Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Kwa utaratibu huu wanapoteza mapato mengi sana. Fikiria gharama za passport kisha uhimize kila raia awe nayo, walau hata milioni 8 tu.
Lakini pia kuwa na passport inaongeza hata usalama wa nchi.
Nahisi, sera ya ujamaa ina tabia ya kulemaza uwezo wa kufikiri.

Hawaoni kama hiyo ni mojawapo ya njia halali ya kuongeza mapato halali ya Serikali. Wanaojua kutumia tu zilizokusanywa, hawajui kuzalisha kihalali.
 
Hii ndio taarifa mpya kutoka Uhamiaji iliyotolewa leo na Msemaji wake Paul Mselle.
View attachment 1727162
Paul Mselle amesema haya...

Pasi ya kusafiria ni 'document' ya kiusalama na ni haki ya kiusalama na ni mali ya Serikali, pale ambapo mtu ataitumia vibaya basi anaweza akanyang’anywa

Pasi ya kusafiria sio kitambulisho kusema mtu achukue abaki nayo ndani ni lazima kuwe na dhumuni la safari, kama hauna safari hatuwezi kukupa pasi ya kusafiria

Mtu atakayepoteza Pasi yake ya kusafiria (Passport), itamlazimu kutoa taarifa Polisi pamoja na kutangaza kwenye gazeti na kwamba ni lazima atoe kiasi cha shilingi Laki tano kwa kupoteza Passport hiyo, na ili aweze kupata nyingine.

Kumekuwa na changamoto ya kuchelewa kwa pasi ya kusafiria sababu unakuta mtu hajakamilisha vigezo vya kupata pasi ya kusafiria. Kuna wengine wanawasilisha vyeti vya kuzaliwa ambavyo haviko kwenye mfumo wa RITA na ukimuuliza alikipataje anasema alimtuma mtu kwa maana ya vishoka na hawa unakuta wengine ni raia wa Tanzania na wengine sio raia wa Tanzania

Wengine nao unakuta taarifa za cheti cha kuzaliwa zinatofautiana na taarifa za vitambulisho vya Taifa, unakuta kwenye Kitambulisho cha TAIFA(NIDA) kazaliwa Temeke kwenye cheti kazaliwa Morogoro.

Passport.png
Kuna haja ya kuishtaki serikali mahakamani kwa haya matamko ya kipuuzi.

Hati ya kusafiria ni haki kwa kila Mtanzania. Sasa leo wanapokuja na vigezo vya kibaguzi ni ujinga mtupu.

Hawa wahuni wameshazoea kula vibudu na wakishastaafu wanagombea kupitia chama kinacholinda uhalifu wa dola
 
[emoji38][emoji38][emoji38]

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Kifupi wewe kama uko serikalini kikazi una mawazo ya kizee hujastaafu tu kikongwe mjinga wewe

Hata huelewi dunia ilipo

Vizee kama nyinyi hopeless kabisa tokeni maofisini mkalee vijukuu vyenu huko

Duh , hata wewe! Kweli kuishi kwingi kuona mengi! Je unaonaje kwa chama chakavu kilichozeeka kisichoelewa dunia ilipo?

Kwa nini hukishauri chama jinga na kikongwe CCM kustaafu?Kwa kweli adui namba wani wa taifa letu pendwa ni CCM!
 
Kuna haja ya kuishtaki serikali mahakamani kwa haya matamko ya kipuuzi.

Hati ya kusafiria ni haki kwa kila Mtanzania. Sasa leo wanapokuja na vigezo vya kibaguzi ni ujinga mtupu.

Hawa wahuni wameshazoea kula vibudu na wakishastaafu wanagombea kupitia chama kinacholinda uhalifu wa dola
Iko vizuri mawakili wasomi waiburuze serikali mahakamani

Mawakili wasomi wanaojielewa wasomi wanaoelewa walichosoma waburuze serikali mahakamani issue hii ya Passport sababu inaonyesha serikali inajifanya kiziwi

Kipengele cha sababu ya safari kiondoke kwenye kupata passport

Vyama vya siasa vyote havijali wala kuongelea Mawakili wa haki za binadamu au wakili yeyote aiburuze serikali mahakamani
 
Kifupi wewe kama uko serikalini kikazi una mawazo ya kizee hujastaafu tu kikongwe mjinga wewe

