Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ni wazi matokeo yoyote ya ushindani, minyukano na uhasama wa kisiasa baina ya viongozi wanao gombea nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa, kutaidhoofisha chadema yenyewe na kuimarisha vyama vingine vya siasa nchini, ikiwa ni pamoja na chama tawala.
Hakuna atakaeshinda uongozi wa chadema Taifa, atafanikiwa kuongoza chama hicho kwa amani, ispokua kwa hujuma za makusudi za mara kwa mara, hususani kutoka kwa masalia ya viongozi na wafuasi wa mgombea uongozi alieshndwa katika uchuguzi huo kama kisasi.
Ndiyo maana kila mgombea hususani baina ya mafahali wawili wa nafasi ya uenyekiti anadai kwamba, asiposhinda uchaguzi huo chadema huenda chadema ikafa. Ni wazi hakuna utashi wa kisiasa baina yao, hakuna mwenye nia wala dhamira njema na chadema.
Aina ya vita ya maneno wanayopigana wagombea uenyekiti wa Chadema Taifa, inajenga uhasama na kuibua vidonda na majeraha yasiyosameheka baina yao na hivyo kuzidisha na kuchochea chuki ya kudumu ambayo inaweza kusababisha hatari zaidi, uharibifu na pengine hata maafa ya kisiasa.
Kutuhumiana kunakoendelea bila ushahidi kupitia mahojiano kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi baina ya wagombea kunaelekea kubaya zaidi hadi kugusa maisha binafsi na ya kifamilia ya wagombea hao, na hii ni hatari zaidi.
Vita hii haiwezi kuisha salama, na ikitokea basi itakua ni kwa unafiki wa kiwango cha juu sana, kama ambavyo mara zote wagombea uongozi hao wa chadema Taifa hutabasamiana kinafiki huku mioyoni mwao pakiwa na chuki binafsi ambayo sasa ndiyo wanaielezea kwa umma kwa maneno.
Kwa majeraha mabaya sana wanayo endalea kujeruhiana wagombea uongozi wa chadema ngazi ya Taifa, hayupo miongoni mwao atakae fanikiwa kuiongoza Chadema kwa amani na utulivu, kwasababu huyo mwingine atakua akihujumu jitihada za mwingine kama kisasi, na hiyo inaweza kua fursa na nafasi kwa vyama vingine vya siasa, kuvuna wafuasi wa chadema watakao kua wamechoshwa na vurumai na songombingo za Chadema na uongozi wake.
Una maoni gani kama mdau wa siasa za ndani ya chama kinachojiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo?🐒
Mungu Ibariki Tanzania