Uhuni wanaofanyiwa vijana waliokuja kwenye usaili wa kada ya afya kituo cha shule ya Sekondari Galanos, Tanga

Ukienda kwenye interviews jiandae nilishawahi kuwafanyia watu usahili ilikua ni madereva kwenye oral interview nikamuomba dereva mmoja anionyeshe kijiko alivyokikosa ikawa sababu ya kumnyima kazi
Sasa jiulize kijiko na udereva wapi na wapi
 
Kwani ni lazima dakitari kujiajiri afungue hospitali? Hapana kuna madakitari wengi wako nje ya fani zao udakitari kaufanya kama addtional income.......
Kama nini boss? Usome udaktari halafu ukawe mchuuzi? Tuwe tunajaribu kuelewa mazingira ya graduate wetu. Kwanini ukafanye kazi nje ya fani uliyosomea miaka 11? Kuna mazingira inaweza kutokea hivyo ila katika hali ya kawaida si sawa. Mtu kasoma udaktari, akawe daktari. Mbona mikoa na wilaya nyingi tu zinawahitaji? Kwamba tumefikia level nchi haiitaji madaktari kiasi cha kwamba ukisoma udaktari ukamaliza unaweza endesha boda kwa kukosa kazi?
 
Mfano
 
Mkuu Tanzania ajira bado zipo nyingi za udakitari za ualimu ila uwezo wakulipwa na serikali haupo kabisa, unakuta shule ya msingi ina wanafunzi 1000 ila waalimu ni 5 tu, hospitali hazina madakitari........Wa Tanzania hatutaki kujiongeza na kujitafuta kuna dakitari moja amefungua duka hapa kwetu udakitari unaufanyia nyumbani kwake kwa wale wanao mfahamu anatoa ushauri na connection za utabibu kipato chake kiko juu sasa kupita wale walio ajiliwa, hawezi kurudi serikalani tena.
 
Kwa mfano k
Mfano kigezo gani kimewarudisha hakikuwepo kwenye tangazo!???

Acheni siasa nyie
 
Upo sawa ila graduate wengi pangu pakavu, wanasubiriwa wamalize waanze kusaidia wadogo na ndugu zao. Akikosa kazi unwambie fungua duka hata huo mtaji tu wa kufungulia duka hana achilia mbali eneo la kufungua hilo duka.
 
Upo sawa ila graduate wengi pangu pakavu, wanasubiriwa wamalize waanza kusaidia wadogo na ndugu zao. Akikosa kazi unwambie fungua duka hata huo mtaji tu wa kufungulia duka hana achilia mbali eneo la kufungua hilo duka.
Lakini kumbuka huyu mtu anaweza kukopa au kutafuta pesa kwa marafiki na ndugu ili afunge ndoa ya 15 hado 30m ila hawezi kukopa kuanzisha biashara ndogo
 
Kwa muktadha huo naweza sema vijana wako ni wazembe!!
Kwani figisu za bongo hawazijui?
Hapo alitakiwa kuchukua barua serikali ya mtaa na kuambatanisha pamoja na vitambulisho alivyo navyo maana hata kufungua AC bank ukienda na NIDA bado watataka barua ya mtaa/kijiji
 
Kuzingatia maelekezo ni sehemu ya usahili. Hivyo kama wamerudishwa ujue wamefeli usahili, jiulize kwanini kuna walioingia. Maelekezo yalisema wasahiliwa waje na vyeti orijino msahiliwa anakuja na copy ya rangi unataka msimamizi afanye nini!!? Umeambiwa njoo na barakoa wewe huna, msaili akufanye nini sasa!
 
Hii tume itafutwa soon kama ilivyo skuli ya sheria
 
Lakini hii haiondoi ukweli kua degree holder wa procurement TAMISEMI anaanza na TGS D<800,000/=,huku MD akianza na TGHS E~1,550,000/=,...........Acha vijana wapambane
 
Nyie mnaongea mko kwenye ulaji, au wazazi wenu wako vizuri kifedha

Watoto wa maskinii, wanaliaa na kusaga meno. [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
fact fact fact nafikiri ni maumivu ya kudumu kwa wale wanaotoka kwenye familia/kaya duni
 
Kwa hiyo serikali inataka kufunika upungufu wa watumishi hao Kwa kuuaminisha umma kuwa upungufu huo ni Kwa sababu wataalamu wapi mtaani kisa wali fail interview? Nchi ngumu sana hii
 
Hiyo inaitwa utajua hujui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…