Uingereza: Chris Whitty asema hakuna haja ya lockdown, wataishi na Corona kama mafua

Ww Dr au mganga wa kienyeji unayetushauri
 
Ajabu
 
Na ndio maana nikauliza, huku tulikoishi kama mbuzi, idadi ya waliougua na kufa kwa Corona, ni tofauti na huko walikofuata hizo precautions?
 
Watuige sana. JPM hakika alituokoa na siasa za dunia za COVID19. Amepigwa vita sana kwa kunenewa maneno mabaya kwa sera yake dhidi ya COVID 19. WaTanzania wezangu tuungane sera za JPM dhidi ya korona ziendelee.

Tunaanza kuwaona watetetea lockdown na chanjo wanaibuka kwa nguvu. Tuendelee kumuenzi kipenzi chetu aliyetutoka JPM.
 
Tutazidi kumkumbuka JPM wanafiki wote waliombeza JPM sasa wanafuata yale yale ya JPM,eh Mungu umpe pumziko la milele mja wako JPM,ametuonyesha njia dhidi ya mabeberu
 
Mhanga wa ujinga mwingine tena huyu kajileta. Hili la kuchanja na kutovaa na kuendelea kuvaa mask limeshaelezwa sana sana hapa na kila mahali ni kwa nini iwe hivyo. Sasa nyie vilaza mnaohangaika na habari za hovyo za kina Diamond hamuwezi kujua. Hata english yenu ni majanga. Nakupa homework ulizia watu wenye upeo ni kwa nini iwe hivyo. Mimi sina muda wa kurudia tena. Chanjo ni hiyo hiyo. Hakuna wa kukudhuru wewe na wengine ambao mnateketea kwa shida, vita na maradhi mengine. Wakitaka kutudhuru watasimamisha misaada tu na tutaisha wote. Usiwe kama nyumbu.
 
Na ndio maana nikauliza, huku tulikoishi kama mbuzi, idadi ya waliougua na kufa kwa Corona, ni tofauti na huko walikofuata hizo precautions?


Hapa hatuongelei juu ya idadi ya watu wakiokufa, tunaongelea juu ya tahadhari inayopaswa kuchukuliwa na serikali/Viongozi kukinga na hata kuwafariji raia wake kutokana na majanga.

Mfano, Kagera walikumbwa na janga asilia la tetemeko la ardhi, mkubwa yule alienda kwenye tukio huku Waathirika wakidhani wamekuja kufarijiwa na kupewa matumaini kinyume chake ilikuwa kejeli na masimango na kuvunjwa mioyo, eti wanaambiwa serikali haikuleta tetemeko na hakuna chakuka na masimango kadha wa kadha na hata fedha zilizochangwa kutoka nje na ndani ya nchi zililiwa au kutumiwa katika shughuli zingine, lakini yalipotokea mafuriko Msumbiji mara moja serikali ikapeleka misaada ya vyakula madawa na fedha!!!!, huu ni mfano mmoja kuonyesha jinsi Serikali ya Magu ilivyokuwa KATILI kwa raia wake na ndiyo maana hata CORONA akaiita "vimafua tu" huku roho zetu zikiangamia.

Ama kuhusu idadi ya watu waliokufa kwa Corona iwe ndogo au kubwa cha msingi ni je Serikali ilichukua hatua gani thabiti kupambana na CORONA ili kukinga raia wake, zipo nchi zilichukua hatua thabiti na zilikuwa ni mfano wa kuigwa duniani, mfano South Korea nk, pia zipo nchi zilichukua hatua lakini idadi ya watu waliokufa ikawa "Comparatively to us" kubwa licha ya kuchukua hatua, sasa hujiulizi kama wasingechukua hatua hali ingekuaje???.

Yapasa ujue kwamba Wazungu wanathiriwa sana na magonjwa ya jamii ya mafua ikiwemo hiyo Corona na hii ni kulingana na hali ya hewa ya huko kwao hiyo nayo imechangia pakubwa katika vifo vya CORONA sambamba na elderly aged kuwa wengi kuliko huku kwetu Africa, hivyo usisahau mazingira hayo mawili.

Juu ya yote serikali na viongozi makini ni wale wanaotaabika kushughulika na shida za watu wao kwa njia muafaka na katika muda muafaka.
 
Kama hatuongelei vifo na kuugua, tunachukua tahadhari ili kujiepusha na nini?!
 
