Uhamiaji ni jeshi au idara ya kawaida?

Uhamiaji ni jeshi au idara ya kawaida?

Salamu, ili taasisi iitwe jeshi means ina uwezo wa ku-access silaha mbalimbali pia Ina kikosi maalumu ndani yake.

Mfano magereza wao Wana K, police wao Wana FFU na jwtz Wana makomandoo.

Je, Hawa uhamiaji wame-qualify kuitwa jeshi? Wana silaha? Wana special forces? Ikitokea mikiki wanaweza kupambana wenyewe?

Pia Wana kambi? Kama hivyo hawana why raia wanaliita jeshi? Kwa Nini wanasalimiana "sijambo afande"? Na kupigiana salute?

Nasubiri majibu.
Na jeshi la uhifadhi je?
 
Paramilitary ni muundo unaofanana na Jeshi kuanzia muundo wa utawala, mafunzo na matumizi ya silaha kubwa. Haiwezekani mamlaka inayoshughulika na mambo ya kiaraia ikapewa jina hata la paramilitary ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Ndiyo maana awali nilikubaliana nawe.
Paramilitary inahusisha mafunzo mengi YANAYOFANANAFANANA na ya kijeshi. Chuo kama Mweka na Pasiansi ni mfano wa mafunzo hayo lakini wahitimu bado si WANAJESHI!
Au wasemaje?
 
Yani hizo tafsiri za mwigulu ndo sheria? Utakua karani wa mahakama za mwanzo nini? Sheria hizo hapo zote tatu kiongozi, unless zilishafutwa. Jeshi halijawahi kuitwa "service"
Mwigulu ndo katafsiri katiba? Unafikiri neno Service lilikua gumu sana kutafsiri kwa kiswahili? Mbona rahisi sana kwenye katiba wangeandika "Idara ya polisi, Idara ya magereza / huduma ya polisi, huduma ya magereza kwani kuna ugumu gani kuandika hivyo kwenye katiba na wakaandika jeshi? Mbona Immigration iliitwa Idara ya uhamiaji?

USA yenyewe kila jimbo polisi inaitwa Idara utakutana na LAPD, NYPD, CPD, PPD , kwanini Tz hazijaitwa idara? Ni kwasababu nchi inaendeshwa na katiba na kwenye katiba yametajwa kuwa ni majeshi, sasa kaniletee katiba yako nyingine iliyokataa kuwa siyo majeshi
Screenshot_20241201_140128_Word Office - Docx Viewer.jpg
 
View attachment 3166635
Brother I got P number and I know what I am talking, anyway!
 
Anayetoa commission kwa wanajeshi sio rais bali ni amiri jeshi japo kibinadamu ni mtu yule yule. Hata unaposoma habari zinazotolewa na Jeshi hutumia jina la amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi kwa sababu akiwa kwenye shughuli za jeshi haendi kama rais bali kama amiri jeshi japo urais wake anakuwa nao.
Same same! Ntu anakuwaje amiri jeshi kabla hajawa rais?
 
Haya maneno yatawavuruga daima
Military
Army
Force
Service
Department
Agency

Lazima tukubaliane jeshi ni nini?
Hayo maneno Yana athari yoyote kwenye utendaji kazi wao?

Magereza ni jeshi ila wanajiita Tanzania Prison Service, je service inaathiri utekelezaji wa majukumu Yao?

Jeshi la kujenga Taifa ni National Service, inawapunguzua wao ujeshi wao?

Tanzania Police Force na Fire and Rescue Force ni majeshi au la!
Ukiwaita Service itaathiri utendaji wao?

Kama neno force sio jeshi basi tukubaliane Tanzania hakuna jeshi Bali Kuna vikosi tu either vya ulinzi au usalama. Maana TPDF ni Tanzania people's defense forces.

Kama force ni nguvu na sio jeshi basi tukubaliane kwenye hoja kwamba hatuna jeshi, kama sivyo tukubaliane hayo tajwa ni majeshi whether ni service au force.

