Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Shida inaanzia kufikiri kuwa ukitaka passort basi tayari unataka kusafiri. Unasahau kwamba ukiwa unaapply kazi nje ya nchi kwenye fomu utajaza passport ukiwa waomba scholarship nako watataka passport, greencard passport na hapo kuna probability ya kupata au kukosa so ina maana kwasababu mtu hana safari hizo fursa zimpite?
Mawazo ya ujima haya na yametolewa na watu ambao wana fikra za kizamani
Ukirudia kusoma niliyoandika wala usingeandika ulichoandika...., Kuomba scholarship, kazi nje sio dhumuni la kusafiri ?

Au unadhani nini maana ya dhumuni ?, Kwamba uombe kazi nje alafu ukipata uifanye remotely bila kusafiri ? Hivyo utaandika barua na reason ni hiyo kwamba kulingana na qualification zako kuna kazi fulani ambayo kuipata utahitaji passport na unaomba upewe..., hata ukikosa hii kazi sababu unaendelea kutafuta next time wala hautahitaji kuomba tena (utakuwa nayo)
 
Wewe unayedhani unaelewa dunia ilipo nifundishe

Taasisi ipi hiyo ya Kimataifa inachukua ID pekee ya PASSPORT na inakataa National Identity ya nchi husika ? Kama hiyo Taasisi ipo ni wakati muafaka kwa nchi / hio Taasisi kufahamishwa kwamba Tanzania tuna National Identity na hicho ndio kitambulisho cha uhakika kwamba wewe ni Mtanzania....

Ukiomba Kazi na unategemea kupata hio kazi mwisho wa siku si lazima utasafiri kwenda kwenye hio kazi ? Kwahio hukatazwi kuweka sababu hio kwamba unategemea kufanya kazi nchi fulani, wanachotaka ni ile barua yenye sababu husika...

Na hapo ndio umeonyesha ufinyu wa mawazo yako, kwanza assumptions ambazo hazipo based kwenye any logical substance.., pili kudhani kwako kwamba wazee ni obsulute na vijana ndio wanashika kila kitu inaonyesha vipi upeo wako ni sawa na urefu wa pua yako....; Kwahio wewe Kijana innovation yako ili kurahisisha watu waweze kufanya mitihani na kuomba passport ni waweze kupata hizo passport (150k at a minimum) na sio kuhakikisha hizo Taasisi zinatambua NIDA (free) kwenye ufanyaji na ujazaji wa hizo fomu za hio Taasisi ?

Kama vijana wote wana akili kama zako..., We need a Divine Intervention (we are absolutely and truly lost)
Kifupi wewe kizee akili huna National ID yaweza hata tumika kwenda Zambia au Malawi?

National Id mwisho Tanzania haivuki mpaka Tanzania wala online kimataifa

Immigration itabadilika vizee vikongwe vya kike na kiume vilivyoajiriwa kipindi cha Nyerere vikiondoka hopeless kabisa

Na havina muda mrefu vitastaafu viachie vijana ndio twaweza ongea nao lugha moja
Vimebaki vikongwe hivyo vichache vitastaafu muda si mrefu vikalee vijukuu vyao vijana wa take over waelewa

Tuvute subira

Tuvivumilie hivyo vizee hopeless vya kike na kiume vilivyoajiriwa kipindi cha Nyerere viondoke sababu haviko flexible na havielewi dunia iendako havina muda vitastaafu
 
Duh , hata wewe! Kweli kuishi kwingi kuona mengi! Je unaonaje kwa chama chakavu kilichozeeka kisichoelewa dunia ilipo?

Kwa nini hukishauri chama jinga na kikongwe CCM kustaafu?Kwa kweli adui namba wani wa taifa letu pendwa ni CCM!
[emoji38][emoji38][emoji38]

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Ukirudia kusoma niliyoandika wala usingeandika ulichoandika...., Kuomba scholarship, kazi nje sio dhumuni la kusafiri ?

Au unadhani nini maana ya dhumuni ?, Kwamba uombe kazi nje alafu ukipata uifanye remotely bila kusafiri ? Hivyo utaandika barua na reason ni hiyo kwamba kulingana na qualification zako kuna kazi fulani ambayo kuipata utahitaji passport na unaomba upewe..., hata ukikosa hii kazi sababu unaendelea kutafuta next time wala hautahitaji kuomba tena (utakuwa nayo)
Kuomba kazi muda mwingine unakuta ni mchakato ambao una muda mfupi sasa uanze kufuatilia passport. Hivi kwnai shida iko wapi mtu kumpa passport as long as ni mtanzania na amelipa pesa. Safari imaweza kuwa wakati wowote na ni ghafla. Umepata zali la kazo ghafla unasepa tu.
Haya mambo ya kufanya complication katika kila jambo ndilo linafanya kuwepo na mianya ya rushwa. Wametoa tangazo ila ukiwa na ela hiyo passport hata bila safari unaipata ndani ya siku 3 kwa kutoa rushwa.
Mawazo ya ujima haya
 
By the way na hawa wazee wanaofanya kazi kwenye Ofisi za Passport USA sijui kwanini na wenyewe wasiache kazi;


Na kwenye Site yao ya

Kuna sehemu namba nne ya requirement - Proof of International Travel

4. What counts as the “proof of international travel” required to apply at a passport agency?

If you are flying internationally, you must provide a flight receipt or an itinerary. If you are traveling by land or sea to Canada, Mexico, Bermuda, or the Caribbean, you can provide a hotel reservation, cruise tickets, or international car insurance. A print version of your proof of travel is required at most agencies.
sasa USA kupata passport kwa mhitaji inachukua muda gani ? sasa linganisha na Tanzania

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Naomba kwanza kujua tunaongelea kitu gani ?

Uzanzibar na Utanganyika au Kwamba kazi ya Passport (Hati ya Kusafiria ni Safari) ? Na kuhusu ID zipo nyingi na inayohakikisha wewe ni Mtanganyika au Mzanzibar ni National Identity Card.

Pili kupewa passport ni requirement utoe dhumuni la kusafiri huwezi kusema nataka hii passport niipambe kwenye nyumba yangu au kama umezuiliwa kusafiri hata hio Hati ya Kusafiria utanyanganywa... na kuwa na dhumuni la kusafiri haimaanishi utasafiri unaweza ukapana kusafiri ukapata passport na usisafiri maisha yako yote ila passport itakuwa yako (hautanyanganywa)

Na kwa wale wanaotaka waipate tu waitumie kama ID kuna cheaper alternative mfano (National ID) na kama hii National ID haina uzito its about time ifanywe iwe na uzito..., Na kama unataka scholarship au kusoma nje (hilo tayari ni dhumuni la kusafiri hivyo utapewa Hati ya Kusafiria)

Passport ni haki ya mtu kuwa nayo nyumbani. Nimetembelea nchi nyingi na raia wao wanapewa passport hata bila kusafiri. Wakati Maalim Seif alipokuwa Waziri kiongozi alisema wazi kuwa kila mtu anayo haki ya kuwa na passport nyumbani hata Kama husafiri. Na Mimi mwenyewe nilichukuwa passport wakati Huo. CCM kwenye mambo ya passport kuwadhibiti watu hayakuanza Leo. Wakati wa Nyerere ndiyo ilikuwa ukipata Passport ukionekana ni mwanamume. Ikiwa nchi nyingi tumewekewa viza, Muna wasiwasi gani kuwapa watu passport ? Kama si ujinga na Roho mbaya ni kitu gani ??
Ndiyo nikasema tupeni nchi yetu ya Zanzibar mliyoivamia tuwaonyeshe namna nchi inavyoongozwa. Wacheni kuwapa shida watu na Roho zenu mbaya. Kama vile nchi ni Mali yenu
 
Kifupi wewe kizee akili huna National ID yaweza hata tumika kwenda Zambia au Malawi?
Wewe mwenye akili ukitaka kwenda Zambia au Malawi hilo sio dhumuni la kusafiri
National I'd mwisho Tanzania haivuki mpaka Tanzania wala online kimataifa
Nimekwambia wewe unayesema unataka kufanya mitihani online (kama requirement ni kujulikana wewe matanzania ni ID gani inakutambulisha kwamba wewe ni Mtanzania) ?

Na kama haitambuliki kimataifa hio ni kosa la nani ? Na kurectify hilo ni kufanya Passport iwe ndio National ID na sio kwamba kufanya National ID itambulike ?
Immigration itabadilika vizee vikongwe vya kike na kiume vilivyoajiriwa kipindi cha Nyerere vikiondoka hopeless kabisa

Na havina muda mrefu vitastaafu viachie vijana ndio twaweza ongea nao lugha moja
Vimebaki vikongwe hivyo vichache vitastaafu muda si mrefu vikalee vijukuu vyao vijana wa take over waelewa

Tuvute subira

Tuvivumilie hivyo vizee hopeless vya kike na kiume vilivyoajiriwa kipindi cha Nyerere viondoke sababu haviko flexible na havielewi dunia iendako havina muda vitastaafu
Hapa sina la kujibu sababu naona hoja imeamia kwenye uzembe wa vizee; na mtu anayedharau wazee wakati ndipo anapoelekea ni kumuonea huruma sababu kama nilivyosema upeo wake huenda ni mrefu kama pua yake...
 
Kifupi wewe kizee akili huna National ID yaweza hata tumika kwenda Zambia au Malawi?

National Id mwisho Tanzania haivuki mpaka Tanzania wala online kimataifa

Immigration itabadilika vizee vikongwe vya kike na kiume vilivyoajiriwa kipindi cha Nyerere vikiondoka hopeless kabisa

Na havina muda mrefu vitastaafu viachie vijana ndio twaweza ongea nao lugha moja
Vimebaki vikongwe hivyo vichache vitastaafu muda si mrefu vikalee vijukuu vyao vijana wa take over waelewa

Tuvute subira

Tuvivumilie hivyo vizee hopeless vya kike na kiume vilivyoajiriwa kipindi cha Nyerere viondoke sababu haviko flexible na havielewi dunia iendako havina muda vitastaafu
Hao vijana ndo pasua kichwa hatari mie leo nmepasuliwa mpaka basi sababu ya uraia
Na nmeenda na viambatanisho vyote
 
Hii ndio taarifa mpya kutoka Uhamiaji iliyotolewa leo na Msemaji wake Paul Mselle.
View attachment 1727162
Paul Mselle amesema haya...

Pasi ya kusafiria ni 'document' ya kiusalama na ni haki ya kiusalama na ni mali ya Serikali, pale ambapo mtu ataitumia vibaya basi anaweza akanyang’anywa

Pasi ya kusafiria sio kitambulisho kusema mtu achukue abaki nayo ndani ni lazima kuwe na dhumuni la safari, kama hauna safari hatuwezi kukupa pasi ya kusafiria

Mtu atakayepoteza Pasi yake ya kusafiria (Passport), itamlazimu kutoa taarifa Polisi pamoja na kutangaza kwenye gazeti na kwamba ni lazima atoe kiasi cha shilingi Laki tano kwa kupoteza Passport hiyo, na ili aweze kupata nyingine.

Kumekuwa na changamoto ya kuchelewa kwa pasi ya kusafiria sababu unakuta mtu hajakamilisha vigezo vya kupata pasi ya kusafiria. Kuna wengine wanawasilisha vyeti vya kuzaliwa ambavyo haviko kwenye mfumo wa RITA na ukimuuliza alikipataje anasema alimtuma mtu kwa maana ya vishoka na hawa unakuta wengine ni raia wa Tanzania na wengine sio raia wa Tanzania

Wengine nao unakuta taarifa za cheti cha kuzaliwa zinatofautiana na taarifa za vitambulisho vya Taifa, unakuta kwenye Kitambulisho cha TAIFA(NIDA) kazaliwa Temeke kwenye cheti kazaliwa Morogoro.

Passport.png


 
Huu ni ujinga wa mwisho pass port ni haki kwa raia yyote ambae ni raia husika wa nchi na vile vile ni kuntroli rai wao kuna nchi mtoto akizaliwa tu basi anapewa passport yake au kwa kipindi cha uchanga wake anatiwa katika passport ya mama ake jina lake .Sasa kusema mpaka uwe na safari ni upumbavu wa mwisho passport ina matumizi kibao ni hati thabiti ya kufanya mambo mengi .vitambulisho vya NIDA its local si international sababu havina sifa ya kimataifa .vitambulisho vya kimataifa hivi sasa viko chip ambayo ina soma data zako .
Kuna mtu, nafikiri Mnigeria, alitaka kumkatia mtoto wake aliyekuwa hajazaliwa. Changamoto ilikuja kwenye picha, ilihitajika picha ya mtoto. Sijui kama alilifanikisha kabla ya kuzaliwa.

Kama nchi zingine passport zinaweza zikatolewa hata kwa watoto waliopo tumboni, kwa nini Watanzania wote watu wazima wenye uwezo wa kulipia wasipewe?
 
Anaambatishaje fomu wakati iko online na sio printable? ina tu button ya submit kwa mhusika ukifika mwisho? Sasa ndio yuko tu kwenye kidirisha kidogo kinachoonyesha jaza namba ya passport ili uende dirisha next haiendi inakwamia hapo sasa akuletee fomu gani au unafikiri mtu akiomba scholarship au kazi nje ya nchi online fomu analetewa kupitia sanduku la posta kama zamani enzi zenu? Ndio unasema jaza uilete copy kama ushahidi? aiseee kazi ipo puuuuu kitengo cha passport kazi mnayo si kwa ujinga huu

Haina maana yoyote kwako zaidi ya international safari, but with people going into international hotels and international deals , passport number is an essential!
Mimi naamini ni faida sana endapo watu wengi watapewa passport.

