Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

SCREEN SHOT OR PRINT-
Mkuu passport ni hati ya kusafiria wala siyo kitambulisho
una screen short nini kibox ambacho hujajaza passport number ? sababu zingine haziwi full form unajaza tu kidirisha kimoja then kina pop up kidirisha cha pili ujaze nk kila unapopiga next .Kwa hiyo mtu asi creen shot kidirisha hicho kitupu cha dirisha la kwanza akuletee kama ushahidi!!!! ha ha ha uwiii mbavu zangu mimi .Uhamiaji kitengo cha passport kuna shida!!!
 
Ndio tumefika huko!? Sitaki kuamini! Lakini haitashangaza ndani ya utawala huu hili kutokea.

Ofcoz ndo tumefika huku...

Labda hujaelewa maana ya kauli na uelekeo wake...

Hapa wanatafuta namna tu ya ku - invoke passport za watu kama Tundu Lissu, Godbless Lema, Evariste Chahali nk

Nothing more, nothing less...

Yaani tumefikia hatua sheria àu katiba au utaratibu fulani unaweza kubadilishwa kwa ajili ya kumshughulikia mtu mmoja tu bila kujali athari za jamii pana...

This is absolute dictatorship...
WE WA AJABU SANA
tena huyo ni wa ajabu jabina

Siku zote mjinga au kichaa huwaona walio na afya ya akili ni "WA AJABU" yeye katikati ya bahari ya ujinga ama ukichaa wake akijiona ni mwerevu...

Kwa muktadha huu, MIMI NI WA AJABU KWELI KWENU...!!
 
Wewe itakuwa huna hiyo nyaraka na hujawahi kukaribianana na yeyeyote aliewahi hata kufikiria kuwa nayo.

Mshangae huyo alielitoa hilo tamko sasa ila utaratibu unalazimisha iwepo sababu ya safari miaka yote sio leo wala jana.
Tunatambua kwamba kigezo hicho kilikuwepo lakini kumbuka kwamba hakikuwa kizuizi kikuu , sasa hivi hicho kimeshakuwa kizuizi halisi , na kwa ajili hii imebidi litolewe tangazo lenye uzito mkubwa kama hili ulionalo hapa
 
Jiki kitu ndicho kinaitwa kufanya kazi kama robot kwa mazoea ohhh miaka yote sisi huwa tunafanya hivi hivi!!!! AKILI INAKUWA ROBOT NA UTENDAJI KAZI WA KIROBOTI

Ndio maana Raisi anakuwa mkali kila siku kuwa watendaji kazi serikalini wabadilike waache kufanya kazi kwa mazoea
Swala sio Roboti wala Karagosi.

Swala ni uthibitisho wa sababu ya Safari na hilo lipo Kisheria,
Huyo Afisa hajaongea wala kusisitiza Matakwa yake, matakwa ya Kamishna wa Uhamiaji au Waziri wake.
Hati ya Kusafiria ni Nyaraka nyeti si vizuri itoke kienyejienyeji.
Kingine, mbona wanachokitaka sio kitu cha kutoa jasho?
Yeyote anaelalama lazima ana makandokano yake.
 
Swala sio Roboti wala Karagosi.

Swala ni uthibitisho wa sababu ya Safari na hilo lipo Kisheria,
Tuwekee hapa hicho kifungu cha sheria kinachosema mwuomba passport atatakiwa kujieleza anaenda wapi na kufanya nini ndipo apewe passport.Hebu tuwekee hicho kifungu cha sheria
 
Sasa utaombaje passport kama huna matumizi nayo?

Si unakua na mpango wa safari ndio unatafuta passport!? Au nakosea ndugu zangu😃😃😃😃
Mkuu, mboma watu wanasoma mpaka Master Degree wakati hawana kazi.
 
Kwani kuna siku uhamiaji washatoa passport bila kuuliza dhumuni? Kwenye form ya kaombi hicho kipengele ni muhimu na nchi unayotaka kwenda wanataka ujaze, sasa hapa atuambie tu kuwa kuanzia leo rushwa imeongezeka kidogo ila hii sio taarifa ngeni labda kwa wale wasiojua huo mchakato.
Tangu zamani mnadai barua za mialiko ndio mtoe pass hizo ila tulipokuwa tumezikosa tuliwapa kuazia laki ili mtupatie ndani ya siku 2 tu. Na wale waliokuwa wakijifanya wanaenda kwenye biashara si mlikuwa mnahitaji leseni zao za biashara na walipozikosa si waliwapa laki ile ile mkawapa passport??
Hakuna jipya hapa.
 
Nikiambatanisha kiambata cha usa lottery kinachotaka nijaze taarifa za passport kabla sijatuma maombi kitakubalika?
 
Tatizo la kudai mtu ajieleze ansenda nchi za watu kufanya nini alete barua ya mwaliko imesababisha mateso ya vijana wengi kuwa wazamiaji nchi zingine bila sababu na kuwafanya wadakwe kule hata kama kule wana shughuli halali kabisa wana maduka nk mfano south Africa msako ukipita wanadakwa kuwa wako nchini bila passport wala kibali.Fursa haina barua ya Mwaliko.Mtu aweza ona kuna fursa Afrika ya kusini barua ya mwaliko hana lakini anajua akifika kule Fursa inamsubiri.Akienda uhamiaji hakuna kipengele cha kupata passport cha kusema naenda kutafuta maisha au kuangalia fursa kama zipo au la!!!

Matokeo wengi unakuta wamerudishwa nchini sababu za kijinga tu za kitengo cha passport eti wameshikwa kule hawana passport!! Wanapekekwa kisutu mahakamani!!! Nchi zenye hii shida ni Tanzania na Ethiopia wanajifanya wagumu kutoa passport wanaumiza mamia ya vijana Ndio maana Tanzania kutwa ni kukamata wahamiaji haramu toka Ethiopia wanaokwenda Africa ya kusini.Wangekuwa nchini kwao wanapata passport kirahisi sisi tungewagongea tu mihuri ya kupita waendelee na safari zao

Roho ngumu ya kutoa passport ndio chanzo cha mateso makuu ya waethipia tunaokamata kila siku.Na sisi tuko kapu moja na Ethiopia

Lakini wa kwetu pia shida hiyo hiyo .Ugumu wa kupata passport unawafanya vijana wa Tanzania kupata shida nchi za watu kitengo cha passport Tanzania ni kitengo hovyo kabisa kinasababisha mateso kwa vijana wengi watafuta maisha nje
 
Nikiambatanisha kiambata cha usa lottery kinachotaka nijaze taarifa za passport kabla sijatuma maombi kitakubalika?
Ushapata hiyo lottery au unamaanisha tangazo tu la hiyo bahati nasibu?
Jamaa watataka barua ya mualiko na sio tangazo la fursa, ila kanyooshe mkono wako mkuu utaipata kirahisi tu.
 
Back
Top Bottom