Tanzania ni nchi ya mateso kupoteza muda na kuuwa vipaji.
Tuanze kwenye Matatu kila mtu anakaa vizuri na mziki plus tv. Hapa Tanzania kuanzia Dar es Salaam, Arusha, Mwanza usafiri wa Daladala ni kama Jehanam mnashindiliwa kama mnapelekwa kwenye Concentration camp za wakazi wa Nazis.
Njoo kwenye mabasi Kenya mtu anashinda Kisumu usiku anasafiri Asubuhi anafanya biashara Nairobi jioni anaondoka anaokoa gharama za muda na Hoteli. Tanzania itakuchukua siku nzima toka Arushahadi Dar itakubidi ulale na ukimaliza shuhuli huwezi kurudi inabidi ulale tena.