RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara (69)✍️
Zipo familia au koo ambazo hazina maelewano miaka nenda'rudi. Yaani ukoo fulani hauelewani na ukoo fulani, familia fulani haielewani na familia nyingine, au ndani ya ukoo mmoja hakuna maelewano kati yao.
Gomvi nyingi za familia na ukoo zinakwamisha mafanikio kwa watoto na wajukuu. Watoto na wajukuu wanashindwa kuoana, kukaribishana, kusali pamoja, kusaidiana, kula pamoja, au kupeana "connection za kazi kwasababu ya familia, koo, au wazazi wao hawapatani kwa miaka mingi.
Gomvi nyingi zinatokana na chanzo cha migogoro ya mipaka ya mashamba, dhuruma za viwanja, urithi wa mali, imani za kishirikina, uchonganishi kutoka kwa majirani wabaya, wivu wa maendeleo, n.k. Mbaya zaidi watoto au wajukuu wanarithi na kuendeleza uadui wa wazazi au ndugu zao, matokeo yake wanashindwa kufanya mashirikiano ya maendeleo.
MWISHO: Ewe mtoto usirithi adui wala uadui usiokuwa na faida kwenye maisha yako. Lakini pia familia na koo mnapokuwa na uadui tambueni kwamba mnaweka vikwazo na mipaka ya mafanikio kwa watoto na wajukuu wenu.
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM