Uhuni wanaofanyiwa vijana waliokuja kwenye usaili wa kada ya afya kituo cha shule ya Sekondari Galanos, Tanga



Twende taratibu. Kitambulisho kinachotambulika serikalini ni NIDA (barua kutoka serikali ya mtaa kama huna NIDA), Leseni ya Udereva, Hati ya Kusafiria na Kitambulisho cha kupigia kura. Hao vijana wako wameenda na nini na wameambiwa waoneshe nini??​
 
Kama kweli hizo additional identification badges hazikuwepo kwenye barua ya wito wa interview basi huo mchakato ni batili.

Huwezi kuongeza vigezo vyako ambavyo havipo kwenye tangazo tena unasubiri wasailiwa wafike ndio useme hivyo.

Ikumbukwe watu wametoka sehemu tofauti tofauti hivyo kumfanyia surprise ya viambatanisho vya ziada ni sawa na kumnyima haki ya fair opportunity.
 
Sasa mkuu si uzioneshe hizo additional IDs? Ni kama zipi?
It will not add any value maana wamesha fukuzwa. This is to notify the concerned authorities to take action. Wakitaka ushahidi watawapata waliotimuliwa!
Mimi nimepewa taarifa na kijana ambaye anarudi Dar baada ya kutakiwa ids ambazo haziko kwenye tangazo
 

Attachments

Azitaje kwaza ni zipi? Ambazo zimeongezwa
 
Huu uzi ni takataka mpka hizo id zitakapotajwa.
 
Unawezaaa kuchizikaa hivii hiviii wallah, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hao madktari hawajawahi kwenda dodoma interview waone jinsi watu wanavyorudishwa wakikosa moja ya vigezo! Wale sio mjomba zako kwamba utalia lia usamehewe mkuu! Fuata taratibu wakikuambia fika kwa wakati fanya hivyo! Vinginevyo hata hiyo ya kutokutimiza vigezo ni moja ya usaili! Usaili unaanzia kwenye vitambulisho, vyeti, ndo maana unaitwa mchakato! Ukiona umeitwa kwenye usaili mchakato wa usaili unaanza toka ulipoitwa kwenye usaili! Vijana kuweni makini!
 
Mods ondoeni huu uzi. Umejaa taarifa ambazo mleta mada ameshindwa kuzithibitisha na hivyo zinaangukia kundi la umbea na majungu. Hatuwezi kuwa tunarely kwenye taarifa za namna hii. Mleta mada waambie vijana wako next time wakienda kwenye usaili wazingatie kwenda na requirements zote kwa mujibu wa tangazo na wakizuiwa kuingi kwenye usaili wapeleke taarifa rasmi PSRS ikiwemo na ushahidi.​
 
Nje ya box wapi boss kwa mtu aliyesoma kwa mkopo udaktari? Afungue hospitali yake?
Kwani ni lazima dakitari kujiajiri afungue hospitali? Hapana kuna madakitari wengi wako nje ya fani zao udakitari kaufanya kama addtional income.......
 
hjasoma uzi ukauelewa1 Read between lines!
 
Kwani ni lazima dakitari kujiajiri afungue hospitali? Hapana kuna madakitari wengi wako nje ya fani zao udakitari kaufanya kama addtional income.......
Nyie mnaongea mko kwenye ulaji, au wazazi wenu wako vizuri kifedha

Watoto wa maskinii, wanaliaa na kusaga meno. [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Nyie mnaongea mko kwenye ulaji, au wazazi wenu wako vizuri kifedha

Watoto wa maskinii, wanaliaa na kusaga meno. [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
Mkuu sio kweli ni kujitoa na kufanya hassling tu, ila watanzania wengi hupenda spoon feeding, hawataki critical thinking kupambana na umasikini.
 
Sasa mkuu si uzioneshe hizo additional IDs? Ni kama zipi?

Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka
Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka

Kijana ana kitambulisho cha kura, anaambiwa alete pia barua ya mweyekiti wa ktaa/kijiji...what next? anaondoka maana hawezi kupatahiyo barua in asuch a short time wakati ana utambulisho mwingine ulioainishwa hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…