Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Tunarudi miaka mingi nyuma kwa kasi
Labda baadhi ya Viongozi wanawaza kinyume nyume, badala ya kufocus mbele.

Tatizo ni uongozi.
Ndiyo maana Dr. John C. Maxwell kasema, " Everything rises and falls on leadership"

Kama viongozi wanawaza kwa kurudi nyuma badala ya kusonga mbele, na matunda ya kazi zao yatakuwa vivyo hivyo.

Hiyo inatoa picha ya mitazamo ya Viongozi. Baadhi yao wangali wakiwaza kijima.
 
Ujue HUU NI UPUMBAVU.

Passport ni haki ya kila raia kuwa nayo.haijalishi una safari au hauna. Passport sio mali ya uhamiaji.

Acheni UKOLONI.

Yaani siku nikipata safari ndo nianze kuhangaika kutafuta passport?
Sidhani kama Wakoloni wangefanya ukatili kama huo! Wanaojua faida ya watu kutoka.
 
H
Hata tiketi za mabasi yanayoenda nchi za nje, details za passport zitahitajika.
 
Yaani hawa watu weusi hawaamini kabisa kama mkoloni alishaondoka na Mwafrika yuko huru sasa, walichorithi ndio wanasimama nacho. wanachobhana hata ukiwauliza wenyewe hawajui
 
Sisi tunatafuta scholarships, kwenye Application wanataka namba za passport itakuaje
Hawafikirii hivyo wenzio.
Wapo pale kuwapa wahindi na wachina vibali vya kuja kuchoma mahindi kariakoo na kufanya kazi ambazo watz wanaziweza.
Unajua Tanzania Kuna Malaya wengi Sana wa kichina na kihindi.
 
Watu wapumbavu walihubiri na kuingia kwenye globalisation huku wakizuia raia wao kuingia kwenye hiyo globalisation. Namna yao ya kufikiri inatia kichefuchefu kabisa.
 
Ujue HUU NI UPUMBAVU.

Passport ni haki ya kila raia kuwa nayo.haijalishi una safari au hauna. Passport sio mali ya uhamiaji.

Acheni UKOLONI.

Yaani siku nikipata safari ndo nianze kuhangaika kutafuta passport?
Bro umesema kile nilichotaka kusema hawa immigration ni watu wajinga sana ndio maana uraia wanapewa watu wa jirani ni watu hovyo sana tuko ktk ulimwengu wa DOT COM lakini hawa wako nyuma sana kila ukenda immigration mijitu mingi sana inafaa serikali wafungue vituo zaidi ya kumi kwa Dar na mambo yende speed .PAUL MSELLE Nenda kasome tena wewe na wote ni watumishi wetu uko pale kwa ajili yetu sisi Raia .Pasport ni haki ya Raia wote usituletee ushamba wako kama hujawahi kusafiri hebu safari kidogo uone wacheni roho zenu mbaya immigration.
 
Bora nilifanya mapema...
Nikapata bila usumbufu
 
Hili neno Pasipoti ni haki ya kila raia liondolewe, ibaki ni haki ya kila msafiri
 
HIVYO VIGEZO HAVIWAHUSU WAHAYA

SISI WAHAYA UKISHAZALIWA UNAHAKI YA PASSPORT KWA MAANA SAFAR HUWA TUNAZO NYINGI
 
Hili neno Pasipoti ni haki ya kila raia liondolewe, ibaki ni haki ya kila msafiri
Tafsiri mbovu sana

Tofauti ya kitambulisho cha NIDA na Passport ni moja tu

Kitambulisho cha NIDA ni kitambulisho local kinachotambuliwa locally kwa local people au taasisi local

Passport ni kitambulisho cha NIDA cha kimataifa kinachotambuliwa kimataifa

Kimataifa huwezi muonyesha mtu kitambulisho cha NIDA hiki local kikadi cha NIDA

Passport ni kitambulisho tu cha kawaida tu sema immigration hawajielewi wala kuelewa kwa nini Passport inatamkwa kuwa ni haki ya kila raia!!!

Kitambulisho cha NIDA ni haki ya kika raia na Passport pia ni haki ya kila Raia

Vyote vitambulisho tu

Mtu akitaka Passport apewe tu awe ana safari au la apewe tu kama kitambulisho cha NIDA whether atakitumia popote kwa lolote au la

Akiomba kitambulisho apewe
 
Hapatakalikaje mkuu? Kwamba kutakuwepo na utitiri wa watu?

Eboo! Sasa hiyo si fursa ya ajira? Ni Watanzania wangali wanaosaka ajira, na wengine hata kutafuta pa kujitolea bure bila mafanikio?

Passport inalipiwa. Kama idadi ya wateja itaongeza, na nguvu kazi ziongezwe.
 
"...mtu akiwa na passport hata akili ya kutoka nje kutafuta maisha inafunguka..."

Uko sahihi mkuu. Hiyo inaitwa "ACT AS IF!"

Mtu akishakuwa na passport, akili itaanza kutafuta fursa ya kusafiri.
 
Kufanikiwa kwa tanzania ni dili au jambo la ajabu,kuna maisha tanzania tunaishi kama zama za mawe.alafu tunashangalia tukisema wakombozi.
Uchumi wa kati wa mlipa kodi ya mwaka shilingi 20k
Inawezekana aliyetunga hiyo sera ni darasa la pili ambaye hajawahi kutoka nje ya kijiji chake

Haiakisi usomi hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…