Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kabla vita havijamalizika Israel imeshaweka tayari baadhi ya mipango yake ya siri dhidi ya ardhi za wapalestina, kwamba wanakusudia kuinyakua milele Gaza.
Uwezo wa kuinyakua Gaza umekwenda bila uzito mkubwa kutokana na kuwahadaa majirani na ndugu wote wa Palestina na wamekaa kimya katika muda muda wa kutoa msaada kwa wenzao hao.
Mara baada ya kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ndani ya mji mkuu wa Gaza, Jeshi la IDF liliwataka wapalestina wanaoishi eneo hilo kuelekea kusini. Ni ukatili sana hata kufikiria watu milioni 2.3 ambao tayari walikuwa wanaishi eneo dogo sana halafu kuwataka wakaishi pamoja kwenye nusu ya eneo walipokuwa awali.
Pamoja na hilo sambamba na kuuliwa wa kaskazini wale waliotii amri kuelekea kusini nao wamekuwa wakiuliwa njiani. Zaidi ya hivyo Jeshi la Israel limesema wakimaliza kaskazini ya Gaza itakuwa ni zamu ya kusini.
Kabla ya kumaliza huko kaskazini kumekuwa na mashambulizi mengi maeneo ya kusini ambako wapalestina wamekuwa wakifa kiwango cha chini kidogo kuliko kaskazini.
Itakapokuja zamu ya kusini watatakiwa waende wapi tena na idadi gani wataendelea kuuliwa kabla Israel kusimamisha mauwaji hao.
Kwa mtazamo wa haraka mzunguko huo wa mauaji kusini na kaskazini ya Gaza. Mashariki na magharibi ya Jerusalem hautakoma mpaka ardhi zote za wapalestina zitakapokuwa zimenyakuliwa. Bila msaada wa nguvu za kijeshi wapalestina peke yao hawataweza na hawana nguvu za kujitetea.
Watetezi wakubwa wa Palestina katika kipindi kigumu wangekuwa ni wale ndugu zao walio nje ya Palestina na ambao wamekosa huruma na umoja wa kuwaokoa. Tatizo halisi la kukosekana nguvu hizo wala sio wananchi wa nchi hizo bali ni Serikali zinazotawala ambazo zimeingia mikataba ya hadaa na Israel na hatimae kuamua kukaa kimya au kutoa matamko mepesi na yasiyokuwa na athari kwa uonevu uanaoendelea.
Nchi tatu miongoni mwa nyingi ambazo zimeonekana kusaidia maangamizi hayo ya Palestina na kushindwa kututea masjid Aqswa ambao utakatifu wake uko kwenye Qur'an ni Saudi Arabia, Misri na Jordan.
Hivyo ukombozi halisi wa Palestina utapatikana kwa kuondoka madarakani kwa Serikali za nchi hizo tatu.