Uingereza kama demokrasia imepitiliza sasa. Keir Starmer njoo Africa utafurahi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Waingereza wamemtimua kazi Waziri Mkuu wao lakini sasa wanabishana walichomfukuzia kazi Keir Starmer ni kipi hata wenyewe hawaelewi!

Haieleweki kwa nini amelazimishwa kujiuzulu na chama chake alichokiongoza kwenye ushindi mkubwa huku akitimiza ahadi zote alizoahidi.

Keir Starmer aje Africa, kwa rekodi yake anakuwa rais au waziri mkuu wa maishe milele popote Africa.

Soma pia
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ajiuzulu

1782454171061.png
 
Mi mwenyewe naanza kuona hii level ya demokrasia ni ujinga.
Unaona demokrasia ya uchawa ndo akili. Hao waingereza kutokana na akili zao hizo ndo waliitawala dunia. Umeshawahi sikia uwingereza inateteleka kwa ajili ya kubadili viongozi. Mifumo yao ya kiutawala haiyumbishwi na mtu mmoja kisa ni Rais au waziri mkuu. Huku Afrika ndo mnaona demokrasia ni mbaya kwa sababu ya ujinga wa kufikiri Rais ni sawa na Mungu.
 
Yaani rafiki yako amefeli vetting ya ubalozi alafu wewe unampitisha,wai gereza hawana katiba ya kukulinda lazima usepe.
Huyu rafiki yake aliyempitisha kuwa balozi wa UK kule US Peter Mandelson hakukizi vigezo na ku-pass high level security clearance. Yeye Keir kama akalazimisha.

Pia anaskendo nyingi zikiwepo kutoa taarifa za siri kwa washikaji zake kama Epstein.

Ushawishi wake kwenye jamii umepungua. Vyama vipya vinaongeza ushawishi na kuungwa mkono. Wapiga kura wanahama kutoka labour kwenda Green, Chama cha Farage na Store.

Gharama za maisha kupanda, mfumuko wa bei, issue za wahamiaji haramu, matokeo ya kura za uchaguzi wa mitaa.
 
Unaona demokrasia ya uchawa ndo akili. Hao waingereza kutokana na akili zao hizo ndo waliitawala dunia. Umeshawahi sikia uwingereza inateteleka kwa ajili ya kubadili viongozi. Mifumo yao ya kiutawala haiyumbishwi na mtu mmoja kisa ni Rais au waziri mkuu. Huku Afrika ndo mnaona demokrasia ni mbaya kwa sababu ya ujinga wa kufikiri Rais ni sawa na Mungu.
Demokrasia ya ujinga. Uingereza ile iliyokuwa na empire imeenea duniani kote ingekuwa na hii demokrasia isingeweza kutawala chochote. Miaka kumi mawaziri wakuu 7!! Kama siyo ujinga ni nini? Watu mambo yamekuwa magumu, badala ya kubadilika nchi yao ijikwamue wao wanaanza kupigizana kelele na kunyosheana vidole.
 
Ndiyo upande wa pili wa gharama ya demokrasia hiyo.Usipoenda nayo kwa mahesabu na akili ndipo utahesabika ni kichaa.
 
Huyu rafiki yake aliyempitisha kuwa balozi wa UK kule US Peter Mandelson hakukizi vigezo na ku-pass high level security clearance. Yeye Keir kama akalazimisha.

Pia anaskendo nyingi zikiwepo kutoa taarifa za siri kwa washikaji zake kama Epstein.

Ushawishi wake kwenye jamii umepungua. Vyama vipya vinaongeza ushawishi na kuungwa mkono. Wapiga kura wanahama kutoka labour kwenda Green, Chama cha Farage na Store.

Gharama za maisha kupanda, mfumuko wa bei, issue za wahamiaji haramu, matokeo ya kura za uchaguzi wa mitaa.
Kuhama Chama kwa wapiga kura kwa wenzetu sio kosa ngoja itokee TZ sasa hiyo kelele yake utazania mtu kaua.
 
