Uhamiaji ni jeshi au idara ya kawaida?


Haya tofautisha sheria hizo kwa lugha na malkia kama zinafanana
 

Attachments

Haya tofautisha sheria hizo kwa lugha na malkia kama zinafanana
Huna hoja ya msingi katiba Sect 147(4) cap 9 imetaja majeshi ya ulinzi kwa kuyataja majina kabisa kuwa ni Jeshi la ulinzi, Jeshi la polisi, Jeshi la magereza na Jeshi la kujenga taifa na hivyo ndo seniority ya majeshi pia ilivyo 1.Jwtz, 2. Polisi, 3. Magereza 4.Jkt haya ya hoja yako ya kingereza hiyo siyo sheria, otherwise leta kifungu cha sheria kwenye katiba kinachosema siyo majeshi
 
Mtoa mada kwenye post namba 4 kamaliza kila kitu nafikiri na imeeleweka, kwenye sheria kutambulisha hivyo vyombo hawajatumia neno moja linalofanana kwa vyote so hoja yake ina mantiki ya kutosha tu! Ingekua majeshi yangepata amri toka kwa rais lkn kwa kuwa sio IGP na mwenzie wanamrisha kwa barua. I rest my case
 
Mbona hauna hoja mkuu? Unavyosema ingekua ni majeshi yangepata amri kutoka kwa Rais kwani wao amri huwa wanatoa kwa nani?

Majeshi yote yanapokea amri kutoka kwa Rais ambae yeye ndo Amiri jeshi mkuu, na hawa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao ni CDF, CPF(IGP), CGP(mkuu wa magereza) wote wanakua Appointed na Rais na akiamua kuwatoa anawatoa muda wowote na anawapa maelekezo moja kwa moja wao wanashusha kwa subordinates wao.
 
Unaonekana bado kinda, anyway I rest my case, watakujibu wengine kuongezea!
 
Jeshi kwa lugha ya kiingereza ni military full stop. Si sahihi kabisa kutumia neno jeshi kwa vyombo vya kiraia kama magereza, polisi, uhamiaji na zimamoto.
Vipi kuhusu Army
USA Army
Chinese liberation army

Unajua kama sisi tuna TPDF na sio army?
 
Jeshi kwa lugha ya kiingereza ni military full stop. Si sahihi kabisa kutumia neno jeshi kwa vyombo vya kiraia kama magereza, polisi, uhamiaji na zimamoto.
Nakubaliana nawe. Bora lingekuwa hata paramilitary
 
Jeshi halipokei amri toka kwa rais bali amiri jeshi mkuu. Magereza, uhamiaji, polisi, zimamoto na usalama viko chini ya rais.

Kuna rais na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi(hakuna usalama). Hivyo rais na amiri jeshi ni mtu yule yule kama alivyo akiwa kwenyekiti wa chama lakini hapo ni ofisi tofauti. Kwenye ofisi ya amiri jeshi mkuu ni Jeshi tu, hakuna such thing kama magereza, uhamiaji au polisi.
 
Ficha hii wenye akili wasione
 
Sasa kati yangu mimi naekuletea hoja na ushahidi wa kisheria na wewe unaeleta hoja za vijiweni nani kinda?
Yani hizo tafsiri za mwigulu ndo sheria? Utakua karani wa mahakama za mwanzo nini? Sheria hizo hapo zote tatu kiongozi, unless zilishafutwa. Jeshi halijawahi kuitwa "service"
 

Attachments

Jeshi kwa lugha ya kiingereza ni military full stop. Si sahihi kabisa kutumia neno jeshi kwa vyombo vya kiraia kama magereza, polisi, uhamiaji na zimamoto.
NChi zetu ni zile unaweza ukazi category kama Jungle countries, zenyewe vyombo vya kutoa huduma kwa raia wamevigeuza kuwa majeshi
 
Anayetoa commission kwa wanajeshi sio rais bali ni amiri jeshi japo kibinadamu ni mtu yule yule. Hata unaposoma habari zinazotolewa na Jeshi hutumia jina la amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi kwa sababu akiwa kwenye shughuli za jeshi haendi kama rais bali kama amiri jeshi japo urais wake anakuwa nao.
 
NChi zetu ni zile unaweza ukazi category kama Jungle countries, zenyewe vyombo vya kutoa huduma kwa raia wamevigeuza kuwa majeshi
Hilo ni tatizo. Unakuta hata mkuu wa mkoa au hata waziri kwenye sakata mfano la watu kutekwa anakwambia wameviachia vyombo vya ulinzi na usalama wafanye kazi yao. Unajiuliza kama mkuu wa mkoa au waziri anaelewa alichokisema. Sasa kama mti hajui hata vyombo vya ulinzi ni vipi na vya usalama ni vipi unadhani akiwa kiongozi mkubwa ataweza kujua wapi mamlaka yake yanaanzia na kuishia? Ndio unakuta wanashauri Jeshi lijihusishe na uchaguzi kwa sababu hawafahamu Jeshini ni nini na majukumu yake ni yapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…