Uhamiaji tusaidieni kwanini passport haitumiki kama National Identification card katika baadhi ya ofisi nchini

Uhamiaji tusaidieni kwanini passport haitumiki kama National Identification card katika baadhi ya ofisi nchini

Uongo

Ukiwa mgeni sawa lakini mwenyeji kitambilisho kikubwa na cha NIDA
Nikuulize tu YEHODAYA . Hivi nje ya mipaka yetu hicho kinida kinatambulika na kuheshimika ?!. Kama ukiwa popote duniani ukitoa passport tena hii ya kisasa (electronic) taarifa zako zinajulikana popote, kwanini ofisi zetu wenyewe iidunishe passport yetu ?!

Hii inanikumbusha kungangania kiswahili humu mwetu. Ingawa ukitoka tu nje ya mipaka yetu tu, hakuna anaekuelewa wala mawasiliano ya kiswahili. Narudia kusema kinachowasumbua viongozi na taifa letu, ni mentality za ki communist. Nothing more , nothing less
 
Kumbe na wewe upo mtupu upustea! Maana ya Passport au pasi ya kusafiria ni nini? Je, kwenye maofisi hayo unakuwa unasafiri nje ya nchi?
Wewe ndio huelewi boss, naomba tafuta maana ya passport kwenye literatures usieleze vile unavyoelewa wewe.
Kuna baadhi ya nchi hata hiyo NIDA ni kitambulisho cha kusafiria.
 
Maana sio Nida haikutambulishi vizuri kama mtanzania ila inakutambulisha ukisafiri tu nchini mwa watu ndio maana Kuna passport na Kuna Identification Card so ni vitu tofauti sana ndio maana watu waliokuwa hawana uraia wanalipia uraia huo
Passport ya Tanzania anaweza kuipewa mtu asiye raia wa Tanzania ?
 
Unamaanisha namba ya kitambulisho cha NIDA au kitambulisho chenyewe kabisa??
Mkorofi tu huyo ndio maana wamemgomea kumpa huduma

Passport mtu hapati hadi awe na kitambulisho cha NIDA kwa nini asiprleke hicho kitambulisho kakomaa tu kuwapa passport?

NIDA anayo kinachomfanya akomae kuwa lazima wakubali passport ni nini?

Waliomkatalia kumpa huduma wako sahihi
 
Incompetence ni tatizo kila mahala katika nchi hii...tuache hizi biashara za kamlete kwenye maofisi, watanzania tena vijana wadogo kabisa wenye akili ya kuisadia hii nchi wapo mitaani huku wanadhurula tu na bahasha zao.
 
CCM inaulea sana ujinga kwa manufaa yake lakini madhara ya ujinga ni makubwa sana na kila siku unaacha makovu makubwa kwenye jamii.

Faida CCM inapata kukumbatia ujinga ni ndogo sana kulingana na hasara Taifa linapata kwa tabia hii ya Chama CCM.

Piga vita ujinga nchi ipone.
 
Wakati wa kujaza form za kuomba NIDA kulikua na sehem inahitaji mhuri wa uhamiaji. Nikaenda wanigongee, wakasema wanataka uthibitisho kwamba mie ni mtanzania. Nikatoa passport ambayo inatolewa na mamlaka hiyo hiyo ikinitamvulisha uraia wangu kwamba mtanzania, wakanigomea. Nikauliza inamaana hamuiamini hata document mliyoitoa wenyewe?

Nikaachana na Hilo zoezi Hadi siku nimekutana na jamaa tunafahamiana nae nikamweleza akaenda nayo ndani na kurudi ikiwa imegongwa mhuri akaniomba radhi Kwa usumbufu.
 
Sababu ni kuwa hakuna intergration kati ya Uhamiaji na hizo Ofisi.

Ofisi zote huchukua taarifa kutoka NIDA including Uhamiaji...

Afu usijipe umuhimu usio na lazima maana huwezi pata Passport bila kuwa na NIDA unless ni under 18
Mkuu kwani NIDA wapi chini ya nani kama sio haohao uhamiaji yaani hapa tukubali tukatae hili linchi linamambo ya kiwaki
 
Nimekwenda ofisi kama tatu za watu binafsi nimeshindwa kupata huduma kwa kutumia kitambulisho cha passport eti hakitambuliki. Yaani kitabu hakitambuliki?

Ni kweli karne ya 22 kuna baadhi ya ofisi hazitambui kama passport ya kusafiria ni kitambulisho.

Wananiambia hicho hakitambuliki sisi hapa tunahitaji NIDA tu.

Kweli nimeshangaa nimejisemea hiki sasa ni nini. Nimetamani kuutangazia uma palepale kuitambua passport kama kitambulisho kwenye ofisi zote za serikali na binafsi.

Passport na NIDA kipi ni kitambulisho.

Uhamiaji tusaidieni ni kwanini passport haitumiki kama National Identification card baadhi ya ofisi.
Hili hutokea only kwenye nchi ambayo haiheshimu utawala wa sheria
 
Kwanza kuipata unaambiwa lete barua ya muariko wa unakotaka kwenda hapo palipo na shida kumbe huwezi kuipata bila sababu ya kutoka nje
Sababu dhaifu.
Ukitaka kutalii au kusafiri kibiashara nani atakualika?
 
Wewe ndio huelewi boss, naomba tafuta maana ya passport kwenye literatures usieleze vile unavyoelewa wewe.
Kuna baadhi ya nchi hata hiyo NIDA ni kitambulisho cha kusafiria.
Ujuaji mwingi, fanya utafiti! Kila nchi na masuala yake. Sijawahi kuona nchi inayotumia passport kama Kitambulisho kwa raia isipokuwa kwa mhamiaji au Mgeni! Kwa uwanja wako wa kujidai -gesi na mafuta hatutii neno ila unapokuja tunapojua, ukiteleza tunakupa tu
 
Mkuu kwani NIDA wapi chini ya nani kama sio haohao uhamiaji yaani hapa tukubali tukatae hili linchi linamambo ya kiwaki
Nida wako Wizara ya Mambo ya Ndani

Uhamiaji ni Jeshi linalojitegemea ila Wizara ya mambo ya Ndani
 
Ujuaji mwingi, fanya utafiti! Kila nchi na masuala yake. Sijawahi kuona nchi inayotumia passport kama Kitambulisho kwa raia isipokuwa kwa mhamiaji au Mgeni! Kwa uwanja wako wa kujidai -gesi na mafuta hatutii neno ila unapokuja tunapojua, ukiteleza tunakupa tu
Kwanza ni ushamba kutembea na passport kama kitambulisho wakati ili upate passport inakubidi uwe na nin
 
Ujuaji mwingi, fanya utafiti! Kila nchi na masuala yake. Sijawahi kuona nchi inayotumia passport kama Kitambulisho kwa raia isipokuwa kwa mhamiaji au Mgeni! Kwa uwanja wako wa kujidai -gesi na mafuta hatutii neno ila unapokuja tunapojua, ukiteleza tunakupa tu
Naomba fuatilia nchi zingine boss uone kama passport sio kitambulisho. Fuatilia UK, CANADA, etc.
 
Acha ushamba basi kama huelewi bakia hivyoo hivyoo nakupa maelezo mazuri hausikii unauliza maswali kaulize ofisini Sina energy
Lakini amekuuliza vizuri tu. Ulipaswa kumjibu kama inawezekana au haiwezekani. Na ukiingalia passport ina details zote ambazo zipo kwenye NIDA.
 
Back
Top Bottom