Hata huelewi dunia ilipo
Wewe unayedhani unaelewa dunia ilipo nifundishe
Passport ukitaka kufanya hata mitihani ya kimataifa online ukiwa Tanzania lazima uwe na passport hata
Taasisi ipi hiyo ya Kimataifa inachukua ID pekee ya PASSPORT na inakataa National Identity ya nchi husika ? Kama hiyo Taasisi ipo ni wakati muafaka kwa nchi / hio Taasisi kufahamishwa kwamba Tanzania tuna National Identity na hicho ndio kitambulisho cha uhakika kwamba wewe ni Mtanzania....
ukiomba kazi au scholarship,online kimataifa au tenda kimataifa online lazima uwe na passport
Ukiomba Kazi na unategemea kupata hio kazi mwisho wa siku si lazima utasafiri kwenda kwenye hio kazi ? Kwahio hukatazwi kuweka sababu hio kwamba unategemea kufanya kazi nchi fulani, wanachotaka ni ile barua yenye sababu husika...
Vizee kama nyinyi hopeless kabisa tokeni maofisini mkalee vijukuu vyenu huko

Pisheni vijana washike nafasi

Upumbavu wenu wa kizee pelekeni kwa vijukuu vyenu pisheni vijana

Vijana washike
Na hapo ndio umeonyesha ufinyu wa mawazo yako, kwanza assumptions ambazo hazipo based kwenye any logical substance.., pili kudhani kwako kwamba wazee ni obsulute na vijana ndio wanashika kila kitu inaonyesha vipi upeo wako ni sawa na urefu wa pua yako....; Kwahio wewe Kijana innovation yako ili kurahisisha watu waweze kufanya mitihani na kuomba passport ni waweze kupata hizo passport (150k at a minimum) na sio kuhakikisha hizo Taasisi zinatambua NIDA (free) kwenye ufanyaji na ujazaji wa hizo fomu za hio Taasisi ?

Kama vijana wote wana akili kama zako..., We need a Divine Intervention (we are absolutely and truly lost)
 
Yule mzee aliwaambukiza tabia mbaya sana watanzania

Mpaka leo ukiwa kidogo na life lenye unafuu, unalo[emoji848]
Sana sana, baadhi walijifunza unafiki.

"Walihubiri", viongozi wasimiliki nyumba za kupanga, lakini wengine "wakajiongeza" na kujenga nyumba za kupangisha kwa siri.

Halafu ni kama vile ujamaa ulikuwa na uhasama na vitu vizuri.

Nilisimuliwa na mtu mmoja kuwa baba yake alikuwa akifanya biashara kipindi hicho, akitoa mzigo Arusha na kwenda kuuzis Dodoma.

Awamu ya kwanza alienda akiwa amevaa suti.

Ndani ya mwezi huo huo, akarudi Dodoma akiwa amevaa suti nyingine. Saa ngapi hajatiwa nguvuni!

Kosa? Kabadilisha suti ndani ya mwezi mmoja, akahusishwa na uhujumu uchumi.

Sasa kama bado kuna watu wenye mitazamo ya aina hiyo, inatarajia nini?

Siyo siri, nazichukia mno sera za UJAMAA na ukomunisti.
 
Kifupi wewe kama uko serikalini kikazi una mawazo ya kizee hujastaafu tu kikongwe mjinga wewe

Hata huelewi dunia ilipo

Passport ukitaka kufanya hata mitihani ya kimataifa online ukiwa Tanzania lazima uwe na passport hata ukiomba kazi au scholarship,online kimataifa au tenda kimataifa online lazima uwe na passport

Vizee kama nyinyi hopeless kabisa tokeni maofisini mkalee vijukuu vyenu huko

Pisheni vijana washike nafasi

Upumbavu wenu wa kizee pelekeni kwa vijukuu vyenu pisheni vijana

Vijana washike
By the way na hawa wazee wanaofanya kazi kwenye Ofisi za Passport USA sijui kwanini na wenyewe wasiache kazi;

You should have a U.S. passport if: You have family living or traveling abroad, You are thinking about a vacation abroad, or. You have a job that could require international travel.
Na kwenye Site yao ya

Kuna sehemu namba nne ya requirement - Proof of International Travel

4. What counts as the “proof of international travel” required to apply at a passport agency?

If you are flying internationally, you must provide a flight receipt or an itinerary. If you are traveling by land or sea to Canada, Mexico, Bermuda, or the Caribbean, you can provide a hotel reservation, cruise tickets, or international car insurance. A print version of your proof of travel is required at most agencies.
 
Kwani nini maani ya Pass- Port...,

Kwahio ndio hivyo ukitaka Passport hautanyimwa bali lazima uwe na nia ya kusafiri, na kinachotakiwa ni barua tu kama procedure kwamba unataka kusafiri kwenda sehemu fulani kwa sababu fulani.

