Uhusiano wa China na Afrika waweka mfano mpya wa ushirikiano wa Kusini na Kusini

Uhusiano wa China na Afrika waweka mfano mpya wa ushirikiano wa Kusini na Kusini

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
kusini.jpg

Uhusiano wa China na Afrika umeweka mfano mzuri wa kuigwa wa ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kuchukua nafasi muhimu sana katika kuendeleza mfumo wa usawa na jumuishi zaidi wa usimamizi wa dunia.

Rais na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Sera ya Afrika yenye makao yake makuu jijini Nairobi, Kenya, Peter Kagwanja, anasema utaratibu wa uongozi wa kimataifa uliopo sasa bado si wa haki na unahitaji sana mabadiliko, na mfumo wa Pendekezo la Usimamizi wa Dunia (GGI) ndio njia inayopasa kufuatwa ili kuleta mabadiliko hayo.

Pendekezo hilo lilitolewa na rais wa China, Xi Jinping, katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ulikofanyika mjini Tianjin Septemba Mosi mwaka huu, na kusifiwa sana na wataalamu wa Afrika. Pendekezo hili ni la nne la Dunia la kihistoria lililotolewa na Xi katika miaka kadhaa iliyopita, kufuatia Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.

Kagwanja amelielezea Pendekezo hili kama bidhaa bora ya kimataifa iliyotolewa na China kwa lengo la kuisaidia dunia kwenda mbele zaidi ya vitendo vya upande mmoja na dola moja kuwa juu ya dola nyingine, linakabiliana na upendeleo katika usimamizi, na linajenga hatma ya baadaye yenye usawa, haki na ustawi licha ya migogoro na sintofahamu iliyopo sasa.

Uhusiano kati ya China na Afrika pia unazidi kuwa wa kina kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ambapo nchi za Afrika na China zimeimarisha uratibu katika masuala muhimu ya maendeleo.

Profesa Kagwanja anaona kuwa, maendeleo ni njia ya amani nay a uhakika zaidi katika kupata maendeleo endelevu, na kwa kuunga mkono maendeleo, ujenzi wa amani ni sehemu kubwa, na China imechukua nafasi yake katika hilo. Anaita vitendo vya China kuwa ni diplomasia ya ukimya, kusaidia, na vyenye maana kuliko diplomasia ya kelele, ambavyo vinasaidia nchi Dunia ya Kusini kama Sudan Kusini na Somalia kupata suluhu ya migogoro ambayo ingeweza kugharimu mamilioni ya maisha ya watu.

Kwa mtazamo wake, Profesa Kagwanja anaona kuwa, maendeleo ya amani maana yake ni kufanya kazi kwa pamoja ili kupata ustawi wa kila mtu, na ni lazima maendeleo hayo yawe ya kunufaishana.

Katika ushirikiano na uratibu kati ya China na Afrika, China imechukua nafasi kubwa na muhimu sana. Katika nchi nyingi za Afrika, miradi mingi mikubwa ya miundombinu imejengwa, inajengwa, ana inatarajia kujengwa na kampuni za China. Tukichukulia mfano wa mradi wa reli ya SGR kati ya Mombasa na Nairobi, na ule wa barabara kuu ya Nairobi (Nairobi Expressway) nchini Kenya ambazo zimejengwa na kampuni za China, imekuwa ni alama ya miradi iliyoboresha maisha ya watu, na kuwa mfano halisi wa ushirikiano wa China na Afrika.

Wakati huohuo, kampuni nyingi za China zimejenga ama kuboresha zaidi ya kilomita 10,000 za njia ya reli, karibu kilomita 100,000 za barabara kuu, kujenga madaraja 1,000, banari 100, na kilomita 66,000 za njia za kusambaza na kupitisha umeme, na hivyo kutengeneza mishipa ya maingiliano katika bara la Afrika.

Uratibu na ushirikiano kati ya China na Afrika, ambao umedumu licha ya changamoto mbalimbali zinazotokea duniani, umedhihirisha tena kwamba ni wa kiufanisi, na kuweka mfano wa ushirikiano kati ya Dunia ya Kusini na mbali zaidi.
 
Back
Top Bottom