Je! Kuna hasara gani kwa upande wa Serikali endapo watu wote watapewa passport?

Au Serikali inahofia kuwa watu wote watasafiri na hivyo kodi kupungua?
 
Kuomba kazi muda mwingine unakuta ni mchakato ambao una muda mfupi sasa uanze kufuatilia passport.
Again ku-solve tatizo ambalo halipo badala ya ku-solve tatizo; kwahio hapa tatizo ni kufuatilia passport (machakato sio rafiki) lakini tatizo sio requirement / dhumuni ambalo ni kusafiri....;
Hivi kwnai shida iko wapi mtu kumpa passport as long as ni mtanzania na amelipa pesa. Safari imaweza kuwa wakati wowote na ni ghafla. Umepata zali la kazo ghafla unasepa tu.
Kama wewe unaweza kupata zali na unashindwa kusema requirement / kuweka attachment ya sababu ya kwanini unataka passport (kusafiri kwenda wapi, hata kama hautasafiri) nadhani hata hilo zali ulilolipata ukifika huko utafeli...., Kwahio hapa tungelaumu mchakato lakini sio ukweli kwamba hicho unachokiomba kazi yake ni kusafiri (kwahio unapewa kwa dhumuni hilo)
Haya mambo ya kufanya complication katika kila jambo ndilo linafanya kuwepo na mianya ya rushwa. Wametoa tangazo ila ukiwa na ela hiyo passport hata bila safari unaipata ndani ya siku 3 kwa kutoa rushwa.
Mawazo ya ujima haya
Again tatua tatizo lililopo ambalo ni Rushwa na mchakato usio rafiki, ila sio requirement ya kuelezea dhumuni
 
Mimi naamini ni faida sana endapo watu wengi watapewa passport.
Hakuna mtu akiamua kupata passport anaikosa, dhumuni sio lazima utekeleze unaweza kuomba passport kwa kusema unategemea kwenda Kenya labda kuangalia bidhaa za Biashara sio lazima uende ingawa ulikuwa na hilo dhumuni na sio kwamba utanyanganywa baadae
Je! Kuna hasara gani kwa upande wa Serikali endapo watu wote watapewa passport?
Kwahio una-suggest zipewe bure (which is good) au watu walazimishwe kununua (which is insanity) au unamaanisha nini kwa neno wote ?
Au Serikali inahofia kuwa watu wote watasafiri na hivyo kodi kupungua?
Watu wote wakisafiri hata matumizi ya hiyo kodi yatapungua pia..., na unless kumetokea vita au hali ya hatari hakuna scenario ya kila mtu atasafiri (ukizingatia safari ni gharama)
 
Namfahamu mtu mmoja kutoka Mwanza, aliyesafiri kwenda Dar akitarajia kurejea nyumbani kwake Mwanza baada ya kufanikisha kilichompeleka Dar Es Salaam.

Lakini alipokuwa Dar, alilazimika kuunganisha safari kwenda ng'ambo. Ilikuwa ni safari ya ghafla sana na ya MUHIMU sana.

Kama asingekuwa na passport, mambo yangemharibikia.
Passport nii kama mkulima na jembe,
.huwezisema wewe mkulima wakati hata jembe nyumbani huna.

Ifike mahali tuache USHAMBA ..
Passport sio big deal kuwabana raia kusafiri.

Kama hoja za serikali ni passport kupoteza au kutokuitumia kwa wakati hilo sio jukumu la serikali.,,
Kwani passport ikipotea na renew bure?.
 
Tafsiri mbovu sana

Tofauti ya kitambulisho cha NIDA na Passport ni moja tu

Kitambulisho cha NIDA ni kitambulisho local kinachotambuliwa locally kwa local people au taasisi local

Passport ni kitambulisho cha NIDA cha kimataifa kinachotambuliwa kimataifa

Kimataifa huwezi muonyesha mtu kitambulisho cha NIDA hiki local kikadi cha NIDA

Passport ni kitambulisho tu cha kawaida tu sema immigration hawajielewi wala kuelewa kwa nini Passport inatamkwa kuwa ni haki ya kila raia!!!

Kitambulisho cha NIDA ni haki ya kika raia na Passport pia ni haki ya kila Raia

Vyote vitambulisho tu

Mtu akitaka Passport apewe tu awe ana safari au la apewe tu kama kitambulisho cha NIDA whether atakitumia popote kwa lolote au la

Akiomba kitambulisho apewe
Laba Serikali haipendi watu wake watambulike kimataifa!
 
Back
Top Bottom