Waingereza wamemtimua kazi Waziri Mkuu wao lakini sasa wanabishana walichomfukuzia kazi Keir Starmer ni kipi hata wenyewe hawaelewi!

Haieleweki kwa nini amelazimishwa kujiuzulu na chama chake alichokiongoza kwenye ushindi mkubwa huku akitimiza ahadi zote alizoahidi.

Keir Starmer aje Africa, kwa rekodi yake anakuwa rais au waziri mkuu wa maishe milele popote Africa.
Hili ndilo tatizo kubwa waliloliona kina Socrates kuhusu demokrasia miaka 500BC. Kuruhusu watu wote kushiriki maamuzi waliona ni tatizo kubwa. Wengi hawana uelewa.

Leo hii nchi nyingi za magharibi zikiwemo Marekani na Ulaya zimejaa watu wenye uelewa finyu (low literacy) na jazba nyingi wanaofanya maamuzi kwa hisia wakighilibika kirahisi na watu wenye pesa na propaganda za agenda za siri. Wanashambulia viongozi wa maana kwa maslahi yao na kukumbatia wahuni.

Kwa mfano UK leo hii wameanza kusikitika kuhusu uamuzi wao wa BREXIT miaka 10 iliyopita. Waliowaghilibu (kina Boris Johnson) wameshafanikisha maslahi yao na kuingia mitini. Nigel Farage wa UKIP leo anajibaraguza kama hakuhusika vile. Tokea hapo waweacha kiti cha Waziri Mkuu wa UK katika vurugu zisizo na mwisho (total turmoil). Kila anayekikalia ama anajiuzulu au kutimuliwa kama mchezo wa kamari. Anayemaliza au kuvuka mwaka ni bahati.
 
Kuna haja gani ung'ang'anie madaraka na walioko nyuma yako hawakukubali? Jamaa kacheza kete ya maana sana na ni mfano wa kuigwa lakini sisi huku kuna watu wanaona ni ujinga.
Kwenye uongo-zi lazima ukubalike japo kwa 51% na sio 49% kurudi chini. Achana na hawa wetu wanaodai wanakubalika kwa 97% na ni 16% ndo inawakubali wanaamua kulazimisha watu kwa mitutu wawakubali shenzi type
 
Hapo bongo kiongozi mkuu hawezi kujiuzulu vile, ataonekana ni msaliti ameusaliti mtandao uliomuweka madarakani, watammaliza mapema tu
 
Hili ndilo tatizo kubwa waliloliona kina Socrates kuhusu demokrasia miaka 500BC. Kuruhusu watu wote kushiriki maamuzi waliona ni tatizo kubwa. Wengi hawana uelewa.

Leo hii nchi nyingi za magharibi zikiwemo Marekani na Ulaya zimejaa watu wenye uelewa finyu (low literacy) na jazba nyingi wanaofanya maamuzi kwa hisia wakighilibika kirahisi na watu wenye pesa na propaganda za agenda za siri. Wanashambulia viongozi wa maana kwa maslahi yao na kukumbatia wahuni.

Kwa mfano UK leo hii wameanza kusikitika kuhusu uamuzi wao wa BREXIT miaka 10 iliyopita. Waliowaghilibu (kina Boris Johnson) wameshafanikisha maslahi yao na kuingia mitini. Nigel Farage wa UKIP leo anajibaraguza kama hakuhusika vile. Tokea hapo waweacha kiti cha Waziri Mkuu wa UK katika vurugu zisizo na mwisho (total turmoil). Kila anayekikalia ama anajiuzulu au kutimuliwa kama mchezo wa kamari. Anayemaliza au kuvuka mwaka ni bahati.
Sahihi mkuu, suala la kuachia kila mtu awe kwenye nchi apige kura lina changamoto zake nyingi sana kwa sababu kuna watu ni vilaza haswa hawaelewi chochote, tatizo ni kwamba nayo jinsi ya kuchuja wapi wapewe kipaumbele katika maamuzi ya kidemokrasia kama hayo ya kupiga kura ni mtihani mwingine.
 
