Uhuru na Haki Haiwezi ikaleta Amani na Maendeleo ya Watu; Amani na Maendeleo ya Watu ni Tunda la Uhuru na Usawa

Uhuru na Haki Haiwezi ikaleta Amani na Maendeleo ya Watu; Amani na Maendeleo ya Watu ni Tunda la Uhuru na Usawa

Chadema imejipambanua kama chama kinachosimamia sera za kibepari hivyo tegemea katika utawala wake kuona matajiri wakirudi kushika nafasi tena kama watu wenye maamuzi katika jamii zetu.

Uhuru huu watu wa kada ya chini na Kati wanaofaidi kwa sasa utapotea na tutarudi katika minyororo ya manyanyaso ya wenye nacho.

Kwa kutambua agenda hii ya siri hutasikia Chadema ikinadi Sana sera zake ili kuficha uhakisia wake kwa wananchi waje kuwashtukiza tayari wakiwa madarakani.

Baadhi ya wafanyabiashara na mabeberu ndio wanaopush agenda za Chadema ili kurejesha ufalme wao walioupoteza katika awamu hii.

Ewe mwananchi tambua kuwa kuipa kura Chadema ni kukaribisha ubepari
Kiongozi gani ndani ya CCM ambaye siyo bepari?
Kashfa zote kubwa nchi hi, pamoja na uchafu wote, wizi wote na uhujumu uchumi mkubwa umefanywa na CCM kushiriki na na wageni.
Kuanzia kashfa ya Chavda Hadi ununuzi wa ndege umefanywa na CCM.
Hawa wezi wa Mali na rasilimali zetu ni majizi yanayotaka na kujipatia mitaji kinyume Cha Sheria.
Upepari ni mtamu bwana asikwambie mtu.
Wala ubepari sio dhambi ndio maana leo kuna Dar Es Salaam Stock Exchange, watu wakanunue hisa wamiliki sehemu ya makampuni.
Hiki kitu hakikuweko Zama za ujamaa.
Sijui Chama Cha Mazezeta mlisomea wapi hizo elimu zenu
 
Kama Gadaffi angetambua kuwa yeye ni sawa na wanaLibya wenzake na kwamba Libya ingeweza kutawala a na Mlibya mwingine pasipo yeye wala kijana wake, Libya ingebaki salama. Lakini kwa kuwa aliamini katika haki, aliona yeye anayo haki ya kuendelea kuiongoza Libya, na ndio mpaka sasa amani imekosekana Libya kwa sababu ya haki.
.
Huyu anayesema akiondoka mararakani hamna atakaye endeleza miradi yake Wala kufanya Kama yeye, je anatofauti gani na mtazamo wa Gadaffi?
 
Ujamaa ni katiba au ujamaa ni mfumo wa uchumi na utawala?

Mkuu umenisaidia kumuuliza Swali Muhimu sana ,Uchumi wa Soko ndio unaamua kila kitu yeye anabaki na Maandishi (Katiba) yalio pitwa na Wakati..

Na mimi nnalisubiria Jibu kutoka kwake.
 
Chadema imejipambanua kama chama kinachosimamia sera za kibepari hivyo tegemea katika utawala wake kuona matajiri wakirudi kushika nafasi tena kama watu wenye maamuzi katika jamii zetu.

Uhuru huu watu wa kada ya chini na Kati wanaofaidi kwa sasa utapotea na tutarudi katika minyororo ya manyanyaso ya wenye nacho.

Kwa kutambua agenda hii ya siri hutasikia Chadema ikinadi Sana sera zake ili kuficha uhakisia wake kwa wananchi waje kuwashtukiza tayari wakiwa madarakani.

Baadhi ya wafanyabiashara na mabeberu ndio wanaopush agenda za Chadema ili kurejesha ufalme wao walioupoteza katika awamu hii.

Ewe mwananchi tambua kuwa kuipa kura Chadema ni kukaribisha ubepari

Kumchukia Tajiri hakuwezi kumuongezea Masikini Kipato ,ni Masikini kuungana na Tajiri ili kujipatia Kipato na kukuza Uchumi wake.

Wananchi wa Hali ya chini hakuna wanacho faidi ktk Utawa huu wa CCM ,bado Kodi zao zina fujwa kwa kufanyika Miradi isiyo leta tija.Hebu fikiri unawezaje kutumia Kodi za Wananchi kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Chato !!!?.Kwa manufaa yapi kwa tija ipi jibu ni hamna ,wakati Pesa hizi hizi ungeweza kuzielekeza kwenye Elimu wapo Watoto ambao bado wanakaa chini/wanasomea nje/hawana Vyoo hakuna Walimu wa kutosha hamna Madawati nothing else.

