Uhamiaji Zambia walitaka kunifunga kisa kuongeza siku

Labda ukali wao ni kwa sababu ya wazamiaji wanaotumia route ya Zambia kwenda Bondeni...
 
Aisee umenikumbusha mwezi wa tatu tu apo niliendaa malawi kuna mizigo nilikuwa nafutriaa kule kuna geti tatu kutoka mpakani mpaka wilaya kalonga . geti la kwanza nikavuka salama la pili nikavuka vizuri huku roho inalia paa.. geti la tatu sasa ndiyo kimbembe.. kwanza wadau wal liambiwa niwe naongea kilugha chetu kinaendana na lugha yao sasa yure bwana kaniuliza swali nikajibu vzurii tu kaniuliza nimwambie waziri mkuu wao anaitwa nani😂😂 nikawa namuangalia tuu kaona haitoshi kaniambiaa nimpe simu yangu kaenda moja kwa moja wasap kakuta kiswahili kitupu kama kuna kitu sijawaza ni kuhusu smu kama ataingia waspu.. badae nikashushwa na kuniweka chini ya ulinzi sina chochote yani.. we sikia tu
Badae dereva akaja kunisadiaa tulimpaa kama 30k iv ya bongo.. kwetu huku wala hata hawasumbuliwi..
 
Akili zetu za kiafrika hizi, bado wiki mbili kwanini wanataka kukuweka lockup, wamelewa madaraka
Labda walikuwa wanataka kumtoa chochote wakaona haelekei kabisaa.
 
Reactions: Lax
Zambia,Malawi,Mozambique zote nchi za kijingajinga rushwa imekuwa ni lazima sio ombi uwe na kosa usiwe na kosa ni Sawa Sawa,Zambia nilipita kipindi cha corona na mipaka ilikuwa imefungwa kipindi hicho nilienjoy show,mwisho wa siku sio kuhusu uhamiaji tu ni kwamba wananchi wa nchi hizo wamezaliwa na roho mbaya
 
Mi nilikuwa na bahati sana sijui kwa sababu ya muonekano yaani wakinikuta kwenye gari nasafiri watapekuliwa wengine tu mi wananiacha alafu mbaya zaidi hata lugha Yao sijui (kitumbuka)
Una lisura lipana kama walivyo wao, Kam sivyo basi una asili ya mbeya na weusi wa kifipa
 
Ndio inabidi tuwaongezee nguvu Immigration Tanzania na kuanzisha detention center Ili waweze kuwanyoosha raia wa kigeni na wenyeji wanaokiuka Sheria.

Mtanzania aliyetoka nje ya nchi, akirudi bongo Huwa na mawazo tofauti na wahapa hapa.
 
Mkuu naomba niku DM nikuulize kitu maana nilikuwa na maswali nataka muuliza mtu aliyeko huko au yupo na uzoefu huko.
 
kweli aisee
 
Noma sana pole mkuu
 
unawakosea walikuwa sahihi ,mtukutu huyu alitaka kwenda kuongeza wikimbili nyingine wakati mkononi anawiki mbili mbele. wakashituka kwann aombe nyingine wakati anazo tayari
Na vipi ningezidisha siku ningekuwa ndio mwema au??
 
Umenikumbusha mbali BODA ya BUSIA. Hongo nje nje.
Kazi ni kipimo cha utu
 
sio migration ni immigration
 
Aisee, next time nitakupeleka Somalia ukafurahie muziki wake
Somalia,SA,Zimbabwe sijui Mozambique hawafikii kwa Wazambia mazee hapo sikia tu mtu unarudi zako nyumbani unashushwa kwenye Bus wakiona vibali havieleweki wanakupeleka ndani harafu utatokea mahakamani pana kondakta mmoja wa Taqwa alikua anafanya mazoea kwa sababu kila siku anapita muda mwingine passport yake anaenda akirudi agongi Tunduma wakati Bus linaonekana limetoka Daslm alitoa hela zote walikataa alibaki pale kama mwezi hivi ndio akatokea mahakamani na mtu kapita njia hiyo zaidi ya miaka 10...
Mimi Wazambia nakua kamili ila pia hawawezi kugundua kwa sababu naongea Kinyanja vizuri wao ukijua lugha basi ni rai kama Malawi hawana mambo mengi..
 
Zambia Migrations yao ni kitu chengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…