Uhuru Kenyatta: The New "Vasco Da Gama"?

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,296
Reaction score
18,027
Baada ya Rais Kikwete kustaafu, inaelekea Uhuru Kenyatta amempokea kijiti kwa safari sana nje ya nchi akiambatana na ujumbe mkubwa. Habari hizi zipo gazeti la Nation leo.

Ndani ya miaka miwili na nusu toka apate urais wa Kenya, kesha safari mara 43 ukilinganisha na safari 33 alizofanya mzee Mwai Kibaki katika miaka yote kumi ya uongozi wake.

Mwaka 2013 alifanya safari 18 mwezi mmoja baada ya kuapishwa. Dr. Magufuli hata safari moja bado. Mwaka huu, 2015 tayari amefanya safari 11, wastani wa safari moja kila mwezi.

Safari ya Paris majuzi kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi, alifuatana na ujumbe wa watu 43 akiwemo binti yake.
 
Kwani shida ipo wapi wacha afaidi urais maana 2017 Odinga ndo anakuja kummbwagaa mchana kweupe.
 
Upepo umegeuka naona, juzi alikuwa asifiwa hapa na wale jamaa wa mtaa wa pili sana tu
 
Kwani shida ipo wapi wacha afaidi urais maana 2017 Odinga ndo anakuja kummbwagaa mchana kweupe.

Mkuu, siasa za Kenya zina tofuati sana na za kwetu.

Tanzania ilikuwa suala la ufisadi zaidi. Halikuwa ni ukabila au udini. Kenya wameungana wakikuyu na kalenjin. Mjaluo Odinga hana chake.

Kwa maana hiyo, Kenyatta bado ana nafasi uchaguzi ujao. Kimbembe kitakuwa baada ya hapo. Kuna makubaliano kwamba umoja wa kikuyu/kalenjini umpe Willian Ruto. Lakini yanaweza kutokea ya Kikwete na Lowassa!
 
Only in East Africa.

East Africa ni shida. Kuna Rais wa kudumu Yoweri Museveni. Ameisha shuhudia kuapishwa kwa Mkapa, Kikwete na Magufuli na bado yupo tu.
 
Huyu Uhuru naye (kama alivyokuwa JK) ni rais mzigo. Wakati mashambulizi ya kigaidi yanafanyika kwenye chuo kikuu cha Mandera na zaidi ya wanafunzi 150 kuuawa, Uhuru alikomaa na ziara yake UAE alipokwenda kutazama mashindano ya F1 Abu Dhabi grand prix! Pia wakati mgomo wa walimu nchi nzima ukiwa umepamba moto mwezi September mwaka huu, Uhuru alifanya ziara ya kimatanuzi Italia kutazama mashindano ya Rome grand prix na kukutana na bosi wa Formula One!
 
Hapana aisee....Vasco hana mfano ...labda Vasco tumlinganishe na Emirate air ...
 

Hivi mkuu wajaluo na wakamba nao hawawezi kuungana kuwang'oa hao wakikuyu+kalenjin?
 
Akishapandisha handas hasikilizi ya mtu .btw Paris alikuwa na ngina? Binti mrembo yule..
 
Hapana aisee....Vasco hana mfano ...labda Vasco tumlinganishe na Emirate air ...

Hahahaaa

Vasco hana mpinzani.

Hata mwezi haujaisha tokea kuachia ngazi tayari keshaenda Afrika Kusini na Uingereza.

Wait....na Ethiopia tayari keshaenda eeh?

Natabiri katika miaka mitano ijayo atakuwa keshasafiri kwenda nje kuliko hata Magufuli mwenyewe.
 
Hivi mkuu wajaluo na wakamba nao hawawezi kuungana kuwang'oa hao wakikuyu+kalenjin?

Nadhani hawawezi. Ndiyo maana alliance ya wakikuyu na wakalenjin inaitwa the tyranny of numbers!
 

Itafika sehemu atabanwa tu. Kwenye retirement package ya former presidents kuna idadi ya safari kwa mwaka kwa fedha za walipa kodi.
 
Hivi mkuu wajaluo na wakamba nao hawawezi kuungana kuwang'oa hao wakikuyu kalenjin?

kikuyu 22%
Luhya 14%
lion 13%
kalenji12%
kamba6%
kisii6%

kwahiyo kama makabila hayo yana ujasiri wanaweza.tatizo ni kwamba karibu viwanda vyoote kenya rais wao kawekeza mwenyewe. Hataki shobo.

napesa na ana nguvu, ukijifanya unajua saana kumfuatafuata utaokotwa ufukweni asubuhi. Kama huamini kawaulize kamuulize Fatuh Bensuda kule zehegue, wale mshahidi wa ile kesi wako wapi? Atakupa jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…