Uhusiano kati ya tasnia ya habari, uhuru wa kujieleza na dhana ya Haki za Binadamu

Uhusiano kati ya tasnia ya habari, uhuru wa kujieleza na dhana ya Haki za Binadamu

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Demokrasia dhidi ya uhuru wa kujieleza/vyombo vya Habari

Demokrasia sahihi hutegemea uhuru wa vyombo vya habari vinavyoweza kusimamia maslahi ya jamii. Kimsingi, haki zinazohusiana na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza bila ya kuingiliwa, kutafuta, kupokea, na kusambaza taarifa na mawazo ya aina mbalimbali kwa kufuata kanuni chache zilizowekwa, ni haki inayotambuliwa na sheria za kimataifa. Vyombo huru vya habari ni msingi muhimu wa kuhakikisha kupatikana kwa uhuru na haki hizi. Katika kuhakikisha hilo, dhima ya waandishi wa habari ni zaidi ya kazi yao; uandishi ni taaluma inayoweza kusaidia kupatikana kwa mitazamo na maoni ya aina mbalimbali kwenye nchi.

Vyombo vya habari hutoa fursa kwa watu kuhabarishwa na wao kuweza kujenga na kueleza mitazamo yao. Tasnia imara ya habari huwezesha jitihada za kushawishi kupatikana kwa hoja mpya na mabadiliko muhimu, na kufuatilia utendaji wa Serikali ili kuifanya iwajibike kwa wananchi wake.

Waandishi wa habari hutegemea taarifa kutoka kwenye vyombo na taasisi mbalimbali, na vyanzo vinavyoaminika (wakiwemo wafichua uhalifu mbalimbali) ili kuandaa habari na kuiarifu jamii. Sheria zinazowezesha (kuliko kuzuia) juhudi hizo ni muhimu katika utendaji wa waandishi na kushamiri kwa tasnia nzima ya habari. Kwa upande wao, waandishi wa habari na watendaji wengine kwenye vyombo vya habari wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wanafuata misingi na maadili ya taaluma zao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Hii ni pamoja na kutoa taarifa za uhakika, kufuata kanuni zote za maadili, na kuhakikisha uhuru wa kiutendaji kwenye tasnia ya habari.

MISINGI YA KISERA NA KISHERIA INAYOSIMAMIA TASNIA YA HABARI – KIMATAIFA

Mikataba mbalimbali ya kimataifa, bara na kanda inalinda tasnia ya habari, waandishi wa habari, na watetezi wa haki za binadamu kutoingiliwa na Serikali. Mikataba hiyo inaweka wajibu kwa Serikali kufuata, kuendeleza, na kulinda uhuru wa kutoa maoni na kujieleza.

TAMKO LA KIMATAIFA LA HAKI ZA BINADAMU (UNDHR)

Kifungu cha 19 cha Tamko hilo kinasema: Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutoa maoni na kujieleza; haki hii pia inahusisha uhuru wa mtu kuamini katika maoni yake bila kuingiliwa kwa namna yoyote, na uhuru wa kutafuta na kusambaza taarifa, maoni na mawazo yake kwa njia yoyote bila ya kujali mipaka
 
Upvote 0
Hakuna Uhuru wa habari usio na mipaka

Mfano Huwezi kwenda nchi za kiisllamu ukaandika makala ya kusifia uzuri wa nyama ya nguruwe

Na Huwezi kwenda andika Marekani kuwa Osama bin Laden alikuwa mtu mzuri Sana

Au ukaenda Israel ukaandika kuwa duniani Hakuna mtu mzuri Kama Hitler aliyeua wayahudi milioni 60

Uhuru wa kujieleza au kutoa habari una mipaka
 
Uhuru wa kujieleza usipokua na mipaka hata sisi wananchi wenyewe tutaanza kulalamika, imagine mtoto wako anatoa malalamiko ya kukosa nyama kwenye chakula mbele ya wageni.
 
JamiiTalks,
Tunachotakiwa kusema bila kuweweseka ni kwamba uhuru wa habari umepokwa nchi hii.
 
Uhuru wa kupata na kutoa habari ni haki ya msingi ya kila raia na hii inaenda sambamba na uhuru wa kujieleza.