Sioni tatizo sababu kuna loopholes nyingi kama unaenda kutembea utaambatanisha barua ya mwaliko kama kutembea kama mtalii utaambatanisha bank statement yako kwamba una uwezo, kama unatumwa kwenda kuangalia bidhaa za biashara utaweka barua ya mwenye biashara anakufadhili, kama ni scholarship utaambatanisha maelezo...

Hili sio jipya ni moja ya Vigezo vya uhamiaji walivyojiwekea; after all Passport kazi yake ni hio kupita border / port; kama ni ID nyingine hizo zipo pia na kwa kazi yake husika

Haya mambo ya katne nyingi zilizopita. Mnaipeleka nchi kuzimu. Passport ni id yako . Kila mtu anatskiwa awe nayo nyumbani, ukisafiri au husafiri Huo ni uamuzi wako mwenyewe.
Hebu tupeni nchi yetu Zanzibar mliyoivamia ,tuwaonyeshe vipi watu wanatakiwa kuishi. Sisi hatuna haja na passport zenu. Mbaki nazo , mkizipikia mboga na ugali shauri yenu.
Tupeni Zanzibar yetu tu. Hatutaki passport zenu
 
Iko vizuri mawakili wasomi waiburuze serikali mahakamani

Mawakili wasomi wanaojielewa wasomi wanaoelewa walichosoma waburuze serikali mahakamani issue hii ya Passport sababu inaonyesha serikali inajifanya kiziwi

Kipengele cha sababu ya safari kiondoke kwenye kupata passport

Vyama vya siasa vyote havijali wala kuongelea Mawakili wa haki za binadamu au wakili yeyote aiburuze serikali mahakamani
Namkumbuka Mch. Mtikila waliyemuua ajalini.
Alikuwa anawakomesha sana na sheria za ajabu ajabu.

Tuwashtaki hawa walioshiba shibe ya dhuluma
 
Haya mambo ya katne nyingi zilizopita. Mnaipeleka nchi kuzimu. Passport ni id yako . Kila mtu anatskiwa awe nayo nyumbani, ukisafiri au husafiri Huo ni uvamizi wako mwenyewe.
Wewe ndio una mambo ya kale kupita kiasi Passport ni haki yako sababu kusafiri ni haki yako na hakuna mtu anakuzuia; kwahio unapotaka kusafiri au unategemea kusafiri unaomba na utapewa ila katika requirements na hilo utaliweka (sababu ya kusafiri) (Hii ni Hati ya Kusafiria sio Hati ya kuiweka Nyumbani)....; sababu huenda unataka kusafiri kwenda Sudan (utashauriwa kule kuna vita kwa sasa), lakini ukiwa na sababu ya kusafiri alafu usisafiri sio kwamba watakunyanganya utaendelea kuwa nayo hata kama hautasafiri kamwe..., Sasa wewe unavyosema kila mtu anapaswa awe nayo naona una genes za udikteta (yaani mtu atoe 150K kwa kitu ambacho wala hakiitaji)?
Hebu tupeni nchi yetu Zanzibar liyoivamia ,tuwaonyeshe vipi watu wanatakiwa kuishi. Sisi hatuna haja na passport zenu. Mbaki nazo , mkizipikia mboga na ugali shauri yenu.
Tupeni Zanzibar yetu tu. Hatutaki passport zenu
Nadhani sentensi yako ya mwisho inaonyesha vipi unahitaji msaada; na mimi kama raia wa nchi yoyote mgeni kama wewe nitafurahi sana kama hautapewa passport sababu huenda ukipewa visa utaleta mawazo yako mgando huko...

By the way hivi unajua kuna kipindi Tanzania ulikuwa hauhitaji VISA kwenda sehemu kama UK (commonwealth country) ila nadhani pamoja na mengi mengi kuna kipindi ndugu zetu nyie wanzibar na zanzibar yenu mlijazana kule na kukimbilia huko eti ni wakimbizi..., nadhani hili na pamoja na passport za Tanzania kuuzwa kama njugu kwa wasomali ndio kulipelekea hili Gamba la nchi letu kupunguza value
 
Mkuu, utafiti wangu usio rasmi umenibainishia kuwa kuna baadhi ya watu walioenda shule na kupata mavyeti kibao lakini vichwani weupe.

Lakini kuna wengine, japo wanaweza wakawa na vyeti vya kawaida ila upstairs kunasoma vizuri.

Matendo ya mtu ndiyo yanayothibitisha kiwango chake cha hekima au upumbavu.
Upo sahihi sana mkuu
 
Wewe ndio una mambo ya kale kupita kiasi Passport ni haki yako sababu kusafiri ni haki yako na hakuna mtu anakuzuia; kwahio unapotaka kusafiri au unategemea kusafiri unaomba na utapewa ila katika requirements na hilo utaliweka (sababu ya kusafiri) (Hii ni Hati ya Kusafiria sio Hati ya kuiweka Nyumbani)....; sababu huenda unataka kusafiri kwenda Sudan (utashauriwa kule kuna vita kwa sasa), lakini ukiwa na sababu ya kusafiri alafu usisafiri sio kwamba watakunyanganya utaendelea kuwa nayo hata kama hautasafiri kamwe..., Sasa wewe unavyosema kila mtu anapaswa awe nayo naona una genes za udikteta (yaani mtu atoe 150K kwa kitu ambacho wala hakiitaji)?

Nadhani sentensi yako ya mwisho inaonyesha vipi unahitaji msaada; na mimi kama raia wa nchi yoyote mgeni kama wewe nitafurahi sana kama hautapewa passport sababu huenda ukipewa visa utaleta mawazo yako mgando huko...

By the way hivi unajua kuna kipindi Tanzania ulikuwa hauhitaji VISA kwenda sehemu kama UK (commonwealth country) ila nadhani pamoja na mengi mengi kuna kipindi ndugu zetu nyie wanzibar na zanzibar yenu mlijazana kule na kukimbilia huko eti ni wakimbizi..., nadhani hili na pamoja na passport za Tanzania kuuzwa kama njugu kwa wasomali ndio kulipelekea hili Gamba la nchi letu kupunguza value

Wazanzibari walianza kuwa wakimbizi toka mlipotuvamia 1964 , au hujui Wazanzibari wengi walikimbilia, Somalia, Kenya, Na nchi Za Kiarabu baada ya mauwaji ya maelfu ya watu ?
Passport mnaziuza wenyewe kwenye balozi zenu. Mimi mwenyewe nilikutana na wahindi wakiwa na passport Za TZ walizouziwa katika ubalozi wenu wa India.
Sisi wa Zanzibar hatuna haja na passport zenu , tupeni nchi yetu mliyoivamia
 
Naomba kwanza kujua tunaongelea kitu gani ?

Uzanzibar na Utanganyika au Kwamba kazi ya Passport (Hati ya Kusafiria ni Safari) ? Na kuhusu ID zipo nyingi na inayohakikisha wewe ni Mtanganyika au Mzanzibar ni National Identity Card.

Pili kupewa passport ni requirement utoe dhumuni la kusafiri huwezi kusema nataka hii passport niipambe kwenye nyumba yangu au kama umezuiliwa kusafiri hata hio Hati ya Kusafiria utanyanganywa... na kuwa na dhumuni la kusafiri haimaanishi utasafiri unaweza ukapana kusafiri ukapata passport na usisafiri maisha yako yote ila passport itakuwa yako (hautanyanganywa)

Na kwa wale wanaotaka waipate tu waitumie kama ID kuna cheaper alternative mfano (National ID) na kama hii National ID haina uzito its about time ifanywe iwe na uzito..., Na kama unataka scholarship au kusoma nje (hilo tayari ni dhumuni la kusafiri hivyo utapewa Hati ya Kusafiria)
 
Kwani nini maani ya Pass- Port...,

Kwahio ndio hivyo ukitaka Passport hautanyimwa bali lazima uwe na nia ya kusafiri, na kinachotakiwa ni barua tu kama procedure kwamba unataka kusafiri kwenda sehemu fulani kwa sababu fulani.

Sioni tatizo sababu kuna loopholes nyingi kama unaenda kutembea utaambatanisha barua ya mwaliko kama kutembea kama mtalii utaambatanisha bank statement yako kwamba una uwezo, kama unatumwa kwenda kuangalia bidhaa za biashara utaweka barua ya mwenye biashara anakufadhili, kama ni scholarship utaambatanisha maelezo...

Hili sio jipya ni moja ya Vigezo vya uhamiaji walivyojiwekea; after all Passport kazi yake ni hio kupita border / port; kama ni ID nyingine hizo zipo pia na kwa kazi yake husika
Shida inaanzia kufikiri kuwa ukitaka passort basi tayari unataka kusafiri. Unasahau kwamba ukiwa unaapply kazi nje ya nchi kwenye fomu utajaza passport ukiwa waomba scholarship nako watataka passport, greencard passport na hapo kuna probability ya kupata au kukosa so ina maana kwasababu mtu hana safari hizo fursa zimpite?
Mawazo ya ujima haya na yametolewa na watu ambao wana fikra za kizamani
 
Back
Top Bottom