wanafanya biashara ambazo hazieleweki.

Unakuta mNigeria eti anashona nguo. Kuna tukio moja limetokea Kidimbwi mwezi mmoja nyuma ambako waNigeria walinunua chupa 100 za champagne aina ya Moet na kugawia watu hovyo.

Bei ya Moet ni 250,000/= Hawa vijana wa Nigeria inabidi wachunguzwe maana sasa hivi wanaenda mbali na kujificha kwenye kujifanya wameoa dada zetu wa kiTanzania.

Lingine ni kuhusu hawa raia wa kigeni wanaopewa Business visa wakati wanafanya kazi ambazo wazawa pia wanaweza kufanya. Hili pia kwakweli tunawaomba muliangalie kwa umakini sana.
Hahaha ungejua wana hadi vitanbulisho vya Nida huku watz hawana ndo ungeshangaa
 
Mwingine huyu huku,watu wamekaa kikuda kudaaaa tu siku hizi si mfanye mambo yenu kwani mnaijeria akiwa hapa nchini wewe unapungukiwa nini?

watu wanafanya biashara ziwe halali au haramu Serikali n wajibu wake kuwafatlia,eti umeumia watu kugaiwa Moet,huo unaonyesha ni wivu wa kimaskini.

Kwahyo hizo moet uliwapa hao wanaijeria hela wakaenda nunulia au walitumia pesa zao? kwanini msijifunze kutafuta pesa na nyie vijana acheni kuendekeza Chuki zisizo na maana.

Umewaona wanaijeria tu hii nchi,wachina huwaoni,wahindi je wote hao huwaoni pelekesha kule roho lako baya.
 
Watu weusi kwa wivu hatujambo...hpo kilichokuuma ni hizo moet wa si lingine
 
Kuna mmoja nilikutana nae dar akataka kuniingiza mkenge, alikua nakaa hotelini tu na alikua na kifaa cha kutengeza pesa fake, alinipa pesa za kubadilisha currency pasipo kujua ni fake, yani ni watu wakuwa nao makini sana, pesa sio chini ya milion na ilikua ni biashara nimefanya nae stupid
 
Watimuliwe haraka, hao watu ni kama Kansa ukiwachekea wanasambaa kwa kasi na kuwatoa itakua ni vigumu.
 
Tusiwe kama Wasouth Africa, tujitume, hakuna mtu atachukua nafasi yako ikiwa wewe una vigezo vya kuajirika kushinda huyo Mgeni. Huu ni mwanzo wa chuki kwa wageni.
Nenda Malawi kuna wabongo kibao na hawasumbuliwi, haya mambo tuwaachie wale maboya wa Afrika Kusini.
 
Kuna mmoja yuko mwanza anauza spea used za magari, nadhani sheria za JF hazikubali kutaja majina. Aisee huyu tunaita wa mwisho, spea ya 40000 ukienda kwake anakutajia laki moja kama hutaki sepa. Yaani ukienda kwake, unaeza amua kupaki gari tu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom