nisinge penda kuingilia kwa undani hii fani ya ushushu, nijikite kwenye mfumo wa kiutendaji.napingana na wanao sifia utendaji wa TISS, tutumie logic kufanya simple analysis.
1. Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani ingawa ina rasilimali nyingi.umasikini unatokana na ubovu wa mifumo mbali mbali ya uwendeshaji wa nchi, kama siasa na utawala,elimu afya,biashara na rasilimali, usalama(TISS) kwa hiyo umasikini wetu una uhusiano wa karibu kabisa na utendaji mbovu wa TISS, haiwezekani nchi ikawa ya mwisho duniani kwa umasikini alafu ikawa ya kwanza kwa inteligensia, inteligensia isiyoweza kuondoa umasikini haina umuhimu ni inteligensia ya majungu na umbea tu. nani anatembea na mke wa nani??.ankunywa bia ngapi baa??. hawana kitu hawa.. kama wanabisha waje mtaani tuwawape shule
2.inteligensia yetu kwa takribani miongo mitatu imejikita zaidi kenye mambo ya umbea na fitna na hujuma za kisiasa tu. kama nadanganya waje hapa watuambie ni lipe jema kwa nchii hii wamelifanya.wao kila kukicha ni kuhangaika na wapinzani wa serilali dhaifu na dhalimu tu. kuonyesha kuwa hawako makini angalia walicho mfanyia DK.ulimboka na Saidi kubenea
3.wakati wa awamu ya Mwalimu, tulikuwa na malengo tofauti na sasa hivi, kwanza kwa kuwa ndo tulikuwa tumepata uhuru kazi ya msingi ya TISS ya wakati huo ilikuwa ni kuimarisha mamlaka na madaraka ya taasisi ya utawala(Raisi) pili ikuwa ni kulinda uhuru na kuleta ukombozi kwa nchi za kiafrika, tatu kulinda falsafa iliyokuwa iliyokuwa inaongoza uchumi na siasa ya wakati ule "siasa ya ujamaa na kujitegemea" baada ya mageuzi ya kisiasa mwanzo mwa miaka ya 90 tulitakiwa kuifanyia mabadiliko makubwa ya kimfumo taaasisi ta usalama wa taifa,wao ndo walitakiwa washinikize mabadiliko, walitegemea wanasiasa ?? kama kweli ni intelligent, vinginevyo nao ni wananufaika na uafisadi tu.wameitelekeza taaluma yao. eti siku hizi na wao wanalamika. wanasahau kuwa wana nafasi kubwa ya kushinikiza mabadilko kuliko hata wabunge
3.tuige mfumo wa wenzetu wa wamarekani, twaweza boresha kulingana na mazingira yetu,tuigawanye taasisi katika idara tatu
a)secret service itayo husika na ulinzi wa raisi, makamu na waziri mkuu wa nchi na famila zao
b)upelelezi-itahusika na mambo ya criminal investigations na mengine mtaongeza wenye fani
c)ujasusi-usalama wa nje na ndani ya nchi, uchumi,siasa,utamaduni,utawala nakadhalika. hii idara itahisika kuangalia na kushauri usalama wa nchi, kiuchumi ,kisiasa na kiutmaduni
wao kama ni inteligent walitakiwa wawe wameyaona kabla, waforesee miaka 100 ijayo tunawategemea wao kwanza sisi baadaye,wafanye kazi zao ndo maana tumewapa kila kitu, haina maana sisi tuache kufundisha, au kutibu watu tuje kuwaambia cha kufanya