Uhusiano wangu na mwanamke wangu kipenzi umeingia doa, muda wowote nitakipoteza nilichokipenda kwa moyo wote

Uhusiano wangu na mwanamke wangu kipenzi umeingia doa, muda wowote nitakipoteza nilichokipenda kwa moyo wote

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,064
Reaction score
4,056
Habari

Ni kijana 25-27 years

Nina mpenzi Yuko chuo anamalizia mwaka wake wa mwisho.

Ninampenda na yeye alinipenda( kwa Sasa sijui make simuelewi elewi)
mpaka nikapanga akimaliza tu masomo yake nipeleke mahari kwao niishi nae.

Uhusiano wetu umedumu kwa mwaka mmoja Sasa.

Kuna taarifa mbaya nilizipata juu yake kuwa wakati akiwa likizo kwenye mafunzo ya vitendo, aliingia mapenzini na mtu mwingine mpaka akapata ujauzito then akauchomoa.

Chuo kimefunguliwa nikamtembelea nikawa nimepewa taarifa na mtu wake wa karibu kuhusu kilichotokea.

Nilimuuliza ila Cha kushangaza hakuonesha kushtuka kwanza aliniuliza Kama napenda kuambiwa ukweli au kudanganywa Kisha akasema nilichokisikia Ni ukweli na kuwa Yale yalishapita hivyo vyovyote nitakavyomchukulia Ni sawa tu.

Niko njiapanda sielewi nimuache vipi coz nampenda Sana
Na anachokionyesha Ni kuwa Yuko tayali kwa maamuzi yangu yoyote.

Mara ananimbia tuachane kisa amefikiria siwezi kumsamehe kwa alichokifanya.
Nifanyeje?

Asanteni.
 
At that age nakuelewa unavyojisikia. Ni umri ambao mapenzi huumiza zaidi ya kidonda. Hata ukiwasimulia watu na wakakupa ushauri unaona ni upuuzi maana hawahisi maumivu unayohisi wewe

Kama kweli unapenda kuambiwa ukweli na kama kweli upo tayari kuishi na consequences za ukweli wenyewe, huyo mwanamke hakufai achana nae. Angekua na hisia na mpango na wewe angejaribu kulipigania penzi lako kwake angalau kwa kukupoza kwa uongo kua hajawahi kukusaliti. Pole sana dogo.

Wewe sio wa mwanzo wala hautakua wa mwisho katika vijana wanaoumizwa hisia zao kiukatili kabisa na wenzi wao wasiojali. Pengine hutaelewa na hutakubaliana na ushauri mwingi utakaopewa humu lakini umri ukienda utaelewa kua mapenzi na ujana ni maji ya moto
 
Na anachokionyesha Ni kuwa Yuko tayali kwa maamuzi yangu yoyote.

Mara ananimbia tuachane kisa amefikiria siwezi kumsamehe kwa alichokifanya
Mbona majibu yako wazi? Ni ngumu sana ila jitahidi utaweza! Utaumia kwa muda ila wanawake wako wengi, mchukue hata Rafiki yake acha ujinga.....au huyo aliyekupa huo umbea pita nae huyo huyo

Siku chache tu atarudi kwako kwa machozi akiomba msamaha
 
At that age nakuelewa unavyojisikia. Ni umri ambao mapenzi huumiza zaidi ya kidonda. Hata ukiwasimulia watu na wakakupa ushauri unaona ni upuuzi maana hawahisi maumivu unayohisi wewe

Kama kweli unapenda kuambiwa ukweli na kama kweli upo tayari kuishi na consequences za ukweli wenyewe, huyo mwanamke hakufai achana nae. Angekua na hisia na mpango na wewe angejaribu kulipigania penzi lako kwake angalau kwa kukupoza kwa uongo kua hajawahi kukusaliti. Pole sana dogo.

Wewe sio wa mwanzo wala hautakua wa mwisho katika vijana wanaoumizwa hisia zao kiukatili kabisa na wenzi wao wasiojali. Pengine hutaelewa na hutakubaliana na ushauri mwingi utakaopewa humu lakini umri ukienda utaelewa kua mapenzi na ujana ni maji ya moto
Nashukuru mno kwa kujaribu kuelewa ninachokipitia.
 
Back
Top Bottom