Lakini kutokana na matukio ya waandishi wa habari kupotea na wengine kushambuliwa inatoa hofu kwa waandishi wa habari kutekeleza jukumu lao la kutoa habari kwa jamii kwa hofu ya kupata madhara au kuchukuliwa hatua kwa kuonekana eidha wanaandika habari ambazo zinaianika serikali au kufichua siri za watu fulani ambao wao hudhani wanatakiwa kufanya mambo yao bila kuguswa.

Vivyo hivyo inawawia vigumu raia kutoa mawazo aukujieleza kwa kuhofia kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa makosa ya kimtandao.

Hivyo basi naweza kuhitimisha kwa kusema kuwa pamoja na kuwa bado uhuru haujaondolewa kabisa ila kwa asilimia kubwa umeminywa sana.

NB Uhuru wa kujieleza unatakiwa kuwa na mipaka kufuata sheria na misingi ya habari kulingana na sheria za nchi MAANA UHURU BILA MIPAKA NI FUJO.
 
Uhusiano kati ya tasnia ya habari, uhuru wa kujieleza na dhana ya Haki za Binadamu ni Mapacha haviachani. Japo ni vyombo vichache vimetoa fursa ya kutoa maoni na kupokea Maoni. Bado tunahitaji vyombo vya habari vyenye kutoa Uhuru wa Kujieleza kama JamiiForums.

Haki za Binadamu wasiishie kutoa matamko bali watumie sheria zilizopo kutetea na kulinda Uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.
 
Jambo lolote hata uweke uhuru wa namna gani pasipokuwa na usimamizi linaleta majanga.

Tasnia ya habari ni moja ya nguzo/mhimili kwa baadhi nchi ila kutokana na kukosa usimamizi unakuta badala ya kujenga wanabomoa.

Tukizungumzia hapa Tanzania tumekuwa na uhuru mkubwa sana kwa media industry kiasi kipa mtu aliyepiyia na wasiopitia kuanzisha platform nk kwa ajili ya kuandika au kusamabaza habari mbalimbali zikiwa za ukweli, uongo, kufitinisha, kumjenga mtu kitu ambacho ni nje ya theory na tasnia hususi.

Sheria inapokuwepo inalinda na kusimamia kile kilichopewa uhuru kisizidishe au kutoka nje ya uhuru uliopewa.
 
Jambo lolote hata uweke uhuru wa namna gani pasipokuwa na usimamizi linaleta majanga.

Tasnia ya habari ni moja ya nguzo/mhimili kwa baadhi nchi ila kutokana na kukosa usimamizi unakuta badala ya kujenga wanabomoa.

Tukizungumzia hapa Tanzania tumekuwa na uhuru mkubwa sana kwa media industry kiasi kipa mtu aliyepiyia na wasiopitia kuanzisha platform nk kwa ajili ya kuandika au kusamabaza habari mbalimbali zikiwa za ukweli, uongo, kufitinisha, kumjenga mtu kitu ambacho ni nje ya theory na tasnia hususi.

Sheria inapokuwepo inalinda na kusimamia kile kilichopewa uhuru kisizidishe au kutoka nje ya uhuru uliopewa.
Point mkuu umeongea ... Hata Marekani japo wana uhuru wa kupata kusambaza habari kadiri inavyofaa na inavyowapendeza lakini haujapitiliza kiasi kwamba kuhatarisha ustawi wa jamii yao. Sisi huku kinachochangia watu kutaka kufukua hata habari nyeti za nchi kunaanzia kwa kutowajibika kwa baadhi ya viongozi....kutoa kauli tata na kuropoka sasa sintofahamu inaahamia kwa wananchi.
 
Hakuna Uhuru wa habari usio na mipaka

Mfano Huwezi kwenda nchi za kiisllamu ukaandika makala ya kusifia uzuri wa nyama ya nguruwe

Na Huwezi kwenda andika Marekani kuwa Osama bin Laden alikuwa mtu mzuri Sana

Au ukaenda Israel ukaandika kuwa duniani Hakuna mtu mzuri Kama Hitler aliyeua wayahudi milioni 60

Uhuru wa kujieleza au kutoa habari una mipaka
Kweli mkuu unatakiwa kuwepo muongozo unaosimamia uhuru huo, shida hapa kwetu ngoma ikilalia tofauti na upande wa serikali ndio muongozo unatumika..
 
Ahsante kwa taaarifa...

Ila uhuru na haki hua hazifuatwi kabisa... endapo maslahi ya watu fulani fulani yakiingiliwa....

Demokrasia hakuna...


Cc: mahondaw
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom