Uhuru Park Nairobi, Kenya nchi yenye uhaba mkubwa wa Ardhi, Vipi sisi Tanzania wenye ardhi tele na miji imejaaa Frame tupu?

Uhuru Park Nairobi, Kenya nchi yenye uhaba mkubwa wa Ardhi, Vipi sisi Tanzania wenye ardhi tele na miji imejaaa Frame tupu?

Nchi inaongozwa kishamba sana ,miji imajaa maduka kila kona, yaani mtaani ambako mtu anapaswa kupmzika baada ya mihangaiko ya siku nzima ndio kwanza kumejaa nigjt club, viwanda, hapo ni mtaani makazi ya watu njoo sasa mjini kwenyewe
Yaani unashughuli zako mjini labda unasubiria jambo unakosa mahali pa kukaa kusubiria. Labda uingie bar
 
Tanzania Kuna ujinga mwingi sana ndugu yangu

Mimi nimekaa tu hapo msumbiji nchi masikin kabisa lakin inapangwa ikapangika kuanzia barabara mpaka hizo bustan ni nyingi sana kwa kila mkoa

Kwa mfano ukifika mkoa kama tete Kuna sehemu ya kwenda kufanyia mazoezi ambayo ni ya bure kabisa na ina kila aina ya kifaa cha kufanyia mazoezi ni bure kabisa lakin tanzania CCM wamekalia kuimba kura tu na kuuwa wapinzan wao huku wakisalimiana samaleko na tumsifu YESU KRISTO
Nyerere pekee na wakoloni waliacha maeneo ya bustani na sehemu za huduma za mazoezi a utamaduni. Angalia mfano Russian Cultural Centre mjini na Vijana Kinondoni. Angalia Garden Posta, Viwanja vya Mnazi mmoja, Bustani mbele ya NBC Posta mpya, n.k.
Ila Mwinyi Snr, Mkapa na Kikwete wameharibu mipango miji na mazingira. Hasa Kikwetwe wakati wake wamejenga kila mahali na kuuza maeneo ya kupumzikia na michezo, maeneo ya shule na huduma zingine za jamii.
 
Kuna siku niliwaza maeneo ya mbezi Magufuli kwa nini wasipande mauwa au miti maeneo ya katikati ya barabara na yale maeneo ya pembezoni kuna kama kimlima kimeota majani hawayapalilii au kubuni muonekano wa kupendeza hata mtu akitoka Burundi ashangae lakini wapi.

Tanzania eeeh!!
Nchi yangu oooh!!
Ciiiciem oyeeh!!
Mitano tena jamani.
 
Hapo Uhuru Park tulienda kutalii 2010 na pisi nnayoiita wife sasa hivi.

Zanzibar wamejitahidi sana kwenye hili eneo, wako vizuri tofauti na bara.
 
Chama cha mapinduzi wanachofanya ni kuharibu nchi yote na kwa upande huo wanagawana maeneo na kwingine wanajenga maduka na kuyamilikisha ccm ili viwe vitega uchumi vya chama na kulinda eneo la wananchi.

Hii ni hatari kwa sababu pindi ikitokea chama kingine kuchukua hatamu basi ccm hawatakubali kwa kudai assets zao, wkt wanajua haikuwa yao ila wameiba from free area zone za wananchi.

Pamoja na nchi kukosa viongozi wenye uchungu na nchi yao, kimaendeleo na vinginevyo hatua ndogo za kulinda maeneo zingefanywa na hawa hawa waliopo ofisini kwa kusimamia sheria.
 
Mipango mingi na Halmashauri ndo kazi zao ila wamejizima data
 
Ukiona watu wanajazana kwenye frwm maana yake watu ajira hawana ni mwendo wa biashara. Biashara ya kupangisha frem inalipa, hasa maeneo ya town.
 
Miji ya Bongo ni aibu tupu na kero, Dar jiji kubwa halina hata Garden ya kusingizia, Jiji limajaa Frame tupu, Aridhi tunayo nini kinashindikana?Kila sehemu ya wazi basi hio ni soko la wamachinga.

Nenda Arusha ni full majengo yalio jaa frame, eti Geniva ya Africa, Ardhi zilizo kuwa za wazi kwa sasa ni masoko ya wachuuzi, ujinga mtupu, nenda huko sijui Mwanza ni the same.

Kenya pamoja na kuwa na uhaba wa Aridhi Nairobi anngalau wana Uhuru park yao nzuri ambapo ingekuwa ni Tanzania in.
View attachment 3163561geisha badilishwa matumizi na kuwa soko la Wamachinga wauza bidhaa za China. Ukienda Mombasa kuna Gadeni, the same na Kisumu kote huko.

Sisi tuna kwama wapi? Aridhi si tunayo? shida ni ipi?
Arusha lilipo soko la Samunge ilikuwa ni open space mbunge mmoja wa viti maalumu CCM Magige Catherine alishauri lijengwe solo,kisa CHADEMA walikuwa wanafanyia mikutano
 
Kuna siku niliwaza maeneo ya mbezi Magufuli kwa nini wasipande mauwa au miti maeneo ya katikati ya barabara na yale maeneo ya pembezoni kuna kama kimlima kimeota majani hawayapalilii au kubuni muonekano wa kupendeza hata mtu akitoka Burundi ashangae lakini wapi.

Tanzania eeeh!!
Nchi yangu oooh!!
Ciiiciem oyeeh!!
Mitano tena jamani.
Watawala wa CCM hawana muda wa ku plan hayo mkuu, wao bora liende mradi madaraka wanayashikilia
 
Moshi town ipo Ila ni ya kitambo Sana same jina na hii ipo nyuma ya MC DC
 
Back
Top Bottom