Uhamiaji tusaidieni kwanini passport haitumiki kama National Identification card katika baadhi ya ofisi nchini

Umejibu vizuri, lakini Kuna swali tena linahitokeza, je kwanini katika sehemu husika wanahijati kitambulisho, kupata taarifa zako rasmi kwa lengo la kukutambua au kujua kama unamiliki kitambulisho cha taifa?!!!
 
Tatizo mnajipatia umuhimu usio na sababu, na ndo maana Uhamiaji hukataa toa pass sababu ya watu kama nyie
 
Tatizo mnajipatia umuhimu usio na sababu, na ndo maana Uhamiaji hukataa toa pass sababu ya watu kama nyie
Umeilewa mada vizuri lakini?. Unaelewa kwanini hii mada imewekwa hapa?. Passport unazijua kazi zake. Tunaomba uwe seriously hapa hatuchezi boss.
 
Sababu ni kuwa hakuna intergration kati ya Uhamiaji na hizo Ofisi.

Ofisi zote huchukua taarifa kutoka NIDA including Uhamiaji...

Afu usijipe umuhimu usio na lazima maana huwezi pata Passport bila kuwa na NIDA unless ni under 18

Duh!
Kweli kuna kwenda shule na kuelimika!
Karne hii, jibu kama hili! Myopic view!
 
Duh!
Inawezekana hao waliokukatalia wenyewe hawana passport..
Mchakato wa kupata passport ni mpana mno, nadhani passport inastahili kuwa namba moja kabla ya hizo I'd za NIDA na Kura.
Ingefaa Waziri wa mambo ya ndani afafanue hili suala.
 
Umejibu vizuri, lakini Kuna swali tena linahitokeza, je kwanini katika sehemu husika wanahijati kitambulisho, kupata taarifa zako rasmi kwa lengo la kukutambua au kujua kama unamiliki kitambulisho cha taifa?!!!
Kwa kawaida au kwenye somo zima la uraia, kitambulisho cha uraia kama ilivyo hapa kwetu NIDA ndio kitambulisho cha msingi kabisa kinachotolewa katika nchi zingine mara mtu anapotimiza miaka 18. Kitambulisho hiki taarifa zake zinaanzia kutoka kuzaliwa na kwa maana hiyo kinaonyesha mtaa, kitongoji kwa maana anwani ya makazi kwa kina zaidi. Kitambulisho cha taifa kinasheheni taarifa zote za uraia na utaifa, taarifa zake kama kitambulisho mama, ndizo hutumika kuzalisha vitambulisho vingine.
Tanzania tulizembea baada ya uhuru kuhusu utambuzi wa raia na uraia. Vuguvugu la study tours, sholarships, kazi za ubaharia na zile za jumuia za kimataifa zilitukuta hatujajiandaa kwenye vitambulisho vya taifa matokeo yake pasi za kusafiria zilihitajika sana na ziliandaliwa haraka haraka kwa kutumia hati za viapo. Haya mazoea ndiyo yanayotutesa sasa wakati huu NIDA ikiweka mambo sawa.......Kwa bahati mbaya sana, watanzania tunaishi kwa mazoea zaidi kuliko mipango ya muda mrefu, ndio maana baadhi wanataka kuhalalisha pasi ya kusafiria, kitambulisho cha mpigakura,leseni ya udereva au vitambulisho vya kazi bima na vinginevyo vitumike mahali pa kitambulisho cha NIDA....Hii sio Sawa.
 
Single mother kaa kwa kutulia kahaba wa baa wewe
 
Hili Tangazo lilitolewa lini?

Passport ni kitambulisho chenye uhakika zaidi kuliko NIDA.
 
Ila passport ni pasi ya kusafiria ila NIDA NI ID YA UTAMBULISHO KWAMBA WE NI MTANZANIA .... NAFIKIRI FOREIGNER LABDA NDIO WANGEITAJI PASSPORT YAKE LAKINI BORN HERE HERE LAZIMA NIDA IHUSIKE TU SIJAONA KOSA KWA KWELI
Hata Mgeni anapewa NIDA?
Unataka kusemaje?
 
Sababu ni kuwa hakuna intergration kati ya Uhamiaji na hizo Ofisi.

Ofisi zote huchukua taarifa kutoka NIDA including Uhamiaji...

Afu usijipe umuhimu usio na lazima maana huwezi pata Passport bila kuwa na NIDA unless ni under 18
Kuna watu wana Hati ya kusafiria lakini hawana Nida
 
Kukosa tu logic. National ID ni information inayohitajika kupata passport. Kwa muktadha huo, huwezi kuwa na passport kama huna national ID
 
Hili Tangazo lilitolewa lini?

Passport ni kitambulisho chenye uhakika zaidi kuliko NIDA.
Kwa mtazamo wako ndivyo, lakini unapaswa kujua maana halisi ya neno passport (Hati ya kusafiria)... Ni kitambulisho ndio kimataifa kwa raia anaesafiri nje ya mipaka yetu. Ndani ya nchi ni NIDA hata kama huiamini.

Taarifa zilitolewa pale passport hizi mpya za kielektroniki zilipoanza kutolewa. Kama hufuatilii matukio kama haya ni wazi utalalama sana, lakini fika ofisi yoyote ya uhamiaji, utapata ufafanuzi murua.
 
Hata Mgeni anapewa NIDA?
Unataka kusemaje?
Ndio, kipo kitambulisho cha NIDA kwa wageni pia. Kwa wakimbizi na wageni wakazi halali wa nchi hii.
 
Halafu inaonekana Kuna vitu vina kutatiza
Sio hati ya kusafiria bali ni pasi ya kusafiria.

Pasi ya kusafiria ni nyaraka anayopewa Mtanzania pekee.

NIDA ni kitambulisho Cha Taifa ambacho wanapewa raia na wasio raia ili mradi wanaishi nchini Tanzania.

Ndio maana Simbachawene alisema kuwa na Nida haikuzuii kuhojiwa na immigration ila mtu mwenye passport kumnyang'anya ujue ni safari ndefu.

Pasi ya kusafiria inaweza kutumika au utumika kama dhamana kwenye taasisi za fedha, Mahakamani wakati NIDA ni supporting documents.
 
Unahitaji kujielimisha zaidi kwenye hili, unajichanganya kwenye tafsiri na kazi za nyaraka mbili ambapo NIDA ndio msingi wa vyote. Jipe muda utafakari zaidi, ukikwama waulize wenye fani zao... Usiwe mbishi, hukuna ligi hapa.
 
Unajuaje na anaye kujibu kama sio[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Unajuaje na anaye kujibu kama sio[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Ok kama wewe unaenijibu ni mmoja wa wataalamu kwenye fani hii, Basi una mapungufu;... nakushauri ujielimishe zaidi kuhusu utendaji wa mamlaka za RITA, NIDA na uhamiaji ....kwa vyovyote vile kwa mtazamo wako huo, utapotosha wengi wasiojua. Na kumbuka hizo mamlaka tatu, utendaji wake ni wa kiulimwengu hivyo viwango vyake vinalingana Ulimwengu mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…