Tuje kwenye Immigration ni jeshi au lah?
Kwanza kirefu chake ni Tanzania Immigration Service Departmental
Kwanza tunaona Service ndani yake kama yalivyo majeshi ya magereza na kujenga Taifa.

Pili ilifanyika hivyo Ili kutoonyesha kwa wageni sisi ni ujeshi ujeshi ila hakuna sababu ya msingi, nje ya siasa.

Ni jeshi kamili kwa mujibu wa Sheria iliyoianzisha na kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Kuna ibara inasema Raisi na Amiri jeshi mkuu wa Tanzania anaweza kuanzisha jeshi kutokana na uhitaji.

Ni jeshi pekee lenye kazi za ulinzi, usalama, intelejensia na diplomasia.

Wana kazi za huduma kama kutoa pasipoti, vibali na control ya wageni ndani ya nchi.

Wana kazi za ulinzi hasa maeneo ya mipakani na doria kwenye vipenyo, kuhakikisha mipaka ya nchi ni salama.

Achana na maeneo ya kuingia na kutoka hasa ambako intelejensia kubwa inakusanywa.

Kuna mtu anauliza kama wana kikosi maalumu?
KMU kipo na kinaopareti kwa namna yake.

Ni jeshi kwa mujibu wa muundo wake na majukumu waliyonayo, ndio maana hawajabadilisha Sheria Yao.

Siraha nzito mpaka ukute wana vifaru?

Tiss
Tanzania intelligence security services Hawa ni mashushu na nature ya kazi zao ni ushushu na covert operations
Ulitaka wajiite jeshi Ili iweje?

Issue ni mafunzo, vifaa na weledi kwenye kukamilisha kazi zao?
 
Same same! Ntu anakuwaje amiri jeshi kabla hajawa rais?
Rais na Amiri jeshi ni mamlaka mbili tofauti kwenye sarafu moja. Ni takwa la kikatiba kwamba rais ndiye atakuwa amiri jeshi kama ambavyo ccm walivyowekeana takwa la kwamba rais ndiye atakuwa mwenyekiti wa chama lakini rais na mwenyekiti wa chama ni ofisi mbili tofauti lakini mtu ni yule yule.

Amiri jeshi au supreme commander au commander in chief ni mamlaka ya kijeshi ya juu kabisa ndani ya jeshi. Commander in chief ndiye anayetoa order ya jeshi kutenda kivita. Point ni kwamba mamlaka ya amiri jeshi yanahusu jeshi la ulinzi tu kwa sababu ni cheo cha kijeshi.
 
Haya maneno yatawavuruga daima
Military
Army
Force
Service
Department
Agency

Lazima tukubaliane jeshi ni nini?
Hayo maneno Yana athari yoyote kwenye utendaji kazi wao?

Magereza ni jeshi ila wanajiita Tanzania Prison Service, je service inaathiri utekelezaji wa majukumu Yao?

Jeshi la kujenga Taifa ni National Service, inawapunguzua wao ujeshi wao?

Tanzania Police Force na Fire and Rescue Force ni majeshi au la!
Ukiwaita Service itaathiri utendaji wao?

Kama neno force sio jeshi basi tukubaliane Tanzania hakuna jeshi Bali Kuna vikosi tu either vya ulinzi au usalama. Maana TPDF ni Tanzania people's defense forces.

Kama force ni nguvu na sio jeshi basi tukubaliane kwenye hoja kwamba hatuna jeshi, kama sivyo tukubaliane hayo tajwa ni majeshi whether ni service au force.

Tuje kwenye Immigration ni jeshi au lah?
Kwanza kirefu chake ni Tanzania Immigration Service Departmental
Kwanza tunaona Service ndani yake kama yalivyo majeshi ya magereza na kujenga Taifa.

Pili ilifanyika hivyo Ili kutoonyesha kwa wageni sisi ni ujeshi ujeshi ila hakuna sababu ya msingi, nje ya siasa.