Sasa hao Wanyonge unao wazungumzia ni wapi !?.Hizo ni Lugha tu za Siasa chafu ili kuwalaghai Wananchi.Wanyonge hao hao ndio mna wanyima Maji kisa hawa waungi Mkono ,huo ndio Ujamaa kweli Mkuu stroke ?
 
Basi kama Paka angeweza kuona kwamba Panya ni sawa na yeye, kwamba inamstahili Panya awe huru kutembea bila hofu ya kuliwa, Basi amani ingekuwepo kwa Panya na kwa Paka vilevile. Hatimaye maendeleo kwa Panya na Paka yangeweza kupatikana.

Uhuru na Usawa ni mbegu ya Amani!

..Sasa Paka atakula nini?

..Hebu tafuta mfano mwingine, kwa sababu huu uliotumia, hauendani na hoja unayojaribu kujenga.
 
Ujamaa ni katiba au ujamaa ni mfumo wa uchumi na utawala?
Bujibuji:

Nitakujibu kama ukiweza kuniambia Malamka ya wananchi ya kuunda serikali ni ya kikatiba au ni mfumo wa uchumi na utawala.
 
Kiongozi gani ndani ya CCM ambaye siyo bepari?
Kashfa zote kubwa nchi hi, pamoja na uchafu wote, wizi wote na uhujumu uchumi mkubwa umefanywa na CCM kushiriki na na wageni.
Kuanzia kashfa ya Chavda Hadi ununuzi wa ndege umefanywa na CCM.
Hawa wezi wa Mali na rasilimali zetu ni majizi yanayotaka na kujipatia mitaji kinyume Cha Sheria.
Upepari ni mtamu bwana asikwambie mtu.
Wala ubepari sio dhambi ndio maana leo kuna Dar Es Salaam Stock Exchange, watu wakanunue hisa wamiliki sehemu ya makampuni.
Hiki kitu hakikuweko Zama za ujamaa.
Sijui Chama Cha Mazezeta mlisomea wapi hizo elimu zenu
Bujibuji:

Huwezi kukaishafu kazi ya Musa akiwa mlima sayuni au kazi ya Mungu aliyoifanya ya kuandika amri zake, kwa kuzifanya kana kwamba hazipo eti kwa sababu kuna watu wanazivunja.

CCM ni Chama kikubwa sana Tanzania, kwa maana ya idadi ya wanachama wake kuwa wengi zaidi. Wapo wafisadi na wapo waadilifu mfano wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Na kashfa ulizozitaja hapo kuhusu ununuzi wa ndege, huna hoja ya kuthibitisha kwamba Kuna ufisadi ulifanyika hapo. Wakati mchakato mzima umeelekezwa kwa mujibu wa sheria na wawakiloshi wetu kwenye majimbo wanayafahamu haya.

Ubepari hauwezi kuwa dhambi, ni kwa sababu ni haki ya watu wa ulaya kuutumia lakini kama ukihitaji usawa hutaupata kwenye ubepari ila ni kwenye ujamaa.
 
Huyu anayesema akiondoka mararakani hamna atakaye endeleza miradi yake Wala kufanya Kama yeye, je anatofauti gani na mtazamo wa Gadaffi?
Bujibuji:

Hakuna kiongozi ye yote nje ya CCM ambaye ana maono juu ya usawa na uhuru wa watanzania wa makundi yote. Hii maana yake kiongozi mzalendo, muadilifu na mwenye hofu ya Mungu huwezi kumpata nje ya CCM.
 
Mkuu umenisaidia kumuuliza Swali Muhimu sana ,Uchumi wa Soko ndio unaamua kila kitu yeye anabaki na Maandishi (Katiba) yalio pitwa na Wakati..

Na mimi nnalisubiria Jibu kutoka kwake.
Nimeshamjibu mkuu Cyril tayari.
 
Kumchukia Tajiri hakuwezi kumuongezea Masikini Kipato ,ni Masikini kuungana na Tajiri ili kujipatia Kipato na kukuza Uchumi wake.

Wananchi wa Hali ya chini hakuna wanacho faidi ktk Utawa huu wa CCM ,bado Kodi zao zina fujwa kwa kufanyika Miradi isiyo leta tija.Hebu fikiri unawezaje kutumia Kodi za Wananchi kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Chato !!!?.Kwa manufaa yapi kwa tija ipi jibu ni hamna ,wakati Pesa hizi hizi ungeweza kuzielekeza kwenye Elimu wapo Watoto ambao bado wanakaa chini/wanasomea nje/hawana Vyoo hakuna Walimu wa kutosha hamna Madawati nothing else.

