Uhuru Park Nairobi, Kenya nchi yenye uhaba mkubwa wa Ardhi, Vipi sisi Tanzania wenye ardhi tele na miji imejaaa Frame tupu?

Nchi inaongozwa kishamba sana ,miji imajaa maduka kila kona, yaani mtaani ambako mtu anapaswa kupmzika baada ya mihangaiko ya siku nzima ndio kwanza kumejaa nigjt club, viwanda, hapo ni mtaani makazi ya watu njoo sasa mjini kwenyewe
Yaani unashughuli zako mjini labda unasubiria jambo unakosa mahali pa kukaa kusubiria. Labda uingie bar
 
Nyerere pekee na wakoloni waliacha maeneo ya bustani na sehemu za huduma za mazoezi a utamaduni. Angalia mfano Russian Cultural Centre mjini na Vijana Kinondoni. Angalia Garden Posta, Viwanja vya Mnazi mmoja, Bustani mbele ya NBC Posta mpya, n.k.
Ila Mwinyi Snr, Mkapa na Kikwete wameharibu mipango miji na mazingira. Hasa Kikwetwe wakati wake wamejenga kila mahali na kuuza maeneo ya kupumzikia na michezo, maeneo ya shule na huduma zingine za jamii.
 
Kuna siku niliwaza maeneo ya mbezi Magufuli kwa nini wasipande mauwa au miti maeneo ya katikati ya barabara na yale maeneo ya pembezoni kuna kama kimlima kimeota majani hawayapalilii au kubuni muonekano wa kupendeza hata mtu akitoka Burundi ashangae lakini wapi.

Tanzania eeeh!!
Nchi yangu oooh!!
Ciiiciem oyeeh!!
Mitano tena jamani.
 
Hapo Uhuru Park tulienda kutalii 2010 na pisi nnayoiita wife sasa hivi.

Zanzibar wamejitahidi sana kwenye hili eneo, wako vizuri tofauti na bara.
 
Chama cha mapinduzi wanachofanya ni kuharibu nchi yote na kwa upande huo wanagawana maeneo na kwingine wanajenga maduka na kuyamilikisha ccm ili viwe vitega uchumi vya chama na kulinda eneo la wananchi.

Hii ni hatari kwa sababu pindi ikitokea chama kingine kuchukua hatamu basi ccm hawatakubali kwa kudai assets zao, wkt wanajua haikuwa yao ila wameiba from free area zone za wananchi.

Pamoja na nchi kukosa viongozi wenye uchungu na nchi yao, kimaendeleo na vinginevyo hatua ndogo za kulinda maeneo zingefanywa na hawa hawa waliopo ofisini kwa kusimamia sheria.
 
Mipango mingi na Halmashauri ndo kazi zao ila wamejizima data
 
Ukiona watu wanajazana kwenye frwm maana yake watu ajira hawana ni mwendo wa biashara. Biashara ya kupangisha frem inalipa, hasa maeneo ya town.
 
Arusha lilipo soko la Samunge ilikuwa ni open space mbunge mmoja wa viti maalumu CCM Magige Catherine alishauri lijengwe solo,kisa CHADEMA walikuwa wanafanyia mikutano
 
Watawala wa CCM hawana muda wa ku plan hayo mkuu, wao bora liende mradi madaraka wanayashikilia
 
Moshi town ipo Ila ni ya kitambo Sana same jina na hii ipo nyuma ya MC DC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…