So
Hili ndilo tatizo kubwa waliloliona kina Socrates kuhusu demokrasia miaka 500BC. Kuruhusu watu wote kushiriki maamuzi waliona ni tatizo kubwa. Wengi hawana uelewa.

Leo hii nchi nyingi za magharibi zikiwemo Marekani na Ulaya zimejaa watu wenye uelewa finyu (low literacy) na jazba nyingi wanaofanya maamuzi kwa hisia wakighilibika kirahisi na watu wenye pesa na propaganda za agenda za siri. Wanashambulia viongozi wa maana kwa maslahi yao na kukumbatia wahuni.

Kwa mfano UK leo hii wameanza kusikitika kuhusu uamuzi wao wa BREXIT miaka 10 iliyopita. Waliowaghilibu (kina Boris Johnson) wameshafanikisha maslahi yao na kuingia mitini. Nigel Farage wa UKIP leo anajibaraguza kama hakuhusika vile. Tokea hapo waweacha kiti cha Waziri Mkuu wa UK katika vurugu zisizo na mwisho (total turmoil). Kila anayekikalia ama anajiuzulu au kutimuliwa kama mchezo wa kamari. Anayemaliza au kuvuka mwaka ni bahati.
Huyo Socrates mfumo aliokuwa anautaka pia hauna mapungufu!?? Mimi nadhani ujamaa ni hatari kubwa zaidi Duniani
 
Vitu tofauti.

Demokrasia sio sawa na au kinyume cha ujamaa. Ni kuhusu mfumo wa kufanya maamuzi na kuchagua viongozi katika jamii au taifa.

Socrates, Plato, Aristotle na wanafalsafa wengine waliishi Ugiriki zaidi ya miaka 400 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu. Tawala zilizokuwepo enzi hizo ni za kifalme za vizazi kupokezana. Wao waliona sio sahihi bali wananchi wenyewe ndio wachague na kuamua masuala makuu katika jamii/nchi. Hiyo ndiyo maana halisi ya neno 'demokrasia'. Ifanyikeje? Ndio uliokuwa mjadala wao mkuu.

Leo hii demokrasia inatumika katika mifumo yote ya kiitikadi iwe ujamaa, ubepari, ukomunisti, n.k. kwa viwango tofauti tofauti. Hata Korea ya Kaskazini inajiita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea. Kuna uchaguzi wa wawakilishi kule.
 
Hili ndilo tatizo kubwa waliloliona kina Socrates kuhusu demokrasia miaka 500BC. Kuruhusu watu wote kushiriki maamuzi waliona ni tatizo kubwa. Wengi hawana uelewa.

Leo hii nchi nyingi za magharibi zikiwemo Marekani na Ulaya zimejaa watu wenye uelewa finyu (low literacy) na jazba nyingi wanaofanya maamuzi kwa hisia wakighilibika kirahisi na watu wenye pesa na propaganda za agenda za siri. Wanashambulia viongozi wa maana kwa maslahi yao na kukumbatia wahuni.

Kwa mfano UK leo hii wameanza kusikitika kuhusu uamuzi wao wa BREXIT miaka 10 iliyopita. Waliowaghilibu (kina Boris Johnson) wameshafanikisha maslahi yao na kuingia mitini. Nigel Farage wa UKIP leo anajibaraguza kama hakuhusika vile. Tokea hapo waweacha kiti cha Waziri Mkuu wa UK katika vurugu zisizo na mwisho (total turmoil). Kila anayekikalia ama anajiuzulu au kutimuliwa kama mchezo wa kamari. Anayemaliza au kuvuka mwaka ni bahati.
Karma hii acha wavurugane tu.

Hawa wamagharibi wamevuruga mataifa mengi sana huku 'Global South ' kwa hila zao na hata kushiriki kupindua na kuua viongozi wasiowataka wao.
 
Back
Top Bottom