Vitu tofauti.
Demokrasia sio sawa na au kinyume cha ujamaa. Ni kuhusu mfumo wa kufanya maamuzi na kuchagua viongozi katika jamii au taifa.
Socrates, Plato, Aristotle na wanafalsafa wengine waliishi Ugiriki zaidi ya miaka 400 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu. Tawala zilizokuwepo enzi hizo ni za kifalme za vizazi kupokezana. Wao waliona sio sahihi bali wananchi wenyewe ndio wachague na kuamua masuala makuu katika jamii/nchi. Hiyo ndiyo maana halisi ya neno 'demokrasia'. Ifanyikeje? Ndio uliokuwa mjadala wao mkuu.
Leo hii demokrasia inatumika katika mifumo yote ya kiitikadi iwe ujamaa, ubepari, ukomunisti, n.k. kwa viwango tofauti tofauti. Hata Korea ya Kaskazini inajiita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea. Kuna uchaguzi wa wawakilishi kule.