Sasa hao Wanyonge unao wazungumzia ni wapi !?.Hizo ni Lugha tu za Siasa chafu ili kuwalaghai Wananchi.Wanyonge hao hao ndio mna wanyima Maji kisa hawa waungi Mkono ,huo ndio Ujamaa kweli Mkuu stroke ?
Ciril:

Tajiri na masikini ni aina ya utabaka kwa kutegemea hali za watu kiuchumi. Na kwa msingi huo, pasipo kuwepo na usawa kuna baadhi ya huduma muhimu za jamii mtu masikini hataweza kuzipata, hivyo masikini huyo hawezi kuwa huru na kwa msingi huo hapawezi kukawepo na amani baina ya Tajiri huyo na masikini huyo.

Hivyo ujamaa na kujitegemea ndio njia ambayo itaweza kuondoa utabaka huo na kuwafanya watu wote ndani ya jamii kuwa sawa. Kuhakikisha kwamba huduma za jamii kama elimu bora, afya bora na maji safi na salama yanapatikana kwa watu wote ama awe tajiri au masikini.

Leo hii unashuhudia uwanja wa Ndege ndani ya Chato, huo ni usawa. Kama ingekuwa ni haki Chato wasingestahili lakini kwa kuwa ni usawa basi utakuja kushuhudia uwanja wa Ndege mkubwa ndani ya songwe ambao utaanza kazi zake siku za usoni, lakini pia uwanja mkubwa Tanga, Lindi, Mtwara na maeneo yote. Na jambo hilo haliwatasaidia watu wa maeneo hayo pekee bali ni kwa watanzania wote nchini, kwa kukuza pato la Taifa na kuongeza fedha za kigeni.

Na kazi ya kuijenga Hekalu sio kazi ya ya siku tatu, uwezo huo ni wa kinabii. Sisi kama binadamu inatubidi tuvuke zaidi ya siku hizo tatu, ila hatutasimama ila ni kuhakikisha Tanzania ina songa mbele na watanzania wanaendelea kiuchumi. Kazi hiyo itawezekana tu ikiwa tutalinda uhuru na usawa kwa watanzania wote.
 
Bujibuji:

Huwezi kukaishafu kazi ya Musa akiwa mlima sayuni au kazi ya Mungu aliyoifanya ya kuandika amri zake, kwa kuzifanya kana kwamba hazipo eti kwa sababu kuna watu wanazivunja.

CCM ni Chama kikubwa sana Tanzania, kwa maana ya idadi ya wanachama wake kuwa wengi zaidi. Wapo wafisadi na wapo waadilifu mfano wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Na kashfa ulizozitaja hapo kuhusu ununuzi wa ndege, huna hoja ya kuthibitisha kwamba Kuna ufisadi ulifanyika hapo. Wakati mchakato mzima umeelekezwa kwa mujibu wa sheria na wawakiloshi wetu kwenye majimbo wanayafahamu haya.

Ubepari hauwezi kuwa dhambi, ni kwa sababu ni haki ya watu wa ulaya kuutumia lakini kama ukihitaji usawa hutaupata kwenye ubepari ila ni kwenye ujamaa.
Kama Magufuli ni mwadilifu, aliwezaje kuuza nyumba za Serikali kwa Bei poa kwa kina kabula?
 
..Sasa Paka atakula nini?

..Hebu tafuta mfano mwingine, kwa sababu huu uliotumia, hauendani na hoja unayojaribu kujenga.
JokaKuu:

Mkuu, Paka itambidi ale chakula. Je, Panya ni chakula cha Paka?

Huo ni mfano tu, lakini nilichotaka kusema ni kwamba palipo na haki pana uonevu; lakini palipo na usawa uonevu hauwezi kuwepo.

Mfano; Kuna haki za watoto, haki za wazazi, haki ya mwanamke, haki ya walemavu, haki ya muuaji, haki mwizi, haki chungu mzima. Na ikiwa utahitaji kutekeleza haki ya upande mmoja ni lazima haki ya upande wa pili uangamizwe au ife kwa muda.

Kwa misingi hiyo upande mmoja utakosa uhuru na hivyo kukosa amani. Ukiwa unatekeleza haki ya mwanamke ni dhahiri kuwa haki ya mwanaume itagandamizwa. Maana yake mwanamke atapewa kipaumbele kuliko mwanamke, tayari umeshawaweka katika makundi mawili mwanamke na mwanaume. Lakini kama utaweka usawa baina ya mwanamke na mwanaume, hapa patakuwa na umoja na sio makundi. Maana yake mwanamke atatendewa sawa na mwanamke si kwa sababu ya jinsia yake bali ni kwa sababu ya utu na ubinadamu wake.
 
