Uhamiaji Tanzania, lisaidieni Taifa kuhusu Yusuf Manji. Ni raia wa Tanzania au Marekani?

Bunge tungeni sheria inayoruhusu uraia pacha,ili nchi iweze kufaidika na diaspora wanaoshindwa kuwekeza nyumbani kwa ajili ya suala LA uraia pacha.
 
Tuache ushabiki hili suala linahitaji majibu wajameni manguli wa sheria mko wapi.

Kweli ujinga Kipaji, nguli wa sheria anasaidia nini? Na haya yana impact gani kwenye maisha yako au ya Mtanzania? Kweli umaskini ni kujitakia !
 
How does that concerns you? Ndo maana Tunabaki kuwa maskini’
Ni Haki yake kuuliza na inamhusu sana.
Mbona watu wengi tu wameteswa na hii Serikali iliyopita lakini hawakuondoka nchini?
Na wale walioondoka tulipewa taarifa zao kama wakimbizi wahanga wa Magufuli
Huyu Manji yeye hatujapewa taarifa yeyote.
So alichouliza huyu ni kutaka kujua
Je Manji ni Raia?
Au ni Mgeni aliyewekeza Nchini?
 
Nani alipaswa kukupa taarifa hiyo?
 
Wahindi wengi wanauraia wa nch mbili kwa siri serikali isilifumbie macho jambo hili maana kuna siku wataingia mpaka nyeti za serikali na kuuza taaarifa za siri ya nchi
Sera ya INDIA ni kama uchina,israel kuwa ukiwa ni mhindi unayohaki ya kuzuru,kuishi na kunufaika na India.Hiii kitu inaiingizia INDIA fedha nyingi sana kwa sababu imekua ndio chanzo kikubwa cha Export yao.Wahindi wote hawapati vizuizi vya biashara wakiwa India.Nchi yoyte ikimtendea vibaya mhindi huhesabika umemtendea vibaya mtu wao kama iwe ana maslahi ya moja kwa moja au la.
 
Mwekezaji mtanzania amerudi nyumbani kwake unahoji badala ya kufurahi ili ajira na kodi iongezeke?
Kenya , Rwanda , uganda wanamuhitaji huyu
 
Naomba kuongeza Jambo hapo, wanaotoa ajira Tanzania siyo Watanzania pekee hivyo Manji awe Mtanzania au Mmarekani akiwa na dhamira ya kuwekeza Tanzania ataajiri Watanzania tu.

Hoja iliyopo hapa na ipo kwa Watanzania wengi wenye utata wa Uraia Ni hii, ukiwekeza Tanzania Kama Mtanzania Ni tofauti na kuwekeza Tanzania Kama mgeni. Utaratibu wakufungua Kampuni upo tofauti,utaratibu wa ukaazi upo tofauti na kila Jambo unalofanya linaangaliwa kwa jicho tofauti la kisheria.

Mfano. Mgeni tartibu za kumiliki ardhi zipo tofauti na Mtanzania na ndio maana Wapo Wageni wanaokuja hapa kuomba ardhi then anaitumia hati miliki ya ardhi kwenda kwao kukopa nakuja kuwekeza. Hivyo Uraia ni components sensitive sana kuliko mwonekano wa nje wa mtu.

Lakini pia pamoja na yote lazima tukubali kuwa Tanzania ya Sasa inatakiwa kuwa nchi yakutoa majibu sahihi kwa raia wake siyo majibu ya kijanja kijanja. Huyu Bwana alituhumiwa na wanaomfahamu wanaeleza kuwa yeye na mama yake Wana Uraia wa Marekana na ukiukana Uraia wa Tanzania hasa mwanaume hakuna namna sheria inaruhusu kuurudia Tena labda tubadili sheria. Hasa Kama wanyamweze, wapare, wandengereko nk waliokuna Utanzania wanaingia nchini wanalipa visa, wanalipa vibali vya kuishi nchini Kama wageni na uwekezaji wao unatathiminiwa kwa ugeni wao ikiwemo wanapotaka kufungua Kampuni lazima wawe na share holder Mtanzania ! Manji yeye anaexption gani kushugulikia kama weusi wengine?

Tusitengeneza ubaguzi kwa kuangalia uwekezaji, Tanzania hii ni Mali yetu so kila mtu ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria zinavyotaka kuepusha mgawanjiko wa rangi au kabila au uwezo wa kiuchumi.

Nimetoa Mfano Jana; yupo Mtu alishiriki Bunge la Katiba la Tanzania akiwa raia wa Marekani bila kubainika. Juzi Kati Mhe. Rais alipomteua kwa nafasi flani wenzake walieleza huyo siyo raia wa Tanzania na ni kweli inadaiwa huyo Bwana alibainika siyo na hivyo uteuzi wake kutenguliwa. Ni kwa sababu Ni kinyume Cha sheria kumteua mgeni kwenye nafasi ya Mtanzania.

So Duniani kote Uraia ni makaratasi na hatuwezi kuyabeza tujibu hoja.

Manji Ni. Raia wa wapi?
 
Umenena vyema. Lukaku naye watasema mbeligiji! Yale makaratasi tu
 
Marekani wanaruhusu uraia pacha, na kwahiyo sidhani kama unaukana uraia wa Tanzania kama ukipata wa Marekani.
 
Marekani wana uraia pacha. Kwahiyo hawakuambii uukane uraia wa nchi uliyotokea.
 
Hueleweki hata kidogo, sio kalamu ya Great thinker hata kidogo. Utaifa hupewa na Mungu,achana na hizo pasi za kusafiria, hizo watu wanachukua kwa ajili ya kusafiria tu.
 
Ni wakati muafaka kurizia uraia pacha,
 
Washapokea rushwa
 
Welldone Mkuu umeijibu hoja kwa kutuletea hoja bora zaidi,agiza wine hapo Rubicon (red one)bill niletee inbox
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…