Ni dhahiri huujui ukristo kabisa.
Tofauti kubwa ya Uislam na ukristo ni kwamba ukristo unashughulika zaidi na roho wakati uislam unashughulika zaidi na mwili.
Agano la kale katika ukristo, kama ilivyo uislam, lilishughulika zaidi na mwili. Na Yesu, ambaye katika Biblia anaitwa NENO ( NENO alikuwako kwa Mungu, NENO alikuwa ni Mungu, aliyekuja kwa wanadamu wakashindwa kumtambua, wakashindwa kumpokea lakini waliompokea aliwapa uwezo wa kuwa wana wa MUNGU) alipokuja Duniani aliwafunulia wanadamu juu ya nini kilikuwa muhimu katika ufalme wa Mungu, ambacho ni ROHO na siyo MWILI.
Yesu hakuongelea ndevu, hakuongelea kubasi au kanzu kwa sababu alijua kabisa kuwa vitu hivyo ni vya kimwili na vinategemea mazingira ya mahali na wakati.
Kuvaa kanzu kwa wakati ule lilikuwa ni jambo la kawaida maana ndiyo lilikuwa vazi la wakati huo lililoendana na tamaduni za wakati huo. Ni vazi lililovaliwa hata na watu wasiomjua Mungu. Hakuna uthibitisho kuwa kulikuwa na mavazi mengine ya tofauti kwa wakati huo katika jamii husika.
Viatu vya wazi kwa sehemu za joto kama nchi za kiarabu inaeleweka. Lakini pia kutokana na teknolojia ya wakati huo, haionekani kulikuwa na viatu vya namna nyingine. Ni uwendawazimu mtu aishiye sehemu za baridi kali kuvaa kubasi eti tu kwa sababu mtume au Yesu alivaa kubasi.
Kwa enzi za Yesu na mtume, teknolojia na mazingira hayakuwa kama ya sasa, hata mashine au shaving foams na after shave havikuwepo. Hata nyembe hatuna uhakika kama vilikuwepo. Hakukuwa na sababu mtu anyoe kwa kisu butu halafu atokwe na upele. Busara ilikuwa kutokunyoa, ni busara ya kawaida. Lazima watu watofautishe nini ni mahitaji ya kawaida na nini ni mahitaji ya kiimani.
Wanaotaka kufuata maisha ya mtume, wasipande magari, wala ndege au engine boats maana mtume hakuwahi kusafiri kwa kutumia vyombo hivyo. Pia wasitumie hata laptop maana mtume hakuwa na computer wala simu ya mkononi.
WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.
Vazi kama kanzu kwa shekhe au kasisi ni vazi rasmi kwa kadiri ya taasisi zinazohusika zilivyoamua, sawa kabisa na sare za jeshi, majoho ya vyuo au jezi za wachezaji, lakini muundo wa mavazi hauna mchango katika core faith.
Kufuga ndevu hakuna mchango wowote katika wokovu wetu ndiyo maana hakuna maagizo kutoka kwa Mungu. Kuna watu waliokuwa wametoa maoni yao lakini Mungu hajatoa maelekezo kuhusu ndevu kwa sababu aliijua Dunia kabla haijaiumba, aliyajua mabadiliko ya Dunia na watu wake. Alitambua wanajme ambao hawatakuwa na ndevu. Maelekezo yake ya moja kwa moja ni kwa vitu vya kiimani, visivyobadilika. Alisema watu wasiibe. Wizi utaendelea kuwepo, utaendelea kuwaudhi na kuwaumiza wanadamu wakati wote japo vitu vitakavyoibiwa vitabadilika kutokana na wakati na mazingira ya mahali. Zwmani watu waliiba zaidi ng'ombe na mbuzi lakini leo watu wanaiba zaidi simu, laptops na fedha. Tanzania watu wanaiba zaidi simu lakini uarabuni watu huiba zaidi rasilimali za kuzalishia.