Uhusiano Huu na Huyu Mshikaji Unanipa Mshangao Mkubwa Sana

Uhusiano Huu na Huyu Mshikaji Unanipa Mshangao Mkubwa Sana

Ni kawaida kwakweli
Huenda mna bond nzuri sana na yeye ni kawaida yake kuwa mtu wa kujali kuliko wewe

Kuna watu wako hivo wakimuamini mtu hua wanajali sana
Huenda pia kunavitu vidogovidogo Huwa unamshauri kwako vilikuwa vya kawaida ila kwake vikawa na maana sana so anakuona kama mtumuhmu kwake
Kabisa Huwa namshauri na kumuonya baadhi ya mambo anapokengeuka
 
Ni upendo tu, usimfikirie vibaya

Huenda kwao yupo wa kiume pekee hivyo anakuona kama kaka

Nataman ningewapata watu kama hao ningejihisi mtu mwenye furaha maishani, upendo wao ni Genuine
 
Mtu hatari unatongozewa demu unaharibu??
Unatolewa out unakubali na unakunywa Kvant mixer kuzima??

Unanunuliwa vizawadi unapokea??

Unapigiwa siku kila asubuhi kijana ajaue mtu hatari kaamkaje??

Stuka, UTASHONWA
Hunijui una haki ku comment mkuu
 
Mh mapenzi ya dogo kwako yamezidi but i believe urafiki wa kweli upo
 
Sina mengi ya kusema zaidi ya kuwatakia kila la heri katika safari yenu ya urafiki mwema

1000012512.jpg
 
Itakua una maokoto/michongo zaidi ake,kwahiyo anakutumia kama sehemu ya mikakati yake mbeleni huko
 
Habari za saivi wakubwa
Kuna dogo bhana wa kiume alitokea kunikubali Sana Tena sana nimemzidi miaka kama mi 3 ivi alianza kunizoea Mimi nikawa namchukulia kama dogo

Alikuja kuniambia siku moja Kuna dada ake angependa niwe shemeji yake dada ake alikuwa sio haba kweli tukazama mapenzini na dada yake kiasi dogo akawa anachekwa kitaa na nyumbani Wana muattack kuwa anamtafutia dada ake mabwana ikaenda Mimi nikawa nampotezea maana nilikuwa karibu Sana na dada yake one day dogo alinilalamikia Sana kuwa dada yake ni wa kupita tu Mimi na yeye ushikaji sio wa kupita alilalamika mno kuwa kumpotezea sio fair

Ikaenda Mimi na dada yake tukaachana dogo kahangaika mno kutuunganisha ila wapi dogo alikuwa karibu na Mimi Sana Iko kipindi akimlaumu dada yake

Imeenda nae mahusiano yake yakawa Yana haribika namjenga na kumtia moyo Hadi Leo hii dogo Huwa Kila siku lazima anipigie simu akiamka kunijulia Hali mwanzo nilikuwa naona usumbufu now akipiga lazima nipokee

Akija mkoa nilipo lazima alete zawadi kwangu akija lazima anitoe out na atake tukae nae mda wote tunapiga story sasa Huwa najiuliza Mimi Nina kitu Gani special kinachofanya anithamini ivyo?
Men of colors mpo active
 
Back
Top Bottom