Uhasama wa kisiasa, kugawanyika na kusambaratika kwa CHADEMA kutaimarisha vyama vingine vya siasa nchini

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni wazi matokeo yoyote ya ushindani, minyukano na uhasama wa kisiasa baina ya viongozi wanao gombea nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa, kutaidhoofisha chadema yenyewe na kuimarisha vyama vingine vya siasa nchini, ikiwa ni pamoja na chama tawala.

Hakuna atakaeshinda uongozi wa chadema Taifa, atafanikiwa kuongoza chama hicho kwa amani, ispokua kwa hujuma za makusudi za mara kwa mara, hususani kutoka kwa masalia ya viongozi na wafuasi wa mgombea uongozi alieshndwa katika uchuguzi huo kama kisasi.

Ndiyo maana kila mgombea hususani baina ya mafahali wawili wa nafasi ya uenyekiti anadai kwamba, asiposhinda uchaguzi huo chadema huenda chadema ikafa. Ni wazi hakuna utashi wa kisiasa baina yao, hakuna mwenye nia wala dhamira njema na chadema.

Aina ya vita ya maneno wanayopigana wagombea uenyekiti wa Chadema Taifa, inajenga uhasama na kuibua vidonda na majeraha yasiyosameheka baina yao na hivyo kuzidisha na kuchochea chuki ya kudumu ambayo inaweza kusababisha hatari zaidi, uharibifu na pengine hata maafa ya kisiasa.

Kutuhumiana kunakoendelea bila ushahidi kupitia mahojiano kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi baina ya wagombea kunaelekea kubaya zaidi hadi kugusa maisha binafsi na ya kifamilia ya wagombea hao, na hii ni hatari zaidi.

Vita hii haiwezi kuisha salama, na ikitokea basi itakua ni kwa unafiki wa kiwango cha juu sana, kama ambavyo mara zote wagombea uongozi hao wa chadema Taifa hutabasamiana kinafiki huku mioyoni mwao pakiwa na chuki binafsi ambayo sasa ndiyo wanaielezea kwa umma kwa maneno.

Kwa majeraha mabaya sana wanayo endalea kujeruhiana wagombea uongozi wa chadema ngazi ya Taifa, hayupo miongoni mwao atakae fanikiwa kuiongoza Chadema kwa amani na utulivu, kwasababu huyo mwingine atakua akihujumu jitihada za mwingine kama kisasi, na hiyo inaweza kua fursa na nafasi kwa vyama vingine vya siasa, kuvuna wafuasi wa chadema watakao kua wamechoshwa na vurumai na songombingo za Chadema na uongozi wake.

Una maoni gani kama mdau wa siasa za ndani ya chama kinachojiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mkuu inaonekana kwenye uchambuzi wa siasa upo shallow sana tofauti na unavyojinasibisha.

Kutofautiana mawazo na mitizamo ya kisiasa sio uhasama au ugomvi kama unavyotaka ieleweke humu, isipokuwa hayo ni matamanio yako kuwa ukinzani huo uwe uhasama.

Mkuu hilo ni joto la kisiasa na baada ya uchaguzi maisha yataendelea kama kawaida.
 
Huko kwenu mshampitisha au maana naona hakuna.mvuto tena
 
Hata CCM ndio imekwisha hivyo imebaki kununua mabasi ya kusomba mabwege.
 
Huko kwenu mshampitisha au maana naona hakuna.mvuto tena
kwenye vyama vya siasa vingine Tanzania hali ni shwari kwa kiasi kikubwa,

hata hivyo,
katika siasa suala la mvuto ni ushirikina gentleman,
ni muhimu kuzingatia, hoja, mipango, uadilifu na umahiri wa viongozi
 
kwenye vyama vya siasa vingine Tanzania hali ni shwari kwa kiasi kikubwa,

hata hivyo,
katika siasa suala la mvuto ni ushirikina gentleman,
ni muhimu kuzingatia, hoja, mipango, uadilifu na umahiri wa viongozi
Mmeshampitisha, kazi ndogo ya kufanya hata kwenye simu mnakusanyika na magari na kuleta fujo barabarani kwa ajili ya kumpitisha makamu huo ni unyumbu kwakweli
 

Kwa hiyo Bakhresa akifilisika Chid Benzy ataimarika?
 
kwahiyo kumbe wagombea uenyekiti wa chadema wanatuhumia na kutwezana utu na familia zao hadharani, huku wake zao, watoto wao na familia zao wakishuhudia sio uhasama, right?

au mpaka maafa yatokee ndipo uelewe kwamba ni uhasama right?

walisema chadema hakuna mpasuko, hivi sasa wao wenyewe wanakiri wamegawanyika vibaya sana,

sasa wewe una mbwelembwela hapa ati hakuna uhasama,
huenda unaamini katika ushirikina
 
Hatuombei, ila CDM kama itakufa watu watakata tamaa kabisa, CCM itatawala itakavyo.
Hao wanaharakati uchwara watatumia muda mrefu sana zaidi ya miaka 20 kuwashawishi tena watanzania kuwaamini endapo watafanikiwa kufanya mapinduzi ndani ya CDM.

Tumeona mwanaharakati mmoja kàanza kutembeza bakuli ili kutakatisha fedha zake kutoka kwa mabeberu.
 
Siasa ya kumkomboa Mtanganyika na kuleta maendeleo makubwa kama Asia na Ulaya ni ndoto. Anayethubutu lazima afe, adhurike kama Mtikila, Lissu nk. Sijaelewa matrilioni wanayojilimbikizia viongozi wa nchi hii yanawapa furaha gani wanapoona maskini wakifa kwa magonjwa yanayotibika na kukosa chakula. Maskini nchi yangu.
 
Mkuu pilipili usiyoila yakuwashia nini?? wakilumbana, wakigombana, wakitwezana au wakisambaratika unaadhirika vipi upande uliopo??

Si ulipaswa kuchekelea kabisa??? Siku hizi hauko sawa sawa kadri siku zinavyoenda.

Mkuu jifanyie taathmini ya afya, unahitaji tiba ya saikolojia na ikiwezekana afya ya akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…