Ni jeshi kamili kwa mujibu wa Sheria iliyoianzisha na kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Kuna ibara inasema Raisi na Amiri jeshi mkuu wa Tanzania anaweza kuanzisha jeshi kutokana na uhitaji.

Ni jeshi pekee lenye kazi za ulinzi, usalama, intelejensia na diplomasia.

Wana kazi za huduma kama kutoa pasipoti, vibali na control ya wageni ndani ya nchi.

Wana kazi za ulinzi hasa maeneo ya mipakani na doria kwenye vipenyo, kuhakikisha mipaka ya nchi ni salama.

Achana na maeneo ya kuingia na kutoka hasa ambako intelejensia kubwa inakusanywa.

Kuna mtu anauliza kama wana kikosi maalumu?
KMU kipo na kinaopareti kwa namna yake.

Ni jeshi kwa mujibu wa muundo wake na majukumu waliyonayo, ndio maana hawajabadilisha Sheria Yao.

Siraha nzito mpaka ukute wana vifaru?

Tiss
Tanzania intelligence security services Hawa ni mashushu na nature ya kazi zao ni ushushu na covert operations
Ulitaka wajiite jeshi Ili iweje?

Issue ni mafunzo, vifaa na weledi kwenye kukamilisha kazi zao?
Wewe hata huelewi ulichaondika. Jeshi la Uganda linaitwa UPDF. Hayo maneno Bombo Military hospital yametokea wapi? Fungua link hiyo
 
Jichanganye kwenye anga zao ndo utajua kama ni jeshi au la... Uhamiaji na Takukuru wanachukuliwa poa ila ukijichanganya utatamani ukutane na polisi wa kawaida.
 
Rais na Amiri jeshi ni mamlaka mbili tofauti kwenye sarafu moja. Ni takwa la kikatiba kwamba rais ndiye atakuwa amiri jeshi kama ambavyo ccm walivyowekeana takwa la kwamba mwenyekiti wa chama ni lazima awe rais lakini rais na mwenyekiti wa chama ni ofisi mbili tofauti lakini mtu ni yule yule.

Amiri jeshi au supreme commander au commander in chief ni mamlaka ya kijeshi ya juu kabisa ndani ya jeshi. Commander in chief ndiye anayetoa order ya jeshi kutenda kivita. Point ni kwamba mamlaka ya amiri jeshi yanahusu jeshi la ulinzi tu kwa sababu ni cheo cha kijeshi.
Habari ya chama imetoka wapi? Sijasema lolote la uenyekiti wala ccm mie
 
Mkuu nyuzi zako za uhamiaji zimekuwa nyingi sana shida nini?

Ulianza kuuliza kama wanalipa nauli kwenye daladala sasa umekuja hapa umepata kazi nini?
Hahahahaha hamna nipo karibu na eneo lao hapa
 
Wewe hata huelewi ulichaondika. Jeshi la Uganda linaitwa UPDF. Hayo maneno Bombo Military hospital yametokea wapi? Fungua link hiyo
Ni vikosi vya ulinzi Uganda UPDF.
Hawa wamefata mfano wa Tz baada ya kuwatwanga na kufuata module zetu.
Uganda sio mfano sahihi.
 
Tatizo wa Tz wengi hamtaki kujifunza hata sheria ndogondogo hata katiba hamuijui Sect 147(4) Cap 9 inatambua Magereza na polisi kama majeshi, na katiba inakataza kuwa ni marufuku mtu yoyote kuunda jeshi ingekua kisheria siyo majeshi wasingejiita majeshi usifikiri wanajiita kimazoea kama unavyodhani kwa faida zaidi soma hapaView attachment 3166532
Kumbuka katiba ni ya mwaka 1977. Kipindi hicho jeshi la polisi lilikuwq na idara ya zimamoto na uhamiaji.. je kwa sasa uhamiaji na zimamoto still zinatambulika kama majeshi... ukumbuke kwa sasa wanasheria tofauti ya uundwaji wao???
 
Back
Top Bottom