Kama hatuongelei vifo na kuugua, tunachukua tahadhari ili kujiepusha na nini?!


Twende huko kwenye vifo.
Ni Idadi ya vifo na sio vifo, tofautisha idadi ya vifo na vifo.

Yaani kama Watanzania IDADI YETU YA VIFO ni ndogo kuliko kule ambako wamechukua tahadhari thabiti ya Corona na IDADI yao ya vifo ni kubwa basi sisi hatuna au hatukua na haja ya kuchukua tahadhari kama wao??!!----- hiyo kweli ni akili ya binadamu kamili???!!.

Maisha hata ya mtu mmoja yanathamani kubwa isiyopimika, assume ni wewe au mzazi wako, mwanao au mtu wako wa karibu sana awe ni miongoni mwa hao wachache waliofariki au watakaofariki utajisikiaje???--- jaribu kufikiri kwa kina rafiki yangu.

Kazi ya serikali ni ku provide wellbeing of its citizens at any cost, be it a citizen or half a citizen his/ her life matters to a keen government.

Tuache idadi tuzungumzie juu ya wajibu wa serikali, serikali inayowajibika ni sawa na yule askari aliyevuka the field of landmines akitumia metal detector na serikali isiyowajibika ni sawa na yule askari aliyevuka ile field recklessly na hiyo ndiyo ilikuwa serikali ya Magu in the case of Corona.
 
Siasa hizi.
 
Basi nadhani, no research, no right to speak, kaa kimya, acha kutupigia kelele, research kwanza.
Acha kutapata ili kutetea upumbavu wa Marehemu Mfalme JUha! Nimeshasema unaojaribu kuwatetea WANAFICHA UKWELI! Wewe unayesema kwamba eti "Mbona TZ wapo vizuri" huku ukimpamba Jiwe, ndie unatakiwa kutoa takwimu kwa sababu kila mwenye akili timamu anafahamu kwamba Tanzania hawafanyi testing wala kutoa hizo takwimu! Wewe ndie umekuja na habari za RITA! Na ni wewe ndie umekazania kwamba Tanzania waathirika ni wachache! Weka hapa hizo takwimu vinginevyo, acha kulinganisha taifa linaloficha uhalisia na wale wanaoweka mambo ya wazi! Na ukijua hilo, ndipo utajua wewe ndie unatakiwa kupiga kimya!!!
 
Waingie step 2 kwa kupiga chini na hiyo michanjo fake waje bongo wajifunze tunavyoishi na virusi vya corona ka vile kule usukumani wanavyolala na mifugo sebulen. Ajaribu mzungu kuishi hata na kukutu tu chumba kimoja aone matokeo yake.
R.I.P Magufuli the Great!
 
Okay, kama swala ni idadi ya vifo as you put it, then wafanya maamuzi tungependa kujua, idadi ya vifo huko walikochukua precautions, na sisi huku mnakodai tunapuuzia, viko tofauti?
 
Huna data, huna taarifa, na hutaki kuzitafuta kwenye mamlaka husika, sasa nina nini cha kujadili na wewe? Kaa kimya hadi utapofanya research.
 
Huna data, huna taarifa, na hutaki kuzitafuta kwenye mamlaka husika, sasa nina nini cha kujadili na wewe? Kaa kimya hadi utapofanya research.
Unatia huruma sana!!! Ikiwa unashindwa kuelewa hata post fupi iliyoandikwa kwa Kiswahili, una kipi unachokielewa?! Nimeshakuambia:-
Sasa utatafutaje kitu ambacho hakipo na nimeshakueleza takwimu za mwisho zimetolewa April 2020? Wewe uliyeleta habari za RITA kwamba--
Labda nikuulize kivingine, kwa mujibu wa data za wasajili wa vizazi na vifo(RITA), idadi ya watu waliokufa kabla ya Corona kwa mwaka na idadi ya watu waliokufa baada ya corona kwa mwaka, ina utofauti?
Weka hapa hizo takwimu unazosema "kwa mujibu wa data za RITA"!!! Nini kinakushinda wakati ni wewe mwenyewe ndie umesema "kwa mujibu wa data za RITA?! Yaani RITA uitaje wewe halafu unaniambia mimi ndie nikutafutie wakati nimeshakuambia hakuna!!! Weka hizo za "kwa mujibu wa data za RITA" na kama usinipotezee muda wangu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…