Uhuni wa DAWASA, Maji hakuna lakini wanaleta bili kubwa kuliko wakati wowote ule

Msiache mabomba/koki wazi. Usiku wanafungulia upepo unasukuma units mbele wakati maji hakuna.
Hawafungulii upepo.

Kama maji yamekatika, bomba zinabaki na hewa tu. Maji yakianza kutoka, upepo uliojaa kwenye bomba unasukumwa na ulivyo na mguvu huzungusha mita haraka kuliko maji.

DAWASA wafunge mita zenye uwezo wa kutoa upepo kwanza kabla ya maji kuanza kutoka
 
Wakija wale wasoma mita,anzia pale kusoma mita yako mpaka watakapokuja tena utajua cubic metres zako ulizotumia
 
Sisi wametuletea bill ya mwezi huu harafu wakasema tuna Deni la 54000 ajabu ni kwamba Hilo Deni haliko na katika kumbukumbu za bill hatujawahi kupata bill hiyo,
 
Kuna haja ya raia kuhakiki namba zao za mita wenyewe ili wajue mwezi uliopita mita iliishia namba fulani na sasa imesoma namba fulani.

Kuna uhuni kwenye kukadiria matumizi, wanainflate bili hawa
Sidhani. Hata mimi nilikua na mtazamo kama huu na nilshabishana nao sana, lakini baadaye ikagundulika tatizo lipo kwangu. 9 times out of 10 ukiona bill ya maji imekuwa kubwa sana kuliko kawaida ujue kuna leakage kwenye mfumo wako wa maji. Wasoma meter wa DAWASA wapo honest sana hata on a one-to-one level ukifahamiana nao.
 
Sa ivi kila sector ina maamuzi yake, tuendelee kuvumilia ila ipo siku
 
Kusema DAWASA wanakudai 80,000 baada ya mgao bila kujua matumizi yako ya nyuma haisaidii lolote.

Angalau ungeweka ushahidi wa past bills zako za nyuma kwa miezi kadhaa hadi latest water bill tuone matumizi yako kwa mwezi kwa kipindi fulani.
 
Was just a joke ndugu. Nafahamu hilo ila juzi walisema wanatoaga upepo kabla ya kuachia maji. Sasa sijui wanatoaje sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…