Wanigeria hadi raha kule kwao passport chap chap lengo sababu nchi wanaona ajira hamna wanatoa kirahisi watu wakatafute fursa mbele kwa mbele nchi za watu
Halafu kuna kichekesho kingine mfano mnigeria kasafiri mfano akakaa nchi ya watu akapitiliza muda wa visa aliyopewa akafungashwa virago kuruidishwa kwao na kwa kawaida mtu kama huyo hugongewa muhuri wa PI kwenye passport kwa wale msiojua PI ni nini ni PROHIBITED IMMIGRANT Kuwa hurusiwi kukanyaga nchi yao tena .Muhuri huo hugongewa wahalifu waliofanya uhalifu nchi za watu kwenye passport zao
Sasa ukienda nchi nyingine yeyote afisa uhamiaji mpakani au airport akipitia hiyo passport akikuta kuna mhuri wa PI hakuruhusu kuingia nchini kwake wala hakuulizi swali hata ukiernda ubalozi wowote ukiomba visa wakiona PI hawakupi VIZA
Sasa wanigeria mabalozi wao nchi zao huwa na taarifa zote za wanigeria wao walioko nchi husika.Wanigeria wakifika nchi yeyote cha kwanza hujitahidi kuripoti ubalozi wao kwa hiyo anajua huyo mnigeria karudishwa kwa kosa la ku over stay.Taarifa zinatumwa haraka ofisi ya makao makuu ya uhamiaji Nigeria kuwa kuna mtu wetu anarudishwa huko kagongewa PI kwenye passport hajafanya uhalifu wowote zaidi ya ku overstay!!.Akitua tu NIGERIA ANAENDA OFISI YA UHAMIAJI nIGERIA ANAPEWA Pole na kupewa passport ingine safi mpya aendelee na safari yake ya kuhangaika kutafuta riziki nchi zingine nje ya ile waliyomgongea PI
Sisi hapa kwetu mtu anarudishwa kisa passport hana alishindwa kuipata akazamia mfano Afrika ya kusini akifika hapa anakamatwa anaswekwa mndani na kuburuzwa mahakamani!!! Utakuta maafisa uhamiaji wanachekelea kuwaafikisha mahakani kisutu Dar es salaam.
Mfano ni hawa wazamiaji 100
"WATANZANIA 100 wamepewa adhabu ya kutofanya kosa ndani ya miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kutenda kosa la kutoka ndani ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwenda Afrika Kusini bila kufata utaratibu wa uhamiaji.
Raia hao ni Laurence Omary, Sultani Ditutu, Nassoro Lingumbulu, Abdul Masoud, Waziri Waziri, Dotto Abdallah na wenzao 94 ambao walipewa adhabu hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.
Katika kesi hiyo, wakili wa serikali Godfrey Ngwijo, akisaidiana na Sitta Shija, wamedai kuwa, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Julai 3 mwaka 2020 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Ilidaliwa kwamba, wakiwa raia wa Tanzania walibainika kutoka nje ya Tanzania katika tarehe zisizofahamika bila kufata utaratibu wa kiuhamiaji na kuelekea Afrika Kusini."
Cheki Afisa uhamiaji anavyosikia raha kuwakimbiza kama wanyama pori mahakamani kisutu Da es salaam
Wanatia hadi huruma
View attachment 1786634
Source ya habari yenyewe: Magazeti mbalimbali na jamii forums