Kama kawaida yenu wanaharakati kuchochea fitna na uharibifu zaidi katika nchi za kiislam huku nyinyi mkiwa mmekaa kwenye makochi yenu. Na baadhi ya wakubwa zenu wakiwa nchi za magharibi wakichochea vurugu na mapinduzi katika nchi za kiislam bila ya kujali umwagikaji wa damu na uharibifu utakaotokea huku wao wakiwa wametulia tu kwenye makochi yao.
Masjid Al Aqsa itakombolewa na Waislam, sio lazima wawe waarabu Salahuddin alikuwa ni Mkurdi na jeshi lake lilikuwa waislam waarabu na wasio waarabu, waliosimama sawa, wanaofuata Qur'an na Sunnah juu ya ufahamu wa wema waliotangulia. Sio mashia, wala ma ikhwaan wala mahizbu tahrir wala khawaarij kwa ujumla wao wala wanaopigania uarabu.
Cha msingi ni kuwaombea ndugu zetu Allah awanusuru na kuwapelekea misaada ya kibinaadamu kama chakula na matibabu kwa wenye uwezo na sisi tufuate njia ya wema waliotangulia na kurekebisha itikadi zetu ziwe sahihi na tushikamane na Tawhid na Sunnah na kuachana na Shirki na Bidaa. Soma Qur'an 24:55.
Huwa hatuangalii vyanzo vya matatizo yetu tunatafuta tu wa kuwalaumu na kuwashushia lawama. Haya yanatukuta kwa sababu ya kupuuzia dini yetu. Tulikuwa tuna nguvu kwa sababu ya kushikamana na dini yetu, kisha tukapata udhaifu baada ya kupuuza dini.
Hao mayahudi wenyewe miongoni mwao wanajua hili. Kuwa watakaowatoa pale ni waislam waliosimama sawa sawa. Na wanaogopa sana Waislam kushikamana na dini yao kiukweli hasa. Wala hawawaogopi wanaharakati wenye jazba za kijinga, bali huenda wanafurahi hasa mnapohamasisha kuzichoma moto nchi za kiislam na kuzitia kwenye machafuko ya kisiasa, ili kuzirudisha nyuma zaidi.
Hivyo, suluhisho ni tubadilike, ili tubadilishiwe hali yetu, soma Qur'an 13:11.
Maandamano ambayo nayo yana maovu mengi, jazba jazba hazisaidii bali huenda zikazidisha matatizo, Allah atunusuru.
Acheni kuendekeza jazba. Hamuoni yaliyotokea kwenye mapinduzi ya miaka ya karibuni katika nchi za kiislam? Hayakuongeza ila uharibifu na hayakupunguza ila zile kheri zilizokuwepo na amani.
Hamfikirii nyinyi wanaharakati?