Uhamiaji Tanzania, lisaidieni Taifa kuhusu Yusuf Manji. Ni raia wa Tanzania au Marekani?

Uhamiaji Tanzania, lisaidieni Taifa kuhusu Yusuf Manji. Ni raia wa Tanzania au Marekani?

Diwani wa ccm wa Mbagala kuu unamhoji uraia wake ?
πšžπš—πšŠπš“πšžπšŠ πš‘πšŠπšπšŠ πš™πšŠπš•πšŽ πšŠπš’πš›πš™πš˜πš›πš πš—πšŠπšœπš’πš”πš’πšŠ πšŠπš•πš’πš”πšŠπšŠ πš£πšŠπš’πšπš’ 𝚒𝚊 πš–πšŠπšœπšŠπšŠ πš”πšŠπšπš‘πšŠπšŠ πšŒπš‘πš’πš—πš’ 𝚒𝚊 πšžπš‘πšŠπš–πš’πšŠπš“πš’ πš’πš•πš’ πšžπš‘πšŠπš–πš’πšŠπš“πš’ πš”πšžπš“πš’πš•πš’πšπš‘πš’πšœπš‘πšŠ πš—πšŠ πšžπš›πšŠπš’πšŠ πš πšŠπš”πšŽ!! πš’πš—πšŠπšŽπš•πšŽπš”πšŽπšŠ πš”πšžπš—πšŠ πšπšŠπšπš’πš£πš˜ πšœπš’πš˜ πš‹πšžπš›πšŽ.

πš—πšŠ πšžπšœπš’πš”πšžπšπšŽ πš£πš’πš•πš’πš™πš’πšπš πšŠ πšœπš’πš–πšž πš”πš πšŠ πš πšŠπš”πšžπš‹πš πšŠ πš—πšπš˜ πšŠπš”πšŠπš›πšžπš‘πšžπšœπš’πš πšŠ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msitake kutupotezea muda na nyie Watu wa UHAMIAJI kujifanya hamjui Kitu wakati inajulikana wazi kuwa Manji aliwatoroka Kininja.

Hivi nyie UHAMIAJI pamoja na Polisi Tanzania si mliambiwa na Mwendazake kuwa hakikisheni Manji hatoroki? Ilikuwaje akawachoropoka?

au UHAMIAJI mnadhani wenye Akili hatujui ni hatua gani baadhi ya Watendaji wenu Waandamizi za Kinidhamu walichukuliwa?

Manji aliwatoroka kwa Mbinu za ' Kimedani ' kabisa tena kwa Kuvalia ' Baibui ' akapita Tanga na kuibukia zake Kenya na kusepa.

Namalizia kwa kuwaambia Manji alitorokea (yupo) sasa nchini Canada kwa Dada yake akiwacheka tu na hana mpango wa kurejea kwa sasa.

Siku zingine msitupotezee muda sawa?
Mbona nasikia ashatua nchini kati ya jana au juzi

Ukiacha ushabiki wa mipira, acha Manji arudi, kampuni zake ziliajiri Watanzania wenzetu wengi,na isitoshe alikuwa ananunua baadhi ya mazao na kwenda kuyauza India na wakulima wetu kunufaika.
 
πšžπš—πšŠπš“πšžπšŠ πš‘πšŠπšπšŠ πš™πšŠπš•πšŽ πšŠπš’πš›πš™πš˜πš›πš πš—πšŠπšœπš’πš”πš’πšŠ πšŠπš•πš’πš”πšŠπšŠ πš£πšŠπš’πšπš’ 𝚒𝚊 πš–πšŠπšœπšŠπšŠ πš”πšŠπšπš‘πšŠπšŠ πšŒπš‘πš’πš—πš’ 𝚒𝚊 πšžπš‘πšŠπš–πš’πšŠπš“πš’ πš’πš•πš’ πšžπš‘πšŠπš–πš’πšŠπš“πš’ πš”πšžπš“πš’πš•πš’πšπš‘πš’πšœπš‘πšŠ πš—πšŠ πšžπš›πšŠπš’πšŠ πš πšŠπš”πšŽ!! πš’πš—πšŠπšŽπš•πšŽπš”πšŽπšŠ πš”πšžπš—πšŠ πšπšŠπšπš’πš£πš˜ πšœπš’πš˜ πš‹πšžπš›πšŽ.

πš—πšŠ πšžπšœπš’πš”πšžπšπšŽ πš£πš’πš•πš’πš™πš’πšπš πšŠ πšœπš’πš–πšž πš”πš πšŠ πš πšŠπš”πšžπš‹πš πšŠ πš—πšπš˜ πšŠπš”πšŠπš›πšžπš‘πšžπšœπš’πš πšŠ.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasikia, huna uhakika
 
Nafikiria kama una familia inayohitaji matumizi, hii kitu sioni kama inaweza toa mkate kwa familia au jamii.
 
