Mjumbe wa kamati kuu ya ya CHADEMA Edward Lowassa amekuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kumpa pongezi nyingi mshindi wa kiti cha urais nchini Kenya Uhuru Kenyatta.
Itakumbukwa Lowassa alipanda ndege hadi nchini Kenya kumpigia chapuo Uhuru Kenyatta ambaye pia ni rais wa sasa wa nchi hiyo.
Lowassa amewahi kujitokeza hadharani mara nyingi akitangaza kumuunga mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi uliohitimishwa kwa Kutangazwa mshindi rais Uhuru Kenyatta. Soma;
Lowassa: Ninamuunga Mkono Kenyatta na nipo tayari kutoa msaada wakati wowote
Bila shaka siku ya kuapishwa mh Lowassa atakuwa miongoni mwa wageni wa heshima kabisa kwa kazi aliyoifanya ndani na nje ya Kenya.