Kama Magufuli ni mwadilifu, aliwezaje kuuza nyumba za Serikali kwa Bei poa kwa kina kabula?
Bujibuji:

Moja ya ladha ya utawala wa sheria, huwa kuna kuwepo na uhuru wa kuzungumza wenye kudhibitiwa kwa mujibu wa sheria. Na hivyo kila utakachoongea ni lazima kiwe na ushahidi na huo ndio uhuru wa kuongea. Leta ushahidi hapa hadharani... au kama unafanya propaganda nikuache uendelee na kazi yako hiyo ya propaganda.
 
Tanzania siyo nchi ya kijana. Hakuna usawa Tanzania? Kwenye nchi za kijanaa watu hawabomoleani nyumba kama Kimara.
Angalia mshahara analipwa Raisi na viongozi wote wa juu linganisha na wa mwalimu ! Usawa upo wapi?
Tazama magari yao wanayotembelea na tunavyominyana sisi kwenye mwendokasi usawa upo wapi?
Nyumba za umma wameuziana na MAHAWALA ZAOhapo usawa upo wapi?
Kaangalie nyumba anayoishi ndugu ndugai na zile za wananchi wake kule KONGWA usawa upo wapi?
Yazama wananchi WALIPOKWA KOROSHO zao kifedhuli Kyle kusini afu twambie huo usawa upo wapi?
Angalia shule za kata na zile wanazosoma watoto wao.
UJAMAA SIYO KUITANA NDUGU NA KUSHIKA VIFIMBO KAMA NYERERE.
KASOME " KAPTULA LA MAX " KWA MAREJEO ZAID
 
Kinoamiguu:

Nazungumza kuhusu ujamaa na kujitegemea. Nazungumza kuhusu usawa na uhuru. Nazungumza kuhusu usawa katika mambo ya muhimu juu ya maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na Kodi kwa wafanyabiashara, huduma za upatikanaji wa elimu bora, afya bora na maji bila kusahau miundombinu ya uhakika na bora. Tunataka kuwepo na upangiliaji mzuri wa makazi katika maeneo yote nchini, sio tu kwa maeneo ya osterbay, masaki, gangilonga n.k ila ni maeneo yote.

Ujamaa haupendelei watu wavivu ila inathamini na kuheshimu kazi ya kila mtu ambayo anaifanya. Ujamaa na kujitegemea inajenga usawa na uhuru kwa watu wakulima na wafanyakazi. Ni lazima ufanye kazi uishi kwa kipato chako. Heshima ya binadamu haipatikani kwa kuwa na gari zuri, jumba zuri, au mshahara mnono. Heshima ya binadamu inapatikana kwa kupata huduma za muhimu ikiwa ni afya bora na chakula bora, elimu bora na maji safi na salama. Na ndio kwa sababu hiyo serikali inasisitiza usawa na uhuru.

Kumbuka kumchagua Rais Dkt. Joseph Pombe Magufuli na CCM ili iyaendeleze hayo kwa miaka Mitano mengine.
 
Pumba tupu
Vitabu vyenyewe vya dini vinakwambia
AMANI NI TUNDA LA HAKI
Ila wewe Mataga baada ya kupewa buku 7 unakuja kupinga pinga
Hivi siku hizi wanalipwa kabla ya kupost? Maana mlipaji angeona uharo Kama huu angerudisha mkono mfukoni.
 
Tofauti ya usawa na haki ni nini?
Je Tanzania kuna usawa? au kuna haki?
Tony92

Haki ni stahiki ya mtu na kwamba ni lazima aifaidi. Haki ni lazima iwe chini ya mamlaka ya mwenye nayo. Mfano, haki ya mtwa kumuamrisha mtumwa wake, na haki ya mtumwa kutumwa na bwana wake.

Usawa ni hali ya kuviweka vitu au watu katika daraja moja. Kwamba hakuna aliye juu ya mwenzake na wala aliyechini ya mwenzake. Kimahesabu kwa mfano, usawa ni 2 = 1, ambapo mbili ni mwanamke na moja ni mwanamke.

Kwa mujibu wa katiba yetu ya nchi ya 1997, ibara ya 3(1) na ibara ya 9. Tanzania ni nchi ya kijamaa na kujitegemea, na kwamba watu wake wapo huru na sawa bila kuwabagua katika makundi yao. Kukiwepo na usawa na uhuru ndani ya nchi, Haki haitafutwi. Maana yake Haki ni kasehemu kadogo sana ambacho kamejishika ndani ya uhuru... Ukiwa huru kutembea, ni dhahiri unayo haki ya kwenda mahala popote n.k
 
Back
Top Bottom