Uhuru Kenyatta atumia jeshi baada ya mgomo wa wafanyakazi JIA, lakini akitumia Rais Magufuli hapa kwetu ni dikteta!

Katumia KDF kufanya kazi Professional na sio kupiga watu na kubangua Koroshow
See the difference

Sent from my TECNO CX Air using Tapatalk
Mtampamba sana Kenyata kwa kila sifa, ukweli ni kwamba wafanyakazi wakigoma ni kuongea nao na kusikiliza shida zao na sio kupeleka jeshi na kingine kulikua na ulazima wavae nguo za Jeshi?Arafu kumbe huko Kenya mnakosifia kila siku kumbe watu hawapewi mishahara?Ingekua bongo si mngeponda sana

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Stupid comment kama tanzania wafanyakazi wote waliogoma wangefukuzwa kazi na kutiwa ndani, kenya kuna sheria na demokrasia raisi anatafuta alternative route, lakini wafanyakazi wanaendelea kudai haki zao kwa dicteta wa tanzania hiyo ni kama ndoto
 
Mbona huko nyuma Tanzania ilishatumia jeshi wakati wa migomo ya madaktari.... Hii ya kudomba na kubangua KORO SHOW... Ndiko lilikuwa na question marks.
Question mark inatoka wapi?Jeshini kuna kila aina ya vitengo.Kuna skilled na non skilled labours. Kama kulikua na uhitaji wa kubangua korosho wangebangua tu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 

Kutumia jeshi siyo mbaya bali je hilo jeshi unalitumiaje?Kama unalitumia kwa manufaa pana ya wananchi ni sawa lakini kama unalitumia kukandamiza au kuua watu hiyo sio sahihi na haikubaliki.Tumia jeshi kwa manufaa pana ya kijamii.Viongozi wengine hutumia majeshi ya nchi zao kukandamiza na kunyamazisha fikra za raia zisisikike kwa walio wengi.Utaitwa Dikteta kama matumizi ya jeshi hilo yanenda kinyume na haki za binadamu kama tunavyoona kule algeria.
 
Stupid comment kama tanzania wafanyakazi wote waliogoma wangefukuzwa kazi na kutiwa ndani, kenya kuna sheria na demokrasia raisi anatafuta alternative route, lakini wafanyakazi wanaendelea kudai haki zao kwa dicteta wa tanzania hiyo ni kama ndoto
mbna unatukana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada ana mawazo finyu kama chama cha mapinduzi
kwa xbu hajaelekea kusema kile unachokipenda hapo hapo nyie ndo mnadai mnataka uhuru wa kutoa maoni, utapewaje huo uhuru kma huheshimu wa mwenzako kwa kutoa mitusi muda wote kuliko kumjibu mtu kwa hoja na kumrekebisha alipokosea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maghufuri ndo nani?
 
Mkuu unatanguliza mkokoteni mbele ya farasi. UK hakufukuza wafanyakazi, bali anahakikisha shughuli muhimu zinaendelea JKIA wakati wahusika wanaendelea kutafuta suluhisho na wafanyakazi. Kwa uzoefu wetu wa hapa , ndugu JPM angekuwa amevunja mifupa, fukuza na mengine mengi (na pia akiomba kuombewa) angepata changamoto aliyonayo UK.
 
acha uongo basi, wewe ndo ufanye utafiti na kufatilia habari, hata magazeti yao yameandika hata bbc imetangaza wewe hiyo uliko ipata kaa nayo tu mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Police wa Kenya hizo ndo unform zaoπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ sio jeshi
 
Ukiwa kiongozi sometimes you have to be aggressive,otherwise nchi haiwezi kutawalika...
 
kama demokrasia ipo kwa nini imefikia hadi wagome na maombi yao ni ya miezi mingine serikali hiyo hiyo ya UK haikutaka kuwasikiliza? na hadi kufikia kugoma walitoa taarifa ikapuuzwa. sioni haja ya kusifia UK.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama demokrasia ipo kwa nini imefikia hadi wagome na maombi yao ni ya miezi mingine serikali hiyo hiyo ya UK haikutaka kuwasikiliza? na hadi kufikia kugoma walitoa taarifa ikapuuzwa. sioni haja ya kusifia UK.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfanyakazi anaweza kugoma mahali ambapo hakuna demokrasia?
 
Kwa Sheria zetu za kazi hapa Tz hairuhusiwi mwajiri kuweka wafanyakazi mbadala pindi kunapo kuwa na mgomo. Sijui kwa Kenya ila nadhani ni ukiukwaji wa Sheria. Mgomo ndio silaha ya mwisho kwa mfanyakazi pindi anapo dai maslahi.
Haipendezi kwa mwajiri mkuu (Serikali ) kukiuka Sheria.
Kama Serikali itafanya hivyo itakuwaje kwa mwajiri binafsi?
Nadhani suluhisho ni kuingia katika meza ya majadiliano.
Vinginevyo basi jeshi waachiwe kufanya kila kazi za kiraia...jambo ambalo sio salama sana kwa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…