Wewe unawezaji kufahamu kinachondelea sehemu za kazi ilhali wewe sio mfanyakazi bali mpigadebe wa siasa. Suala la kupambana na wafanya kazi hewa halijaanza leo, hata kitendo cha kulipa wafanyakazi kupitia benki ilikuwa ni kupambana na wafanyakazi hewa, enzi za kulipia dirishani ndilo ilikuwa mbaya zaidi, alikuwa akilipa dirishani fungu likabaki anaweka sahihi na kuishia nalo, na ilikuwa rahisi kuongeza majina hewa. Lakini kupitia benki, wafanyakazi hewa wanakuwa ni wale waliofariki, kustaafu au kuacha kazi ambap maafisa utumishi wamechelewa kuwafuta kwenye pay roll, kwa kuwa mshahara huo unaingia benki ni rahisi kuufatilia. Sasa kama kweli huyo unayemsifia anawajibika, twambie kawachukulia hatua gani watendaji waliosababisha mishahara hewa kulipwa, maana mtu hajilipi mshahara bali anajilipwa, hata mimi ningekuwa nafanya kazi halafu nikaacha, mshahara ukaendelea kulipwa, sio kazi yangu kumwuliza mlipaji kwa nini anendelea kukulipa, kazi yangu ni kuangali kila mwisho wa mwezi kama umeingia natoa haraka na kununua mifuko ya twiga cement na mabati.