Wakati huu tulionao sasa hivi ni kutekeleza ile dhana mashuhuri ya "Kula na wewe ukubali Kuliwa" Hii ndiyo phylosophy inayotawala kwa sasa hivi. Sahau yote ya "Uraia na Utu"

Wakati huu tulionao sasa hivi ni kutekeleza ile dhana mashuhuri ya "Kula na wewe ukubali Kuliwa" Hii ndiyo phylosophy inayotawala kwa sasa hivi. Sahau yote ya "Uraia na Utu"

Kula nini na kuliwa kupi? Watu wengine ni wazito sana. Ukweli utakuja kujulikana tu kwamba kama mtu ni mzawa hakuna propaganda au mtu yeyote ataweza Utanzania wako wamejaribu ili kutafuta mbinu za kuwa nyanganya wana diaspora urithi wao wameshidwa, nyumba zao wameshidwa, mashamba yao wameshidwa wengine walitaka wazuie hata watu kuzikwa Tanzania wameshidwa kwa roho zao za tamaa na mbaya.

Mungu hawapagi watu wa roho hizo hata siku moja upendo ndiyo unashindaga. Kitu kimoja ambacho wengi hawajui kila diaspora ana ndugu tena wengi na wanasaidia nyumbani sana sana leo hii eti umkatalie ndugu yao kuingia nchini utakuwa umetangaza vita Tanzania! Kuna diaspora kwa mamilioni na wamegusa familia nyingi sana hakuna vibali vyovyote vitaweza kuzuia haki zao. Hayo mabaya sijui kula huku au kule mbona hatujasikia Kenya! Kwa miaka yote hii. Tatizo ni chuki tu na kila siku ziendavyo zinaahidwa.
 
Ana hela ndiyo maana anabembelezwa ukileta wewe mgogoro wa uraia ni mabomu ya machoz kwa kwenda mberee
 
Mtu kazaliwa Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ halafu leo unataka kumwita Mmarekani kwasababu ya kibali. Watanzania ni wajinga sana wakati mwingine utu wa mtu sio makaratasi yake.

Kila Mtanzania anajijua popole alipo mimi nimekaa US miaka 20 lakini mpaka leo wanasema mimi ni Mtanzania hakuna mtu anaweza kunitaja bila kuhusisha na Utanzania wangu maana Utanzania ni utu sio makaratasi siku hizi ndiyo watu wanataka kubadilisha Utanzania kuwa vitabu na vibali.

Mtu kazaliwa Tanzania ni Mtanzania awe na passport ni mambo ya sheria tu na yanabadilika kila siku lakini Manji ni Mtanzania na hakuna binadamu anaweza kubadilisha hilo passsport unapewa na watu lakini utaifa unapewa na Mungu.
Kwahiyo unatufunga midomo tusijadili wanaoukataa uraia wao japo walizaliwa nchini kwao?

Ongelea sheria, kuna Wazungu wengi wanazaliwa humu lakini sio waTz .
 
Bado mnamfuata fuata akiwa raia marekani kuna shida gani atakuja kama mwekezaji...atafuata sheria zote
Bashe alivyombiwa sio mtanzania nani akijitokeza kuhakikishia watanzania ni mtanzania sio msomali na Leo ni waziri !!??
 
Naona Jf inarudi kwenye ubora wake, umewasilisha hoja kubwa na inayohitaji intelligence kubwa kung'amua madhara ya utata wa Uraia katika uwekezaji au uchumi wa nchi.

Nakumbuka Abromovich bosi wa Chelsea alilazimika kuomba uraia wa Israel ili tu aweze kuingia Uingereza bila usumbufu baada ya kutokea mgogoro wa kidiplomasia na Urusi.

Watawala wetu hasa Wataalamu wa Uhamiaji wanapaswa kuliangalia hili suala kwa angle hizi
1. Huyu mtu alishadhalilika na naamini ana hasira na hofu yakuweka fedha zake nchini.
2. Alipata hasara kubwa
3. Kesi nyingi alizotuhumiwa nazo zilibaki kwenye majalada
4. Akiwa na haki ya Utanzania huku akiwa pia Mmarekani anaweza kujimilikisha Mali au akapewa tenda itakamlazimu akope au Kampuni zake zikope. Aki default akakimbilia Marekani tutalazimika kulipa Kama garantor
5. Wapo Watanzania na wageni wanaomjua na wenye Siri ya Uraia wake, siku wakitoka adharani huku tukiwa tumedanganywa atafedheesha dola na kiti Cha Rais pia.
6. Binadamu uishi na uondoka Duniani, tusipotenda haki tukiamini tuna miaka mia ya mashirikiano Mwenyenz Mungu anaweza akawa ametupa miaka michache, uongo wetu utawarithisha wasiostahili kuirithi nchi yetu
7. Uraia siyo Siri
8. Uraia uliofichwa unaweza kutumika kutubomoa dhidi ya mataifa mengine
9. Tusiruhusu upendeleo kwa msukumo wa rangi Wala fedha tutende Kama tunavyowatendea wasio na kitu machoni pa waona Mali.
10. Tanzania ya kesho inategemea maamuzi yetu ya leo

