Kama mtu hana marafiki wengi, sio mtu wa kutoka sana lakini pia ana moyo mzuri. Siku zote hutengeneza bond kali sana na watu anaowapenda kwa sababu anakuwa real sana
Kipindi cha High school nilimpokea dogo wa form 5 ambaye baadae alikuwa kama mdogo wangu na tulivyofananana kutokana na kuwa na asili moja, watu hawakubisha hata nilipowadanganya kuwa tumeshea damu
Kwa ufupi jamaa ni loyal sana na hata nikiwa na shida hajawahi nitupa. Kwa hiyo hata kama nina marafiki wengine na ninaowachukulia kwa uzito kuliko yeye. Lakini nikihitaji mtu wa kumuamini kwa jambo lolote, yupo katika top 3 yangu daima
Ni sawa kuwa na mashaka lakini kama hajawahi kukuoneshea dalili zote mbaya. Usimshuku kwa sababu niamini, siku akijua na akikubadilikia utaimiss hiyo bond yake kwa sababu dunia ya sasa hakuna urafiki zaidi ya watu kuwa karibu yako kwa manufaa yao wenyewe. Kwa hiyo ukipata mtu anaekujali wewe kama binadamu pasipo kutaraji chochote toka kwako. Mshikilie na usimuumize maana upendo mkubwa siku zote hugeuka kuwa chuki kubwa. All the best