Malalamiko hayasaidii ndugu, wajipange tena msimu ujao. Baadhi ya wasaka ajira huwa wanachukulia mambo easy, tena hata kutafuta taarifa sahihi kwao ni mzigo. Wafuatao ndio wahusika anaoongelea mleta mada
1. Vijana walioenda na copy za vyeti zenye rangi na kuweka lamination, wakati wametangaziwa waende na vyeti halisi.
2. Walioenda na vyeti vyenye majina tofauti bila deed pool au affidavit (supporting documents)
3. Walioenda bila leseni au leseni zilizoisha muda. Wengine wameenda na risiti za malipo ya leseni.
4. Mtu anaenda na picha ya kitambulisho iliyopigwa ipo kwenye simu (softcopy ya NIDA). Vitambulisho vinavyokubalika vimeorodheswa ila mtu anaenda na kitambulisho cha chuo aliposomea.
Hayo makundi manne ni walalamikaji wasio na mashiko. Usaili unahitaji umakini, moja ya sehemu ya interview ni kufuata maelekezo.
Next time wajitahidi kufuata maelekezo sio ukaidi.