Kama Ni raia apewe haki yake, Kama aliukana Utanzania aishi nakuwekeza Kama mgeni.
Good. Siongezi. Maana hujajibukwa mihemuko
 
Sasa Kama utanzania wa mtu unatokana na kuzaliwa Tanzania kwanini ukaukana na unasema makaratasi siyo kitu ,hebu nenda airport bila hayo makaratasi na useme mi ni mtanzania kama utapita

Hakuna mtu amekana Utanzania yaani wanavyosema kukana ni kuchukua uraia wa nchi nyingi lakini hakuna kiapo cha kukana chochote kwasababu mfano US hawakuulizi wala kujali uraia wako saaa unakana vipi? Ni sheria za kikoloni za kukanaπŸ˜‚. Mnataka diaspora wakae hizo nchi kama watumwa au wawe ma house boy pekee? Wasiwe na bima, haki, haiwezekani na wengi wanategemewa na familia TZ kwa kutuma pesa
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kwa taarifa yako huyu manji alishinda kedi ya uraia na alirudishiwa pasi yake ya Tanzania, amezaliwa Mbagala.
 
Mtu yeyote anayeifadhiri CCM ni raia wa Tanzania,kibao kinakuja kubadilika pale ambapo mtu huyo anapoacha kuifadhiri CCM, ndipo sakata la uraia wake linapoanza na kuitwa Mrundi, Mnyarwanda, Mmarekani kama ilivyokuwa kwa Manji baada ya kumuita aliyekuja kuwa mungu mtu kuwa yeye haongei na mbwa ana ongea na mfuga mbwa.

Lakini usipoiudhi CCM udiwani utapata kwa tiketi ya CCM, ubunge utapata kwa tiketi ya CCM, tenda za serekali zitamwagika kwako kama maji ya bomba, habari za huyu ni murundi, mnyarwanda, mumarekani na habari za kupimwa mkojo hazitakuhusu.
 
Kwahiyo unatufunga midomo tusijadili wanaoukataa uraia wao japo walizaliwa nchini kwao?
Ongelea sheria, kuna Wazungu wengi wanazaliwa humu lakini sio waTz.
Fikra za kiajabu sana wanasema hatukupi kwasababu umekana sasa kama kweli mtu.

Kakana kwanini tena aombe uraia wa nchi ambayo kaikanaπŸ€” hai make sense.
 
Manji amefanya ukarabati mali zake zilizoharibiwa kwa chuki anakuja kivingine ngoja tukachangamkie ajira sijui huko alipo mwendazake na vibaraka vyake wanajisikiaje.
 
Msitake kutupotezea muda na nyie Watu wa UHAMIAJI kujifanya hamjui Kitu wakati inajulikana wazi kuwa Manji aliwatoroka Kininja.

Hivi nyie UHAMIAJI pamoja na Polisi Tanzania si mliambiwa na Mwendazake kuwa hakikisheni Manji hatoroki? Ilikuwaje akawachoropoka?

au UHAMIAJI mnadhani wenye Akili hatujui ni hatua gani baadhi ya Watendaji wenu Waandamizi za Kinidhamu walichukuliwa?

Manji aliwatoroka kwa Mbinu za ' Kimedani ' kabisa tena kwa Kuvalia ' Baibui ' akapita Tanga na kuibukia zake Kenya na kusepa.

Namalizia kwa kuwaambia Manji alitorokea ( yupo ) sasa nchini Canada kwa Dada yake akiwacheka tu na hana mpango wa kurejea kwa sasa.

Siku zingine msitupotezee muda sawa?
Utamshikilia vipi mtu asiye na kosa kwa mtu mwenye akili timamu utazama kuna kesho mabosi upita,asiye na akili ndo utenda kama Sabaya bashite kwa kuamini boss uishi milele.
 
Wahindi wengi wanauraia wa nch mbili kwa siri serikali isilifumbie macho jambo hili maana kuna siku wataingia mpaka nyeti za serikali na kuuza taaarifa za siri ya nchi
 
Back
Top Bottom